Asante Mkuu, namaanisha hapohapo Tanzania Postal Bank. Kama anayekata viuno ili kunufaisha familia yake na watoto sio vibaya sana.
Nipo hapa TPB kama Channel ya kuniweka vizuri ili niende sehemu nyingine, mshahara wa hapa ni tegemezi kwangu na kwa wengine. Ninachokipata nitawaachia wanaonitegema kwa kiasi flani ili kiwasaidie punde nikienda JKT.
Naenda JKT kutazamia kutimiza ndoto zangu, katika maisha yangu nafanya kile ambacho moyo wangu unatamani, napenda sana kuwa na amani. Nikishindwa JKT na seheme zingine zote ambazo zinaweza kutimiza ndoto zangu basi nitatafuta kazi nyingine ya kufanya, ila kwa sasa bado sijakata tamaa kwamba siwezi timiza ndoto yangu. Na sijaona cha kunizuia ili nisitimize ndoto yangu.
Sijui kwanini umesema mimi ni muanzilishi wa Thread zinazohusu JKT, unaweza ukanionesha ni thread gani nimeanzisha? Napenda kuingia ktk Thread zinazohusu JKT ili nijue naenda wapi na inabidi nifanye nini ili kukabilia na changamoto hizo kabla ya kuanza mafunzo na baada.
Wewe ni mtu mzima, kama umetimiza malengo yako basi hongera sana, sisi bado tuna kwenye process, hata wewe ulivyokuwa kwenye process haukutamani ukatishwe tamaa, na sisi pia hatutamani kusikia mambo vitu hasi bali chanya.
Umeongea mengi na maneno ya ajabu na matusi kedekede ila naomba nikwambie kwamba mimi ndo kwanza naona umenipa hali mpya na shauku mpya ya kuingia JKT, mahali palikuwa na shida au kikwazo mbele basi kuna ushindi karibu. Wana wa Israel walikutana na ukuta wa Yeriko ila Yeriko ilidondoka, walipita jangwani ila Mungu aliwapa maji ktk mwamba, Wana wa Israel walivyoona bahari, waliingiwa na wasiwasi ila baadae mlango ukafunguka, vijana wenzangu mnaosubiri nafasi za JKT nawaambia ya kwamba mlango utafunguka. Usisikilize maneno ya watu wanakwambia nini, tazama moyo wako una shauku ya nini. Wapinzani ni wengi na vita ni nyingi ila nawasihi tupambane, Mungu atafungua mlango.
Kusudi la Mungu haliwezi kuzuiwa na chochote kile, cha msingi ni uvumilivu na kujiandaa kisaikolojia.
Nawapenda sana vijana wenzangu.