Anayejua Rais Magufuli anatupeleka wapi atuambie, naona kama tumepotea

Status
Not open for further replies.
imani yangu.. magufuli anapewa lawama sababu tu raisi... ila wanaomharibia ni watu wake wa karibu... yeye ana nia nzuri sana na nchi ila kuna wale wanaotaka ashindwe na ndo wanasababisha kero zote hz..!
 
Umepata like zakutosha ila nizakinafiki. Umepotea mwenyewe.

Nimesoma baadhi ya post na mada zako, nashindwa kuelewa inawezekanaje mtu mwenye akili timamu na mwenye utu kuthubutu kutetea baadhi ya mambo na kauli za Mh Rais wetu.

Ukijaribu tu kushirikisha brain yako, je ni nani hasa kati ya alivyevaa kiatu na Mkuu wa nchi anayejua wapi kiatu kinabana na pia maumivu yake? Kati ya mwananchi anayekula mlo mmoja kwa saa 24 na Rais wa nchi nani anayejua makali/maumivu? Siasa na takwimu zisizo na uhusiano wa moja kwa moja na maisha halisi ya Mtanzania hazitufai na tunazikataa.

Tanzania kuna ukame. Tanzania kuna njaa. Hilo halihitaji mjadala wala idhini ya Rais au binadam yoyote kulibaini na kulifanyia kazi.
 
imani yangu.. magufuli anapewa lawama sababu tu raisi... ila wanaomharibia ni watu wake wa karibu... yeye ana nia nzuri sana na nchi ila kuna wale wanaotaka ashindwe na ndo wanasababisha kero zote hz..!

Hakuna kitu kibaya na hatari kama "nia njema". Maovu mengi na uharibifu mwingi na mkubwa katika historia ya mwanadamu umefanyika kwa "nia njema". Ndio maana ninyi mnaotumia hisia kutazama au kuchambua mambo mnajikwaa na kuanguka hapo mara nyingi.
 
kwahiyo mkuu unataka kusema.. ukiwa na nia njema ndo chanzo cha majanga!
 
kwahiyo mkuu unataka kusema.. ukiwa na nia njema ndo chanzo cha majanga!

Historia ndio msemaji.

Madikteta karibu wote, vita nyingi na maamuzi mengi mabovu mengi yalitendwa kwa "nia njema". Ni mara chache sana ambapo watendaji hawakuwa na "nia njema"
 
Mwl Nyerere aliwahi kusema "hatuwezi kuwa na rais ambaye hatujui kesho ataamka amefikiria nini au ameshauriwa nini na mke wake". Kwa wakati ule kilionekana ni kijembe kwa mzee Mwinyi lakini leo kauli yake inaonyesha maana.

Hatujui mwelekeo wa nchi kiukweli hatujui kesho atafukuzwa na nani au ziara ya rais au waziri mkuu itakuwa wapi. Hatujui kama tutaamka tunafagia barabara au tutaingia ofisini kwetu kama kawaida.

Hatujui tunaanza na nini, kujenga viwanda au kuboresha miundombinu na kuimarisha kilimo ili tupate malighafi.

Hatujui tatizo la sukari kwa mfano linaondoka kwa kurekebisha viwanda vyetu na kuongeza uzalishaji wa miwa au kuruhusu sukari ya nje au tuvamie magodauni ya watu

Ukimuangalia usoni na ukasikia anachotamka unakiri ana nia kabisa ya kututoa hapa. Swali ni je? anajua jinsi ya kututoa?

Anajua anakotupeleka? Nimejitahidi kuangalia bunge ili nione labda mawaziri wake wanaweza kuonyesha mwelekeo, huko nikachanganyikiwa zaidi.

Mwanamtandao mmoja alisema unaweza kuwa na dereva mzuri anayefuata sheria zote za barabarani lakini hajui anaenda wapi!
Hata Magufuli mwenyewe hana uhakika na wapi anakotupeleka. Kapoteza dira, hana mipango zingatifu, hashauriki, amejaa vitisho, ghiliba na visasi na hatabiriki. Bila shaka anatumia ndoto kufanya maamuzi!
Inaweza kuchukua muango mzima kurekebisha uharibifu alioufanya kwa mwaka mmoja!
 
Mwl Nyerere aliwahi kusema "hatuwezi kuwa na rais ambaye hatujui kesho ataamka amefikiria nini au ameshauriwa nini na mke wake". Kwa wakati ule kilionekana ni kijembe kwa mzee Mwinyi lakini leo kauli yake inaonyesha maana.

