Kuhusu Wabunge 19 waliofukuzwa CHADEMA; ninachokiona mimi ni Uhalifu na Ugaidi wa Kiserikali dhidi ya Katiba na Sheria

Tulimumu

JF-Expert Member
Mar 11, 2013
14,305
12,969
Katika hali ya kawaida ungetegemea serikali iwe mfano wa kuigwa kwa kufuata na kutekeleza katiba na sheria. Lakini toka awamu ya tano imeingia na hii iliyopo ya kurithi tunashuhudia uvunjaji na usiginaji mkubwa wa katiba na sheria unaofanywa na watu walioapa kuilinda katiba na kufuata sheria huku wakiwa wameshika vitabu vitakatifu.

Kuzuiwa kwa mikutano, maandamano na shughuli huru za kisiasa ni mfano wa kwanza kabisa alioanza nao wendazake na sasa kurithiwa na mwenza wake.

Suala lawabunge 19 waliofukuzwa uanachama na chama chao lakini wakiwa wanakingiwa kifua na serikali ni mfano wa dhahiri wa uvunjwaji na usiginaji wa katiba na sheria.

Tumeshuhudia huko nyuma vyama ikiwemo CCM na CUF vikifukuza wanachama wao ambao ni wabunge na kwa mujibu wa sheria watu hao walitolewa bungeni wakiwa wamefungua kesi mahakamani au hawajafungua kesi kwakuwa kufungua kesi au kukata rufaa hakubatilishi uamuzi uliotolewa na chama mpaka hapo mahakama itakapoamua vinginevyo.

Kama ingekuwa kukata rufaa kunamuweka aliyehukumiwa huru ilipaswa Sabaya naye aachiwe maratu alipokata rufaa lakini aliendelea kubaki ndani hadi uamuzi ulipopitishwa. Hata CUF ilipowavua uanachama wabunge wake wa viti maalumu waliondokewa bungeni licha yakuwa walifungua kesi mamahakamani. Lakini leo tunashuhudia jinsi spika mwanasheria anavyoshiriki uhalifu dhidi ya katiba na sheria za nchi.
 
Mliambiwa katiba ililindwa baada ya kifo cha Legendary John now mbona hamtoki kuilinda au kuna sehemu na sehemu za kuilinda katiba?
 
Nyie hamuelewi, kwa ufupi akina Halima.

They are there to stay mpaka 2025! Sababu kuu ni undumila kuwili wa Mbowe, serikali inajua kabia Mbowe hatoteua wabunge hivyo kulifanya bunge kukosa uhalali kwa sababu halitakuwa na upinzani. Kwa hiyo hiyo ya mahalama ni dana dana tu.
 
Back
Top Bottom