Anayejua Rais Magufuli anatupeleka wapi atuambie, naona kama tumepotea

Status
Not open for further replies.
Mwl Nyerere aliwahi kusema "hatuwezi kuwa na rais ambaye hatujui kesho ataamka amefikiria nini au ameshauriwa nini na mke wake". Kwa wakati ule kilionekana ni kijembe kwa mzee Mwinyi lakini leo kauli yake inaonyesha maana.

Hatujui mwelekeo wa nchi kiukweli hatujui kesho atafukuzwa na nani au ziara ya rais au waziri mkuu itakuwa wapi. Hatujui kama tutaamka tunafagia barabara au tutaingia ofisini kwetu kama kawaida.

Hatujui tunaanza na nini, kujenga viwanda au kuboresha miundombinu na kuimarisha kilimo ili tupate malighafi.

Hatujui tatizo la sukari kwa mfano linaondoka kwa kurekebisha viwanda vyetu na kuongeza uzalishaji wa miwa au kuruhusu sukari ya nje au tuvamie magodauni ya watu

Ukimuangalia usoni na ukasikia anachotamka unakiri ana nia kabisa ya kututoa hapa. Swali ni je? anajua jinsi ya kututoa?

Anajua anakotupeleka? Nimejitahidi kuangalia bunge ili nione labda mawaziri wake wanaweza kuonyesha mwelekeo, huko nikachanganyikiwa zaidi.

Mwanamtandao mmoja alisema unaweza kuwa na dereva mzuri anayefuata sheria zote za barabarani lakini hajui anaenda wapi!
Umepata like zakutosha ila nizakinafiki. Umepotea mwenyewe.
 
RAIS WETU NI CHAGUO LA MWENYE ENZI MUNGU. ....WAFALME WA PILI SURA YA SABA. ....
 
Sasa ni wakati wa kuchagua vipaumbele.Sio rahisi kuendeleza kila kitu kwa pamoja.Resources hazitatosha na juhudi itatapanywa.
 
[HASHTAG]#Invisible[/HASHTAG] naomba hii iwe special thread mpaka hapo tutapopata jibu
 
imi ni kama mleta na mwasilishaji TU wa hii maada ambayo inaonesha kuna upendeleo Fulani kutoka kwa raisi wetu.
Tangu aingie madalakani ziara zake ameelekeza kaskani na hata moja hakuna ambayo ameifanya kusini mwa Tanzania. Hilo limepelekea watu wa kusini na kuconclude kwani JPM NI RAISI wa kaskazini. Tumekuwa tukisubiri kwa hamu RAISI afanye ziala hata moja kwa sababu kuna mambo mengi tunahitaji msaada wake
By mkeleketwa south highland
 
Fasihi tamu sana.
Hata mimi nimeshuhudia Raisi anafanya ziara kaskazini tu.
Kila akifika kaskazini lzm afanye mkutani na kuongea lugha ya huko kaskazini.

Kajenga kiwanja kaskazini kisichokuwa na tija huko kaskazini.

Kwanini nyie watu wa kaskazini mnapendelewa hivi?
 
Hii ni stress lazima serikali iwasikilize na kuwajali raia wake...ubabe hadi msibani?
Rambirambi za wanakagera lazima zimuumbue mtu mzima
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom