Anayejua dawa ya jino, leo sijalala

Anayejua dawa ya jino, leo sijalala

Pole sana mkuu binafsi mpaka mwaka 2005 nilikuwa tayari nishang'oa meno matano na lingine likawa lina fuata mkumbo wa kuoza. Nilipata kupitia zoezi la kuziba ambalo ni suluhisho la muda mfupi si zaidi ya wiki mbili utarudi kule kule! Hii miti shamba siyo ya kuipuuza hata kidogo! Mzee mmoja akanituma kutafuta ndulele na mzizi wa mnyonyo akazikata ndulele katikati akaosha ile mizizi akachemsha akaweka chumvi na majivu kidogo ule mchemsho ukachemka kama dak 5 akaipua ulipoa kiasi cha uvuguvugu nikasukutua mara moja tu aisee yale maumivu niliyo yapata! Baada ya dakika kama 20 hivi yakapoa na sijawahi pata tena changamoto ya meno tangu ile siku mpaka sasa na lile lilokuwa limeoza liliendea kumeguka tu lenyewe vipande vipande hadi likaisha lenyewe!
Hata mimi nilipokuwa mdogo nilipata maumivu ya meno usiku, bahati bibi alikuwepo alichemsha mizizi ya ndulele nikasukutua yale maji na maumivu yakapotea.
 
Write your reply...pole naona kama nitakuchanganya ila mimi nimepoteza jino moja na lingine limebak kipandf tangu mwaka 2015 nilivyotumia dawa hakuna jino tena lililotoboka au kuniuma na kimebaki kipande. Lakini kama upo dar es salaam nenda ubungo plaza ingia ndani kuna duka lipo karibu na ttcl wanauza madawa ya asili waambie tatizo lako watakusaidia mim kipind hiko nilinunua elfu kumi
Duh I wish ungekuwepo mapema humu kwenye ule Uzi wa shida ya meno uliwekwa humu
Mimepoteza meno ya kutosha
 
Chukua matula also known as ndulele, yale matunda yake, kamulia sehemu inayouma ila tahadhari, maji yake usimeze, dakika 3 jino linapoa na mdudu anakufa na unaweza kusahau hata issue za kungoa meno, nasisitiza, maji yake ya ndani dondoshea kwenye jino linalouma ila usimeze, baada ya hapo anza utamaduni wa kupiga mswaki kwa kutumia chumvi iliyochanganywa na limao

View attachment 3411738
Duh jino la juu SS hapa ni mitihani
 
Write your reply...pole naona kama nitakuchanganya ila mimi nimepoteza jino moja na lingine limebak kipandf tangu mwaka 2015 nilivyotumia dawa hakuna jino tena lililotoboka au kuniuma na kimebaki kipande. Lakini kama upo dar es salaam nenda ubungo plaza ingia ndani kuna duka lipo karibu na ttcl wanauza madawa ya asili waambie tatizo lako watakusaidia mim kipind hiko nilinunua elfu kumi
Hujasema umetumia dawa gani. Hilo ulilopoteza ilikuaje? Ulidondosha au ilikuaje likapotea? Meno unatakiwa uyaache kinywani ukitoa ni rahisi kupoteza. Na why utoe?
 
Mimi nilihakikisha nakuwa msafi kinywani. Hadi leo Sina kesi ya jino

Swaki kila muda haswa unapojijuua unatatizo la meno.

Mimi hata ofsn Nina mswaki. Nikicharara natumia kuswaki kwa chunvi
Yes hili watu hawalifuatilii wanatumia dawa shida inarudi hawajui hii nayo ni muhim mi piga ua siwezi lala bila kuswaki
Ni muhim snn km una shida ya meno ht km huna
 
Wapendwa sijalala naugilia maumivu jino linanitesa hua linauma linaacha nimetumia dawa dawa hapo kati lakini Leo limeniamulia.

Kuhusu kutoa nimetoa meno kama ma 5 tokea udogoni Hadi hivi ukubwani pia mwaka Jana nilitoa ma wili kwakupishana miezi nilihisi nitapumzika Sito pata tena shida mwaka huu limenianza hili la juu limetoboka linanipa shida sana

MSAADA WA DAWA yoyote nitumie kama naweza kupona haraka.
Unaishi wapi
 
Dawa iliyoniponesha mimi bila kung'oa jino.

LIMAO1
MAFUTA YA TAA MILLS 10(VIZIBO2 VYA MAJI)
MAJI KIKOMBE 1 CHA CHAI

Namna ya kuandaa.

Katakata vipande vya limao kisha weka kwenye sufuria bandika jikoni
Tia maji yako kile kikombe chote cha maji.
acha ya chemke hadi limao zibadirike rangi.Kisha weka mafuta ya taa acha kidogo kisha ipua na yaache ya poe.

Tafuta mswaki wa mti kisha uwe unachovya yale maji unasukutulia na kudondoshea matone ya maji hayo kama jino lako lina shimo.

Fanya hivyo kutwa mara3 kwa siku3-5 mfululizo.Baada ya hapo wadudu wote watakufa kifo cha mende na hutpata shida hiyo tena

Wakifa sasa wanaenda wapi, unawameza au unawaona nje? Nataka niwaone wanakuaje.
 
Wapendwa sijalala naugilia maumivu jino linanitesa hua linauma linaacha nimetumia dawa dawa hapo kati lakini Leo limeniamulia.

Kuhusu kutoa nimetoa meno kama ma 5 tokea udogoni Hadi hivi ukubwani pia mwaka Jana nilitoa ma wili kwakupishana miezi nilihisi nitapumzika Sito pata tena shida mwaka huu limenianza hili la juu limetoboka linanipa shida sana

MSAADA WA DAWA yoyote nitumie kama naweza kupona haraka.
Nenda kaling'oe
 
Kama uko Moshi, ni pm nikupatie dawa kwa 3000/- tu ni kiboko ya jino linalouma ndani ya nusu saa utapata nafuu then utasahau issues ya kung'oa kabisa. Ila kwa sasa nashauri usipige mswaki na dawa ya meno hizi za chemicals/ madukani badala yake tumia chumvi mawe, mkaa au karafu.
 
chukua kifuu cha nazi kichome kiwe majivu.Tafuta ndulele wengine wanaita ndula au kama huijui yale matunda jamii ya nyanya chungu au wengine wanaita ngogwe japo lakini hayaliwi.Pasua yale maji kamulia kwenye hayo majivu kisha weka kwenye shimo la jino.
Mdudu atakufa haraka sana
utakuja kunishukuru mimi nilifanya hivyo
 
Tafuta mzizi wa ndulele au ndula ,tia mafuta ya taa kidogo kama nucta ,brush Hilo jino ukisikia mauvimu niite kima
 
Back
Top Bottom