Kumbukeni huyu alikuwa CCM kindakindaki akiwa na akina James ole Millya na akina Mrisho Gambo. Binafsi sina Imani kabisa wanaCCM waliohamia Chadema. Wapo Kimaslahi zaidiNimemsikia Ally Bananga kwenye mahojiano, nadhani amepanic nakuanza vita bila kujua anapambana na nani. Amepambana na Lissu, Lema, Mnyika kwa maana wamekosea sehemu fulani kutokana na tweet zao juu ya kukutana na Rais, Diamond pamoja na wabunge 19.
Anapohojiwa msimamo wake kuhusu wabunge 19 anaeleza kwamba familia Kwanza Katiba baadaye. Najiuliza anaamini hiki ndicho wananchi wanachokihitaji? Leo viongozi wote wa upinzani wakiwaza familia zao watapata muda wakuwaza Katiba mpya?
Anasema wakutane na shibuda Kwanza kabla ya kwenda kuonana na Rais Kama takwa lakukukuna linavyotaka, je leo tunaamini shibuda anakubaliana na agenda za Chadema wanazotaka kuziwasilisha kwa Rais? Je waende kukutana na Rais kama fasheni au waende kwa msingi wa mahitaji ya hoja zao.
Anadai atamuunga mkono Diamond, lakini wengine wanaopingana na Diamond anadai wamekosa agenda. Kwanini anaamini kwake kumsapoti diamond ni agenda lakini wengine mmojammoja awapaswi kumpinga diamond? Ni wapi chama kimetoa msimamo wake juu ya bet ya Diamond?
Lakini pia overconfidence inamwondoa kwenye mjadala nakufikia kuona Kama alistahili kuwa mgombea wa Chadema Arusha na si Lema. Je Kama alikuwa na kinyongo juu ya lema kwanini asimwambie?