Ally Bananga: Nina kiapo na mke wangu, nitamlinda kwa gharama ya damu yangu

Nimemsikia Ally Bananga kwenye mahojiano, nadhani amepanic nakuanza vita bila kujua anapambana na nani. Amepambana na Lissu, Lema, Mnyika kwa maana wamekosea sehemu fulani kutokana na tweet zao juu ya kukutana na Rais, Diamond pamoja na wabunge 19.

Anapohojiwa msimamo wake kuhusu wabunge 19 anaeleza kwamba familia Kwanza Katiba baadaye. Najiuliza anaamini hiki ndicho wananchi wanachokihitaji? Leo viongozi wote wa upinzani wakiwaza familia zao watapata muda wakuwaza Katiba mpya?

Anasema wakutane na shibuda Kwanza kabla ya kwenda kuonana na Rais Kama takwa lakukukuna linavyotaka, je leo tunaamini shibuda anakubaliana na agenda za Chadema wanazotaka kuziwasilisha kwa Rais? Je waende kukutana na Rais kama fasheni au waende kwa msingi wa mahitaji ya hoja zao.

Anadai atamuunga mkono Diamond, lakini wengine wanaopingana na Diamond anadai wamekosa agenda. Kwanini anaamini kwake kumsapoti diamond ni agenda lakini wengine mmojammoja awapaswi kumpinga diamond? Ni wapi chama kimetoa msimamo wake juu ya bet ya Diamond?

Lakini pia overconfidence inamwondoa kwenye mjadala nakufikia kuona Kama alistahili kuwa mgombea wa Chadema Arusha na si Lema. Je Kama alikuwa na kinyongo juu ya lema kwanini asimwambie?
Ni kweli mke kwanza Saccos baadae!
 
Tatizo Kubwa La chadema Ni Kuwakuza hawa watu baadae wanajiona Wakubwa kuliko Chama chao.Wakitemwa wanalia tena...Ushauri kwao Ni kwamba Waje CCM...sisi Wewe Bananga hutaruhusiwa kuongea au Kukiuka Miiko Ya chama chetu...Hata ANC Ukikiuka Miiko wanakula Kichwa Hata Republican ilipofika Muda wa Kusimama na Trump Ili wasiwape Ujiko Democratic walisimama na Trump...Misimamo ya Taasisi Haikiukwi hata Majeshini ukigeuka wakati wa Vita ni balaa kubwa.
 
Bananga anamawazo ya wanawake sana.. mwanaume hata siku moja huwezi anza kulia lia mbele ya mke wako
 
Nimemsikia Ally Bananga kwenye mahojiano, nadhani amepanic nakuanza vita bila kujua anapambana na nani. Amepambana na Lissu, Lema, Mnyika kwa maana wamekosea sehemu fulani kutokana na tweet zao juu ya kukutana na Rais, Diamond pamoja na wabunge 19.

Anapohojiwa msimamo wake kuhusu wabunge 19 anaeleza kwamba familia Kwanza Katiba baadaye. Najiuliza anaamini hiki ndicho wananchi wanachokihitaji? Leo viongozi wote wa upinzani wakiwaza familia zao watapata muda wakuwaza Katiba mpya?

Anasema wakutane na shibuda Kwanza kabla ya kwenda kuonana na Rais Kama takwa lakukukuna linavyotaka, je leo tunaamini shibuda anakubaliana na agenda za Chadema wanazotaka kuziwasilisha kwa Rais? Je waende kukutana na Rais kama fasheni au waende kwa msingi wa mahitaji ya hoja zao.

Anadai atamuunga mkono Diamond, lakini wengine wanaopingana na Diamond anadai wamekosa agenda. Kwanini anaamini kwake kumsapoti diamond ni agenda lakini wengine mmojammoja awapaswi kumpinga diamond? Ni wapi chama kimetoa msimamo wake juu ya bet ya Diamond?

Lakini pia overconfidence inamwondoa kwenye mjadala nakufikia kuona Kama alistahili kuwa mgombea wa Chadema Arusha na si Lema. Je Kama alikuwa na kinyongo juu ya lema kwanini asimwambie?
Hakuna anaemkataza kua na kiapo na familia yake , ubavu wake but ajue tu Kama mke wake ni Kati ya wale wasaliti wa chama 19 atatimuliwa tu no way na ndo ukweli..hakuna Katiba au kifungu ndani ya Katiba inasema utapewa favour KWA kuvunja Katiba ili Hali hu kiongozi ,na chama hakiongozwi kifamilia, hivi ni vitu tofauti ,unaona shida chapa mwendo
 
Na ndio maana wanapohamasisha maandamano huwa wanawahamasisha wengine tu kamwe hawabebi familia zao.
 
"Mimi ni mwanachama wa CHADEMA, Suala la wabunge 19 wa viti maalumu ambao Chama chetu kinasema hakiwatambui, mke wangu (Hawa Bananga) pia ni miongoni mwao na katika vitu ambavyo nimekuwa nikijiepusha kuvizungumza ni suala hili kwasababu bado maamuzi yako ndani ya chama,

Kuliweka hili kwa ufupi mimi nitasimama aliposimama mke wangu kwasababu sikufunga naye ndoa CHADEMA, sikufunga naye ndoa mitandaoni nilifunga naye ndoa msikitini, kiapo changu kwake ni kumlinda kwa gharama ya damu yangu....

Lolote lenye udhaifu kwake ni wajibu wangu kulipa uimara, ndio kitu cha thamani ninachomiliki, nitamlinda mama wa watoto wangu

"-Mwanasiasa Ally Bananga kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

Chanzo: Star TV
Hapo kwenye red, kwamba ameapa atamlinda kwa gharama ya damu yake.
Moja ya kauli za kijinga toka kwa Wanaume!
 
Iwe mkewe ndio analeta msosi mezani au haleti, kwa maamuzi ya kifamilia NAOMBA TUWE WAKWERI, jamaa ametoa jibu sahihi kwa swali.

Kwa ufupi, ni heri kusimama na mkeo katika upuuzi wake mbele za watu, na kumkanya mkiwa faragha.

Ni heri kuficha migogoro ya kifamilia mbele za macho ya walimwengu, kuliko kujifanya unawaridhisha walimwengu..maana huwa hawaridhiki, rejea kisa cha PUNDA na yule Bwana na MKEWE.

Wanaume tujifunze KUSIMAMA NA KUTETEA WAKE ZETU MBELE ZA WATU NA KUWAKANYA FARAGHA.

UNAMUANIKA MKEO MBELE ZA WATU ili UWARIDHISHE WALIMWENGU....WANAKUPA NINI?
Maza anapesa yeye hana
 
Maza anapesa yeye hana
Ni sawa na mkeo kwenda kutibua ugomvi huko, alafu akimbilie home wewe Mume wake upo na umkatae...

Pigana na maadui wa nje kwanza, ndipo upambane kumrekebisha mkeo...

Muulize Kim na Kanye, japo ni mfano wa nje, ila jua hata hapa Bongo wapo ...

NAKUBALIANA NA WEWE, MAZA ANA PESA YEYE HANA..

LAKINI TUJIFUNZE KUSIMAMA NA WAKE ZETU MBELE YA JAMII..TUWALINDE.

TUKIWA FARAGHA NDIO TUADHIBIANE
 
Akishalipwa mke wake zinasaidia familia. Mnataka asimame nanyi mnaitunza familia?

Kwa mwanaume makini hakustahili ajibie hoja zakikatiba kupitia mke wake.

Ameuza utu wake kwa maslahi ya wawili na si taifa.

SIKU NYINGINE ANYAMAZE TU.
Sasa analishwa afanyaje? Angejua huyo anayemsifia angekaa kimya tu. Anyway he is jobless kwa hiyo wacha ajitoe akili maana hana nafasi kwenye chama na udiwani hana sababu alitaka ubunge kwa tamaa zake.
 
Back
Top Bottom