Aliyekuwa Rais wa Tanzania, Hayati Dkt. John Magufuli azikwa Chato mkoani Geita

IMG-20210326-WA0048.jpg
 
Kuongoza nchi sio jambo rahisi sana.

nawaza mtu ana mke na watoto wawili ila hawezi kuongoza familiya migogoro kibao,sembuse magufuli kuongoza hili linchi looote? Lawama zote kwake?...
Kabisa ni kazi kubwa,kuongoza watu zaidi ya mln 50 si mchezo

Ova
 
To be honest, sijasikitishwa na kifo chake. Kama ambavyo sikufurahishwa na utawala wake.

Namshukuru Mungu kwa yote na namuomba ampokee kiumbe wake.

Sote njia ni moja, ila yeye katangulia tu.
Hivi ni utawala up ushawahi kupendwa??

Ova
 
" Bungeni ni mahali patakatifu siyo sehemu ya kujadili mambo ya kipuuzi puuzi" asema baba askofu.

Alichosahau baba askofu nadhani ni namna wabunge hao walivyofika hapo bungeni.
 
" Bungeni ni mahali patakatifu siyo sehemu ya kujadili mambo ya kipuuzi puuzi" asema baba askofu.

Alichosahau baba askofu nadhani ni namna wabunge hao walivyofika hapo bungeni.
Atakua Askofu Gwajima tu huyo.

Nadhani atakua chato anasubiri Magufuli azikwe halafu arudi Ubungo kudanganya kondoo wake kua anafufua wafu.
 
Kabisa ni kazi kubwa,kuongoza watu zaidi ya mln 50 si mchezo

Ova
Haiwezi kuwa kazi kubwa kamwe.

Kutoa uongozi sehemu ambayo una taasis kibao zinakusaidia.

Unasheria na taratibu za kufanya mambo ambazo zinakuwa enforced.

Tenda haki,fuata sheria,kanuni na taratibu. Heshimu mamlaka nyingine kwenye utendaji wao. Ingilia pale tu inabidi na kufuata utaratibu.

Epuka kujiona wewe ndiyo wewe,bila wewe mambo hayaendi.

Wote wanaolalamika uongozi mgumu ama shida wao ndiyo tatizo.
 
Habari za muda huu.Kwanza nitoe pole kwa msiba huu mzito uliotukumba taifa letu na mpaka sasa tupo katika hatua za mwisho za kumpumzisha mpendwa wetu JPM katika makazi yake ya milele.

Lakini pia katika hali isiyo ya kawaida siku ya kuamkia tarehe ya kutangazwa kifo cha JPM yaani tarehe 18/03/2021 hali ya hewa haikuwa ya kawaida.Kwani kulikuwa na wingu zito juu ya Dar yote na mvua ilinyesha hali ya kuwa ni muda mrefu ulipita bila mvua kunyesha.Hata Leo tar 26/03/2021 Siku ambayo mpendwa wetu JPM anapumzishwa katika makazi yake ya milele hali kama hii imejirudia tena.Natambua kuwa ni msimu wa mvua lakini kwanini haikunyesha juzi au jana au siku zingine za nyuma? Je hii huashiria nini?

Mwisho natoa pole kwa watanzania wenzangu na itoshe tu kusema Mh wetu JPM vita vizuri amevipiga imani ameilinda mwendo ameumaliza.Bwana ametoa Bwana ametwa Jina lake lihimidiwe.Apumzike kwa amani.Amina

Sent from my SM-A305F using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom