Ally Bananga: Nina kiapo na mke wangu, nitamlinda kwa gharama ya damu yangu

Nimemsikia Ally Bananga kwenye mahojiano, nadhani amepanic nakuanza vita bila kujua anapambana na nani. Amepambana na Lissu, Lema, Mnyika kwa maana wamekosea sehemu fulani kutokana na tweet zao juu ya kukutana na Rais, Diamond pamoja na wabunge 19.

Anapohojiwa msimamo wake kuhusu wabunge 19 anaeleza kwamba familia Kwanza Katiba baadaye. Najiuliza anaamini hiki ndicho wananchi wanachokihitaji? Leo viongozi wote wa upinzani wakiwaza familia zao watapata muda wakuwaza Katiba mpya?

Anasema wakutane na shibuda Kwanza kabla ya kwenda kuonana na Rais Kama takwa lakukukuna linavyotaka, je leo tunaamini shibuda anakubaliana na agenda za Chadema wanazotaka kuziwasilisha kwa Rais? Je waende kukutana na Rais kama fasheni au waende kwa msingi wa mahitaji ya hoja zao.

Anadai atamuunga mkono Diamond, lakini wengine wanaopingana na Diamond anadai wamekosa agenda. Kwanini anaamini kwake kumsapoti diamond ni agenda lakini wengine mmojammoja awapaswi kumpinga diamond? Ni wapi chama kimetoa msimamo wake juu ya bet ya Diamond?

Lakini pia overconfidence inamwondoa kwenye mjadala nakufikia kuona Kama alistahili kuwa mgombea wa Chadema Arusha na si Lema. Je Kama alikuwa na kinyongo juu ya lema kwanini asimwambie?
Kumbukeni huyu alikuwa CCM kindakindaki akiwa na akina James ole Millya na akina Mrisho Gambo. Binafsi sina Imani kabisa wanaCCM waliohamia Chadema. Wapo Kimaslahi zaidi
 
Akishalipwa mke wake zinasaidia familia.Mnataka asimame nanyi mnaitunza familia?

Kwa mwanaume makini hakustahili ajibie hoja zakikatiba kupitia mke wake.

Ameuza utu wake kwa maslahi ya wawili na si taifa.

SIKU NYINGINE ANYAMAZE TU.
MwanaCCM ni mwana CCM tu. Huyu Bananga alikuwa CCM na bado ana vimelea vyote vya uchafu huo.
 
sawa, kumfuata mkeo ama kubakia CDM huo ni uamuzi wako ndugu - CDM haiwezi kukuingilia mambo yako ya ndani... - after-all uanachama wako ni kwa hiari yako na maisha ya kisiasa ni ya kwako - uamuzi wowote utakaouchukua hilo ni la kwako na mkeo (familia), sisi hayatuhusu - chama kinasonga mbele.
Hili jamaa jinga sana! Sasa linamtisha nani? Hata kabla yake Chadema ilikuwepo. Anasubiri nini kuondoka amfuate mkewe huko kwa Ndugai? Janaume zima linategemea kuishi kwa posho ya mkewe aliyeingilia mlango wa nyuma bungeni!
 
Good, good! Mwisho wa siku lazima mtu asimame kwenye ukweli. Familia kwanza kabla ya kitu chochote. Huwezi kutelekeza famila halafu eti ukawa mtiifu wa chama. Hata Lissu na Lema walikimbilia nje ya nchi na familia zao! Hawakukimbia na Chadema wala wana Chadema!
Kwa hiyo? Uibe kwa kuwa nyumbani hakuna chakula na familia inakufa njaa? Uinde kinyume na utaratibu ili tu familia ipone? Kwanini usihangaikie kipato halali kwa familia yako?
 
Yupo kwenye list wateuliwa watarajiwa..DCs,DEDs... Mama ameona uvccm hamna kitu..rejea ya Sabaya,Makonda...linganisha na Gekul,Waitara,Silinde
CCM hakuna Kijana wa maana wakumlinganisha na akina Mnyika, Pambalu, Heche, Kiwanga, Sugu, Prof. Jay, n.k. CCM kuna akina Polepole, Makonda, Sabaya. Shida tupu! Acha tu mama achukue wa upande wa pili nchi iendelee
 
Ukijua ma boss wako wanaimba usafi huku wanaogelea kwenye uchafu unakua smart sana

Ally Bananga ni mwanachadema mwenye akili kubwa sana zaidi ya watu wanavyomwangalia

Kwangu alikua diwani bora kwa kipindi chote cha uwakilishi wake
Nini kilimnyima udiwani? Kama siyo uhuni wa CCM aipendayo
 
Je, kama jina lilienda kwa rushwa ya ngono kwake sawa tu.Hasimamii utu Bali mali
Ndio maana yake. Wewe unafikiri Ndugai alimpa mkewe ubunge wa dezo bure tu? Janaume zima eti mradi familia inapata chochote yeye atamuunga tu mkono mkewe aendelee na anachofanya. Dume bahati mbaya hili
 
Ally Bananga anababanganya huku "anabananga"!What a name!Anamtetea mkewe ili asipewe chai na matembele!🤣🤣🤣
 
Nimemsikia Ally Bananga kwenye mahojiano, nadhani amepanic nakuanza vita bila kujua anapambana na nani. Amepambana na Lissu, Lema, Mnyika kwa maana wamekosea sehemu fulani kutokana na tweet zao juu ya kukutana na Rais, Diamond pamoja na wabunge 19.

Anapohojiwa msimamo wake kuhusu wabunge 19 anaeleza kwamba familia Kwanza Katiba baadaye. Najiuliza anaamini hiki ndicho wananchi wanachokihitaji? Leo viongozi wote wa upinzani wakiwaza familia zao watapata muda wakuwaza Katiba mpya?

Anasema wakutane na shibuda Kwanza kabla ya kwenda kuonana na Rais Kama takwa lakukukuna linavyotaka, je leo tunaamini shibuda anakubaliana na agenda za Chadema wanazotaka kuziwasilisha kwa Rais? Je waende kukutana na Rais kama fasheni au waende kwa msingi wa mahitaji ya hoja zao.

Anadai atamuunga mkono Diamond, lakini wengine wanaopingana na Diamond anadai wamekosa agenda. Kwanini anaamini kwake kumsapoti diamond ni agenda lakini wengine mmojammoja awapaswi kumpinga diamond? Ni wapi chama kimetoa msimamo wake juu ya bet ya Diamond?

Lakini pia overconfidence inamwondoa kwenye mjadala nakufikia kuona Kama alistahili kuwa mgombea wa Chadema Arusha na si Lema. Je Kama alikuwa na kinyongo juu ya lema kwanini asimwambie?
Ameamka na hangover mlevi was the.don huyo
 
Sio sababu ya mkewe kuwa mbunge, Bananga ni akili kubwa.... anajua kuishi ndani ya itikadi bila kuathiri jamii
Bananga hanaga akili za kushikiliwa
Ni kweli kabisa, maana kipindi cha dhalimu aliwashikia ccm wote akili zao.

Nenda kwenye ule uzi wa Mbatia ukatoe maelezo ni kwa nini dhalimu alipandishwa deni la taifa na kuwa 71t+, toka 39t+ aliyokuta kwa JK. Ukifanikiwa kutoa maelezo nitajua hushikiwi akili.
 
Back
Top Bottom