Anayejua Rais Magufuli anatupeleka wapi atuambie, naona kama tumepotea

Status
Not open for further replies.
Kuna thread humu inaelezea ahadi za Magufuli nenda kaisome....

Halafu kuna Ilani ya CCM nenda kaisome pia.

Halafu rudi hapa uje kutuuliza ambacho hujakielewa....

HAYA ZUNGUSHAA ZUNGUSHAAA TENAA ZUNGUSHA MIKONOOO....MABADILIKOOOO!!!
Mpaka unaona aibu kueleza kuwa tumepotea.
 
Akupeleke kwani wewe umekuwa zombie? Raisi Magufuli hayuko hapa kukupeleka wewe popote pale, bali wewe ndiyo unatakiwa ujipeleke mahali kwingine, wewe ndiyo unatakiwa ujitoe hapo ulipo na kwenda sehemu nyingine, wewe ndiyo unatakiwa ujifungue minyonyoro uliyofungwa na fisadi Lowasa, Mbowe & Co. na kuwa mtu huru Raisi Magufuli hawezi kulifanya hilo na wala siyo kazi yake!
Kushuka makusanyo ya kodi ndio minyororo. Kukosekana sukari,....
 
Nashauri moderators kama wapo na wanahitaji mijadala makini kwa maendeleo ya jukwaa wafanye kazi yao kwa kuondoa hizo hoja za nje ya mada na kebehi ili watu makini tujadiliane uelekeo wa nchi yetu.

Wengi tumeanza kuona nyota kwa vile serikali haijishugulishi na vitu vya kukuza uchumi, imetunga sheria ya kufanya usafi kila mwezi na faini zake, lakini imeshindwa kuifanyia marekebisho sheria ya kazi inayowapa wageni fursa za kupora ajira. Haijafanya chochote kuboresha mazingira ya kufanya biashara so far not so good
Bila ufumbuzi wa taka zinaendaje dampo.
 
Huu utawala hautapga hatua katika maendeleo maana JPM ana dhamira nzuri ila watendaji wake hawatak kubadilika.... ataishia panga pangua na siku znaenda.... hakuna priorities, kipi kianze kipi kimalizwe... bajeti za wizara hazi reflect hali halisi.... uhaba wa maisha utazid
ndo kauli zenu za miaka yote!!! Inamaana maprofesa wote hawafai?
 
Muda mwingine unaweza kuonyesha uwerevu lakini kupitia uwerevu wako ujinga wako pia ukaonekana, hivi Dkt Magufuli tangu aingie madarakani alikua anaenda na bajeti aliyoiandaa au aloandaa Kikwete? Tabia za namna hii haitusaidii sisi kama watanzania, hata kama aumpendi jitahidi kupima kwa haki, nafikiri unafuatilia bunge la bajeti na kilichomo unakiona hapo ndo tuanzie, nchi haiendeshwi wewe unavyotaka bali Rais anavyoona inafaa muda wa kupima anafanikiwa au la bado aujafika kupitia bajeti hii tutaweza kupima ni kwa kiasi gani Rais anafanikiwa lakini hii tabia ya kumkatisha tamaa Rais haifai ni tabia za watu wenye husuda na zaidi wamejaliwa wanawake kuwa nazo nchi ikiyumba sio yeye Rais atakayeteseka bali ni sisi wananchi, ni jukumu letu kukosoa pale palikosewa na kuonyesha njia sahihi ya kupita lakini kukosoa tu bila kuonyesha nini kilitakiwa kifanyike hiyo ni tabia ya kike
Wasiwasi wake ni mwenendo wa makusanyo ya mapato na mwelekeo wa bajeti.
 
Utajuaje umepotea wakati hujui unakwenda wapi!


Utapoteaje wakati hujui unapokwenda? JPM anayo ilani wewe ulikuwa unazungusha mikono sasa umedandia safari ya watu tuliza kipago uone driver anavyolenga madaraja
Sio jibu na hujui jibu nilipi.
 
KUNJAA NGUMI, zungurusha, zungurusha, mabadikooo-lowasaaaaaa, LOWASAAAA-Mabadilikoooo! twende kaziii, tumewashika pabaya, niliwaambia niachienii mimi nawajua CCM! Kama nawaona wazungurushaa mikonoooo vileee!
Hilo ndio jibu?
 
Unaposema "anatupeleka wapi" ili kukujibu lazima ueleze kuwa ana/metutoa wapi. Wapi tulikuwa ndo tujue wapi tunaenda badala ya kuzungusha mikono.
Ni swali gumu kwenu ndio maana mnaangaika. Majibu hamna.
 
Hivi mkuu makusanyo ya mwezi April yalikuwa trilioni ngapi? Na za mwezi May je?

Zamani tulikuwa tunatangaziwa mapato na matumizi ya serikali lakini kwa sasa ni kimya kabisa. Pia ukiongea na watumishi serikalini watakwambia hakuna hela ya DEVELOPMENT imetumwa mwezi wa nne na wa tano, pia hata hela ya kuendesha ofisi maarufu kama OC haijatumwa kwa miezi miwili. Hii ni dalili kuwa nchi haina muelekeo mzuri kiuchumi ingawa sisi wengine tunampa muda huyu nahodha wetu hadi atakapoanza kutekeleza bajeti yake mwezi July
Kumbe unaelewa ee!!!bac kuwa mpole kuanzia Jully makamuz yanaanza.Saiv bado bajeti inayotumika ni ya mjomba
 
Nchi haiendeshwi kwa matakea ya rais ndiyo maana kuna miongozo kama ilani, mipango ya muda mrefu na mfupi, katiba, sheria, miongozo na nyaraka mbali mbali. Wananchi ni haki yetu kuhoji, kukosoa, kushauri na kulalamika kama mambo hayaendi vizuri. Tatizo linakuja pale anayehoji au kukosoa anapoonekana adui. Tabia hii siyo nzuri na haiwezi kutupeleka popote kama taifa
Check unavyodhihirisha upumbavu wako,nyaraka na mwelekeo wa nchi wap na wapi?Lala ukue unaleta tu michosho humu ndani
 
Kama hujui unakoelekea ni wewe sisi tunajua magufuri anatupeleka kwenye raha sasa wewe tunaomba ukae pemben usubiri 2020 uzungushe kiuno maana haitakuwa mikono tena.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom