We jamaa nakuona sana humu ndani JF masaa yote 24, wewe nawe ni Jobless tu kama vijana wanaosubiri nafasi za JKT humu ndani.
Wengine tunaenda huko kwa mapenzi yetu kabisa na tunaipenda hiyo kazi. J3 njoo TPB tawi la Metropolitan (Ukifika pale Posta kwenye yule Askari kwa pembeni utaona hiyo TPB) Ingia ndani, kisha kunja kushoto, tembea kidogo utatazamana na Credit Department, achana na ya kwanza njoo ya pili yake. Utamkuta kijana wa kiume na binti mwingine wa kike mweupe, huyo wa kiume ndo mimi.
Usifikiri kila anayekwenda JKT hana cha kufanya, wengine wana mipango wa kutimiza ndoto zao, kuna watu wana ndoto za Usalama wa Taifa, Polisi, JWTZ n.k hawezi kusitisha kupigania ndoto yake eti kisa waombaji ni wengi.
Nimekujibu hivi maana naona unawakomalia sana watu wanaotaka kuingia JKT 2016, ni vema ukakaa kimya na ukawaacha kama walivyo maana hatuwezi kukata tamaa kwa maneno yako.