Anayejua dawa ya jino, leo sijalala

Anayejua dawa ya jino, leo sijalala

chukua kifuu cha nazi kichome kiwe majivu.Tafuta ndulele wengine wanaita ndula au kama huijui yale matunda jamii ya nyanya chungu au wengine wanaita ngogwe japo lakini hayaliwi.Pasua yale maji kamulia kwenye hayo majivu kisha weka kwenye shimo la jino.
Mdudu atakufa haraka sana
utakuja kunishukuru mimi nilifanya hivyo
Asante
 
Kama uko Moshi, ni pm nikupatie dawa kwa 3000/- tu ni kiboko ya jino linalouma ndani ya nusu saa utapata nafuu then utasahau issues ya kung'oa kabisa. Ila kwa sasa nashauri usipige mswaki na dawa ya meno hizi za chemicals/ madukani badala yake tumia chumvi mawe, mkaa au karafu.
Asante
 
Changamoto ya meno inatesa watu sana.
Ni kweli na sababu wengi hatuna japo elimu kidogo ya afya ya kinywa, jamii imekariri kung'oa jino tu au kutafuta dawa ya kupoza maumivu bila kutaka kujua chanzo cha tatizo ni nini.

Mate yetu yakiwa kwenye afya kwa maana hayana asidi na yana madini yenye kuhitajika basi hufanya kazi ya ku repair zile damage ila sisi damage ni kubwa kuliko kiwango cha repair.
 
Nimetafuna sana karafuu
Wanachemsha star anise pamoja na karafuu. Ikipoa unasukutua kinywani mara kadhaa kwa siku.
Zingatia, dawa ya uhakika ya jino ni kuziba, kuondoa mzizi wa jino(root canal) au kung'oa.
 
Ni kweli na sababu wengi hatuna japo elimu kidogo ya afya ya kinywa, jamii imekariri kung'oa jino tu au kutafuta dawa ya kupoza maumivu bila kutaka kujua chanzo cha tatizo ni nini.

Mate yetu yakiwa kwenye afya kwa maana hayana asidi na yana madini yenye kuhitajika basi hufanya kazi ya ku repair zile damage ila sisi damage ni kubwa kuliko kiwango cha repair.
Hakika mkuu.
 
Back
Top Bottom