Hatujui mwelekeo wa nchi kiukweli hatujui kesho atafukuzwa na nani au ziara ya rais au waziri mkuu itakuwa wapi. Hatujui kama tutaamka tunafagia barabara au tutaingia ofisini kwetu kama kawaida.

Hatujui tunaanza na nini, kujenga viwanda au kuboresha miundombinu na kuimarisha kilimo ili tupate malighafi.

Hatujui tatizo la sukari kwa mfano linaondoka kwa kurekebisha viwanda vyetu na kuongeza uzalishaji wa miwa au kuruhusu sukari ya nje au tuvamie magodauni ya watu

Ukimuangalia usoni na ukasikia anachotamka unakiri ana nia kabisa ya kututoa hapa. Swali ni je? anajua jinsi ya kututoa?

Anajua anakotupeleka? Nimejitahidi kuangalia bunge ili nione labda mawaziri wake wanaweza kuonyesha mwelekeo, huko nikachanganyikiwa zaidi.

Mwanamtandao mmoja alisema unaweza kuwa na dereva mzuri anayefuata sheria zote za barabarani lakini hajui anaenda wapi!

Kuna bango kwenye pikipiki(bajaji) niliona limeandikwa "Msinifuate mwenzenu nimepotea"
 
Raisi mtukufu Magufuli nimekaa nikatafakari nguvu kubwa inayotumika kupambana na wapinzani hapa Tanzania, pia nguvu kubwa inayotumika kupambana na mitandao ya kijamii kama vile jamiiforums, nimeshindwa kuelewa, ushauri wangu mimi ni kuwaongezea watumishi mishahara kama alivyofanya mwenzako wa Zanzibar, haiwezekani mtumishi aliyepo Zanzibar alipwe mshahara tofauti na mtumishi wa bara, hii ikitokea dunia itashangaa sana Zanzibar ni Tanzania na Tanganyika ni Tanzania haki sawa kwa wote otherwise utakuwa umewavunja moyo sana watumishi waliopo bara katika utendaji wao wa kila siku. Nakuhakikishia mheshimiwa ukiwaongeza mshahara watumishi utakua shujaa mithili ya Mao tsetung yule baba wa taifa la China. Kila mfanyakazi atafanya kazi kwa moyo na kwa ufanisi, kila mfanyakazi atahubiri falsafa zako yeye pamoja na familia yake, hakuna tena atakayesikiliza porojo za wapinzani hata ukiachia mikutano ya hadhara. Najua raisi wangu unapita huku naomba uchukue mawazo ya raia zako na kuyafanyia kazi kwa mstakabali wa taifa letu pamoja na chama na watumishi watakukumbuka na hawataisha kukutaja midomoni mwao kwa kile ulichowafanyia. MUNGU IBARIKI TANZANIA, MUNGU IBARIKI AFRIKA!!
 
Huyo ukitaka kumfurahisha mwambie hongera sana kwa kuwabana wapinzani na kutokuongeza mishahara ya watumishi wa umma, sasa umekomesha rushwa ndiyo maana Mahakama ya mafisadi imekosa watuhumiwa
 
Rais Magufuli kuna mambo unayo wafanyia Watanzania ni sahihi kabisa ila unapwaya sana kwenye diplomasia ya mahusiano na jamii ya Watz na Kimataifa na kila siku iendayo kwa Mungu unazidi kuchemsha!!!!
Haiwezekani uwafanye watu waishi kama enzi za utawala wa Makaburu wa Afrika Kusini!
Makaburu walikuwa hawataki Waafrika wajitawale kwa hofu ya kunyang'anywa madaraka!
Sasa na wewe inaonekana una hofu kubwa sana ya kupoteza Urais kwa Wapinzani! Kwa namna unavyowashughulikia na kuwatesa Wapinzani haijawahi kutokea hapa Tanzania!!!
Kama umeweza kuwaruhusu Polisi Geita kumkamata,kumpiga na kumweka ndani Waziri Mkuu mstahafu, Mhe. Lowassa kosa tu eti kasimama kuwasalimia wananchi na wafuasi wa Chama chake CHADEMA, you're going a bit too far Mr. President!!!
Baba wa Taifa Mwl.Nyerere(RIP) aliwahi kusema CCM haikuwa mama yake na alikuwa tayari kuhamia UPINZANI.Je, kama angelikuwa hai na yuko CHADEMA ,CUF,UDP,NCCR-Mageuzi n.k. ungelimkata, kumhoji na kumweka ndani kisa yuko upinzani???Try to think big Mr. Presida, we do respect you!
Kumbuka haya hayakujengi wewe wala CCM yako baali yana kubomoa kwa 100%! Hebu jaribu kubadilika. Huu ni ushauri nasaha usio na gharama yoyote!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom