Aliyekuwa Rais wa Tanzania, Hayati Dkt. John Magufuli azikwa Chato mkoani Geita

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,536
9,346
Fuatilia mbashara hapaRAIS Samia Suluhu Hassan leo ataongoza waombolezaji kumzika Rais wa Serikali ya Awamu ya Tano, John Magufuli.

3.jpg

Jeneza lililobeba mwili wa Hayati Dkt. Magufuli likiwa Kanisani kwa ajili ya Misa ya Mazishi

1.jpg

Kaburi la Hayati Rais Dkt. John Pombe Magufuli


2.jpg

Mama Janeth Magufuli Mjane wa Hayati Magufuli akiweka mchanga kwenye kaburi

4.jpg

Rais wa JMT, Mama Samia Suluhu Hassan akiweka mchanga kwenye kaburi la Hayati Dkt. Magufuli

Mama.jpg

Mama Janeth Magufuli akiweka shada la maua kwenye kaburi

Watoto.jpg

Watoto 7 wa Hayati Magufuli wakiweka shada la maua kwenye kaburi

Rais.jpg

Rais Samia Suluhu akiweka shada la maua kwenye kaburi


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Uratibu, Bunge, Vijana na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama atamkaribisha Mwenyekiti wa Kamati ya Mazishi ya Kitaifa, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa atoe neno la utangulizi likifuatiwa na salamu.

Salamu hizo zitatolewa wawakilishi wa makundi wakiwemo wazee wa Chato, vyama vya siasa, na viongozi wa nchi za nje. Salamu nyingine ni kutoka kwa vyombo vya ulinzi na usalama, Mahakama ya Tanzania, Bunge la Jamhuri ya Muungano, Rais mstaafu Jakaya Kikwete, Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi, na Rais wa Zanzibar, Dk Hussein Mwinyi.

Baada ya salamu, Rais Samia atahutubia waombolezaji na kisha ataongoza wananchi na wageni kutoka nje ya nchi kutoa heshima za mwisho kumuaga Rais Magufuli.

Baada ya tukio hilo, familia ya Magufuli ikiongozwa na mkewe Janet Magufuli, Rais Samia na viongozi watakwenda eneo la maziko nyumbani kwa Magufuli.

Saa 8:00 mchana mwili wa Rais Magufuli utaondolewa uwanjani na kupelekwa mazikoni ambako itafanyika ibada itakayoongozwa na Askofu wa Jimbo la Rulenge wilayani Ngara Mkoa wa Kagera, Severine Niwemugizi na kisha yatafanyika mazishi ya kijeshi.

Mazishi hayo ya kijeshi yatahusisha gwaride la mazishi na upigwaji wa mizinga 21 kutoa heshima kwa aliyekuwa Amiri Jeshi Mkuu wa majeshi ya ulinzi na usalama.

Tukio hilo litahitimisha safari ya mwisho ya maisha ya Rais Magufuli aliyefariki dunia Machi 17, katika Hospitali ya Mzena, Dar es Salaam alikokuwa akitibiwa ugonjwa wa umeme wa moyo uliomsumbua kwa zaidi ya miaka 10.


Samweli Bigambo, Mwakilishi wa Wazee Chato
Rais Magufuli ametutoka kimwili lakini kifikra tupo naye.

Wazee wa Chato tuna matumaini makubwa kuwa hakutuacha pekee, alikuwa na mwenzake -- Samia Suluhu Hassan. Walikuwa wanafanya kazi pamoja.

Tunaamini kwamba miradi yote iliyobaki ataitekeleza na kuongeza mingine. Tunachoamini ni kwamba kipimo cha uongozi uliopo ni uongozi uliopita.

Kwajhiyo Mama, ndiyo kazi kubwa hiyo tunayokupima kwayo. Hayati John alipanga mambo mengi kufanya...Yoote aliyotuachia na aliyotuahidi, ni wewe ndiyo ulituahidi.

Nikudokeze tu kidogo. Kuna wakati alituahidi kuwa hii Chato tunataka tuifanye kuwa mkoa. Sasa je, hiyo ahadi ife? Haiwezi kufa kwasababu wewe ulikuwepo. Tuna matumaini makubwa.

Na kwa uzoefu wangu katika maisha yangu, na mara nyingi huwa tunasema kuwa kuliko mama kufa, afadhali afe baba. Hata kama mkikataa, miji inayoachiwa wanaume huwa ianaharibika. Lakini miji inayoachiwa wanawake huwa inaendelea.

Kwahiyo, mimi ninaamini Mama yetu atatufanyia yaliyo mazuri zaidi. Wamama ni wajasiri.

Jenerali Venance Mabeyo, Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama
Kwa niaba ya wakuu wote wa vyombo vya ulinzi na usalama, naomba nieleze kuwa nasi tumepokea kwa masikitiko makubwa na mshtuko mkubwa taarifa za kifo cha aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Mh. Dkt. JohnJoseph Pombe Magufuli. Kwakweli ni simanzi na masikitiko makubwa.

Simanzi na masikitiko hayo yametokana na ukweli kwamba tangu alipoingia madarakani mwaka 2015 Hayati Dkt. Magufuli alionesha kuvipenda vyombo vya ulinzi na usalama kwa dhati kubwa. Alihakikisha kuwa anaviwezesha kwa mahitaji ya kiutendaji na mahitaji ya kiutawala ili viweze kutekeleza majukumu yake ya kiulinzi na usalama kwa ufanisi na weledi mkubwa.

...alivishirikisha katika shughuli mbalimbali za kiuchumi na maendeleo ya nchi yetu.

Alisema, "Hatuwezi kuwa na vyombo imara bila kuwa na uchumi madhubuti. Hatuwezi kutegemea misaada ya kuimarisha vyombo vyetu; lazima tuimarishe uchumi wetu ili tuimarishe vyombo vyetu vya ulinzi na usalama"

N katika hali hiyo, vyombo vyetu vimeshirikishwa katika shughuli zote za kiuchumi. Mifano michache ni ushiriki wetu kuhakikisha tunaulinda mgodi wa Tanzanite. Kabla ya kuulinda, lakini tujenge ukuta kuzunguka mgodi huo.

Mh. Rais, mimi binafsi alinidokeza lakini naomba nisilitoe dokezo hilo. Nitakuomba nikuone ofisini.

Pamoja na ujenzi huo wa shughuli za kiuchumi, alisema lazima tushirikishe kwenye miradi yetu mikubwa yote ya kitaifa. Na moja ya miradi mikubwa ni ujenzi wa Ikulu ya Chamwino unaoendelea na upo katika hatua za kumalizika.

Rais Dkt. John Magufuli alikuwa muumini wa dhati wa nadharia na falsafa mpya kwamba katika zama hizi ambapo nguvu za kiuchumi zinachukuwa nafasi ya nguvu ya kijeshi, kama kipimo sahihi cha ukuu au nguvu ya nchi -- Tanzania yenye uchumi imara ndiyo itakayoweza kuibuka kuwa taifa lenye nguvu.

Uumini wake huo, aliudhihirisha mara nyingi kupitia kauli yake kuwa: "Vita vya kiuchumi ni vita vigumu zaidi kuliko vita vya kawaida"
Katika kipindi cha uongozi aliwateua baadhi ya maofisha kwenye mfumo wa serikali. Hasa kushika nyadhifa kubwa zikiwemo Wakuu wa Mikoa na Wilaya, Makatibu wakuu wa Wizara, pamoja na idara na taasisi mbalimbali za umma. Mchango wake huo kwa vyombo vya ulinzi na usalama utakumbukwa daima na kuendelea kuwa alama isiyofutika kwa vizazi vingi vijavyo na kwa miaka mingi ijayo.

Pia katika kudhihirisha hilo, ziara ya mwisho kuifanya katika vyombo vya ulinzi na usalama, ilikuwa tarehe 26 Februari, 2021, alipotembelea Jeshi la Polisi ambapo aliweka jiwe la msingi kiwanda cha kushona nguo na kuzindua ofisi za utawala na bweni katika Chuo cha Polisi Kurasini.

Baada ya ziara hiyo, alikuwa amepanga tarehe 10 Machi, 2021 kutunuku kamisheni kwa maafisa wanafunzi wa JWTZ ambayo ingekuwa ni ya kwanza kufanyika Ikulu ya Chamwino, Dodoma.

Wanafunzi hao, walikuwa wameshahitimu mafunzo yao. Mara ya kwanza ilikuwa watunukiwe kamisheni tarehe 20 Februari, 2021 lakini kutokana na ziara alizokuwa anazifanya, akanielekeza tusogeze mbele hadi tarehe 6. Lakini alipokuwa Dar es Salaam anamaliza ziara katika Jeshi la Polisi, akaniambia: "Sijisikii vizuri. Unaonaje tusogeze hadi tarehe 10 nijitazamie hali yangu?" Bahati mbaya haikuweza kuwa hiyo tarehe 10.

Na kutokana na maradhi hayo, alishindwa kabisa kufika.

Kwakuwa wanafunzi wapo tayari, Mh. Rais na Amiri Jeshi Mkuu, tunakukaribisha kwa mara ya kwanza kuja kutoa kamisheni kwa maafisa wanafunzi wa JWTZ kwa tarehe utakayoona inafaa kulingana na ratiba yako.

Kwa heshima na taadhima naomba nitumie pia fursa hii kwa niaba ya vyombo vyote vya ulinzi na usalama, ingawa pengine isingependeza sana katika siku hii ya leo, lakini niseme tu kwamba tunakupongeza kwa dhati kabisa kwa kuapishwa kwako kuwa Rais wa Jmhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu kwa mujibu wa Katiba.

Tunashukuru Baraza la Kiswahili limerekebisha; utaendelea kuitwa Amiri Jeshi Mkuu, na si Amirati kama ilivyokuwa inapendekezwa.
Vyombo vya Ulinzi na Usalama vinapenda kukuhakikishia kuwa ulinzi wa nchi na mipaka yake ni salama. Na kwamba, vitaendelea Kumlinda, kukulinda wewe kama Rais -- kukutii, kama Amiri Jeshi Mkuu na kutekeleza majukumu yake kama ilivyoainishwa katika Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Aidha, vyombo vya ulinzi vinakuhakikishia utiifu, uadilifu na uaminifu mkubwa kwako Mh. Rais na Amiri Jeshi Mkuu, kama ilivyo mila na desturi kwa majeshi yetukatika awamu zote zilizopita za nchi yetu.

Job Ndugai, Spika wa Bunge
Kipekee, sisi Bunge tumhakikishie Mheshimiwa Rais wetu Samia Suluhu Hassan, ushirikiano wa kila aina.

Tutasimama naye. Tutasimama naye kwa kila tunaloweza kufanya kuhakikisha kwamba anafanikiwa na nchi yetu inafanikiwa zaidi, na zaidi, na zaidi.

Nitumie nafasi hii kumkaribisha Bungeni. Pale ndipo ataweza kuzungumza Watanzania wote katika hotuba ambayo tutamuomba aipange kwa siku ambayo ataona inafaa.

Kwa watanzania wote, kwakuwa leo ni ibada, na mimi niwaachie neno la Isaya 41:10.

Prof. Ibrahim Juma, Jaji Mkuu wa Tanzania
Nimepokea salamu za rambirambi kutoka kwa majaji wa nchi za bara la Afrika. Nimepokea salamu kutoka kwa
Jaji Mkuu wa Rwand, Gambia, Namibia, Na katibu Mkuu wa Chama cha Majaji wa Jumuiya ya Madola.

Pia kuna mtumishi wa Benki ya Dunia ambaye anajihusisha na maboresho ya mahakama, anaitwa Walid Malik. Yeye ni raia wa Pakistan.
Ananikumbusha kwamba mwezi Februari 2017, alikuwa Addis Ababa na wakati huohuo Mh. Rais Magufuli ilikuwa ni ziara yake ya kwanza kabisa kutembelea Umoja wa Afrika.

Kilichomshangaza Dkt. Walid Malik ni kwa namna gani viongozi wa Afrika katika mkutano huo, walikuwa wanamzunguka Dkt. John Joseph Magufuli. Kwahiyo, kwakuwa alikuwa anakuja Tanzania, aliniomba Siku ya Sheria nimtambulishe kwa Dkt. John Joseph Pombe Magufuli angalau amshike Rais Magufuli mkono aone huyu ni kiongozi wa namna gani wa Bara la Afrika ambaye anatoa msisimko kwa viongozi wengine wengi wa Afrika.

Majaji hawa wanamzungumzia kuwa Dkt Magufuli ni " Kiongozi mwenye maono ya mbali aliyetumia uwezo wake wote kustawisha na kutetea maslahi ya Tanzania na Afrika. kwa dhati"

Vilevile, alikuwa ni "Sauti mbadala. Alikuwa anaongea mambo ambayo wengine walikuwa hawataki kuyaongea"

Mohammed Shein, Rais Mstaafu wa Zanzibar
Nilipata bahati ya kuishi na kufanya kazi na Dkt. Magufuli kwa takriban miaka 19 na nusu. Miaka 9 na nusu nikiwa Makamu wa Rais wa JMT, na miaka 10 nikiwa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar. Tulikuwa karibu sana.

Katika moja ya sifa alizokuwa nazo, alikuwa ni mkweli wa dhati. Ni muungwana. Ukweli wake alimwonyesha kuwa haogopi binadamu mwenzie; anamuogopa Mwenyezi Mungu peke yake.

Ni mtu anayedhibiti siri ya anayoyasema na anayoyafanya. Hamhadithii asiyehusika.

Wengi wanamdhania ni mkali, si mkali. Ni kiongozi na lazima aongoze kwa misingi ya haki na usawa. Ameyafanya haya kwa vitendo. Wengi wetu tumeyaona. Wengi wetu tumeshuhudia katika matukio mbalimbali. Alikuwa anaweza kuona mbali zaidi.

Tukio ninalolikumbuka ni siku aliponiambia tukazindue barabra inayoanzia pale Tegeta - Bagamoyo. Na ninakumbuka nilikuwa na Rais Mstaafu Dkt. Kikwete siku hiyo, yeye alipokuwa waziri wa mambo ya nje.

Akaninong'oneza jambo, mwanzoni sikumwamini kwamba: "Unaona barabara hii; itafika mpaka Kusini, mpaka Kaskazini. Tutakwenda Kaskazini na Kusini kwa teksi."

Mimi nikashangaa. Akaniambia: "Na Mzee Mkapa nimeshamwambia"
Juzi nilikuwa Lindi katika uzinduzi wa daraja la Nangurukutu, nikamwamnia hivyohivyo, "tutakwenda kwa teksi" Nadhani hii sasa imetokea, ni kweli.

Ni jitihada zake. Na akaniambia tutafanya hizo si kwa misaada ya kimataifa. Tutajitahidi tuweke utaratibu tukusanye fedha zetu wenyewe na tunaweza na fedha nyingi zipo.

Nilikuwa namuamini sana.

Katika Muungano alinitia moyo sana, hasa baada ya matukio yanayotokea baada ya uchaguzi mkuu. Akaniambia we chapa tu kazi, watu wataona wenyewe.

Mheshimwa Rais (Samia Suluhu) wengi tunafahamu uwezo wako, uchapakazi wako, uhodari wako, imani yako kwa nchi yako na namna ulivyokuzwa katika kuwatumikia watu wako.

Juzi nimepata faraja kubwa ulipotoa kauli kwenye hotuba yako siku ya mazishi ya kiserikali pale Dar es Salaam. Uliposema " Mimi ni Rais"

Sikukuangalia usoni kwani ulikuwa umenipa kisogo. Natamani ningekuona usoni. Nikaona ile facial expression yako, hima na hidaya ya uso wako ulipotakimka lile. Mimi nilivutiwa sana.

Lakini hukusita, ukasema "Maumbile yangu mwnamke, lakini mimi Rais" Na huo ndiyo ukweli.

Sisis tunaokufahamu, hatuna shaka. Mwenyezi Mungu amesaidia kwa shani yake na uwezo wake kukupa nafasi hii kwa mujibu wa Katiba ya nchi yetu. Na mimi naamini hii kazi utaifanya bila wasiwasi wowote. Na tutafanikiwa chini ya uongozi wako.

Rais Mstaafu, Jakaya Kikwete
Sisi (Marais wastaafu) kumzika Rais Magufuli, ni jambo ambalo sikulifikiria kabisa
Nilitamani akamilishe kazi yake nzuri aliyoianza na atuzike sisi Kaka zake, ambao ni Marais tuliomtangulia

Mimi na mpendwa wetu, John Magufuli tumetoka mbali. Alikuwa Rafiki yangu kwa miaka kumi akiwa Waziri mimi nikiwa Rais
Alikuwa mtani wangu, alikuwa ni Waziri pekee aliyekuwa akinitania tulipokutana

Mheshimiwa Magufuli alinitunuku Kiwanja hapa Chato, kipindi akiwa Mbunge na Waziri. Alipokuwa Rais akaongeza eneo
Ilikuwa matarajio yangu kujenga nyumba, ili siku akistaafu tuendelee kupiga soga hapa Chato

Nilipokuwa Rais Mheshimiwa Magufuli alikuwa ni mmoja ya Mawaziri niliowaamini na kuwatumaini
Alikuwa jembe langu. Ndio maana nilimuweka kwenye Wizara tatu zilizokuwa ngumu anyooshe mambo

Alipojitokeza kuomba uteuzi wa kuwa Mgombea wa Urais wa CCM mwaka 2015, sikusita kumpendekeza katika majina matano niliyoyafikisha kwenye kikao cha juu cha chama

Sikuwa na tabu na Magufuli ndio jina la kwanza halafu yakafuata mengine
Unaposikia minong’ono kuwa JK hakumtaka Magufuli. Heee! Mie? Labda JK mwingine

Nimewasimulia leo mchakato tulivyokwenda nao. Yale majina matano nimekuja nayo mie
Tumepambana mpaka yakatoka matano na la kwanza lilikuwa la JPM nililoliweka mie

Ooh! JK anamchukia Magufuli, eehe! Labda mwingine sio mie. Unamchukiaje Mtu uliyemkabidhi ilani ya Uchaguzi na ameitekeleza kwa kiwango cha juu sana? Kwa sababu ipi?

Unajua Duniani waganga njaa wengi, wengine wanapata mradi wao kwa kuongopa
Maaskofu wanatufundisha “Hajui alitendalo, msamehe”

Nilikuwa nikutane naye(Magufuli) Machi 2 alipokuwa ziarani Dar. Alikuwa anikabidhi nyumba aliyonijengea
Haikuwezekana kutokana na majukumu, natamani ningerudisha muda nipate picha naye ya mwisho

Nchi yetu iko katika mikono salama, na hakuna litakaloharibika. Binafsi sina shaka na uongozi wa Rais Samia
Wewe ni mbobevu kabisa. Nakuhakikishia mimi na wenzangu tutakuwa pamoja nawe. Tutume tutaitika, usipotutuma tutaendelea na shughuli zetu

Tunashukuru kwa Mungu kwa kumuheshimisha na kumpa mwisho mwema. Tuendelee kumuombea kwa Mola ampe mapumziko mema na siku ya hukumu amjalie pepo

Mhe. Rais (Samia) nimesikia hotuba yako nikiri maneno yako yamenifariji sana na ilikuwa hivyo kwa wengi
Hatua zako ni nzuri sana, umetufariji Watanzania, umetufuta machozi na muhimu zaidi umetuhakikishia kuwa nchi ipo katika mikono salama na hakuna litakalo haribika

Binafsi sina shaka na uongozi wako kwani nakufahamu kwa muda mrefu.
Baada ya matatizo ya Zanzibar Rais Mkapa aliunda timu niliyoiongoza mimi, alikuwepo Dkt. Shein alikuwepo na Samia
Lakini nimekufahamu zaidi ulipokuja kuwa Waziri wangu katika Serikali, ulisaidia kuimarisha Muungano kwa kushughulikia kero za Muungano

Kama ulifanikisha vile kwa kiasi kile ulipokuwa Waziri, tunatarajia ufanye makubwa zaidi sasa wewe ndio Rais. Muungano utaimarika zaidi
Kipaji chako cha uongozi kilionekana zaidi na kujipambanua ulipokuwa Makamu wa Mwenyekiti wa Bunge la Katiba
Unayajua vema matarajio ya CCM na matarajio ya Watanzania kwako, kwa Serikali yao

Umekuwa sehemu ya mipango na uendeshaji wa Serikali ukiwa sambamba na Magufuli
Wewe si mwanagenzi wewe ni mbobevu uliyepikwa ukapikika barabara! Wewe ni mtu sahihi

Ali Hassan Mwinyi, Rais Mstaafu wa Tanzania
Miongoni mwa mamba aliyotuachia, jambo la kwanza nalo ni kubwa, ni pale alipoamua kutekeleza maagizo ya Baba yetu wa Taifa, Mwalimu Nyerere.

Kijana amewaza na kuamua tuhamie Dodoma. Na kutekeleza jambo hilo kwa miaka miwili, jambo ambalo sisi wengine tulichukuwa mika 40, bado hatukujtekeleza.

Kwa kipindi kifupi cha miaka mitano, nchi yetu imepiga hatua kubwa sana, hata kuushangaza ulimwengu kwa namna alivyoletea taifa lake la Tanzania maendeleo ya haraka sana.

Mh. Mama Samia, Dkt Magufuli ameondoka ametuachi wewe. Ametuachia wewe ambaye ulikuwa msaidizi wake wa karibu sana.
Kwahiyo alichokikusudia Hayati Mgufuli, ndicho ulichokusudia wewe. Nilifurahi sana uliposema siku ile kwenye hotuba yako kuwa " Huyu aliyesimama hapa ndiye Rais mwenyewe huyo"

Rais Samia Suluhu Hassan, Rais wa Tanzania
Kwaajili ya kumuenzi Rais Magufuli, kamilisheni mchakato wa Wilaya ya Chato kuwa Mkoa

Kama hamtakuwa mmekidhi vigezo tutawaambia nini cha kufanya ili muweze kuwa Mkoa

Hapa Rais Magufuli tunazika kiwiliwili chake tu lakini mawazo, falasafa na mipango yake itaendelea kuwepo

Falsafa ya hapa ni kazi tu, itaendelea kuwepo na itaendelea kufanya kaziPia soma>>

Askofu Niwemugizi: Rais Magufuli aliagiza nirejeshewe Passport yangu na alisema 'Wewe ni Askofu wangu utanizika'
 
Kuongoza nchi sio jambo rahisi sana.

Nawaza mtu ana mke na watoto wawili ila hawezi kuongoza familiya migogoro kibao, sembuse Magufuli kuongoza hili linchi looote? Lawama zote kwake?

Wewe unaeshindwa kuongoza familiya usimame kumuhukumu Magufuli?

Nahisi Magufuli kaishi maisha magumu pale Ikulu, wabaya wake wote wenda waliishi nae.

Sisi hatuwezi kujua ni makubwa gani alikuwa akiyapitia ila mtu anamuhukumu tu.

Wacheni akahukumiwe mbinguni ila sisi ambao tuko hai tukae kimya. Kile kiti cha Urais sio chepesi kukikalia ukawa na amani ya moyo.

Kinachomponza Magufuli ni the so called " employer's liabbility. Yaan sometimes analazimika kubeba dhambi za watu wengine.

Kila binadamu ana mapungufu yake hivyo basi itoshe kusema that man was a good person.

Ameniuma sana coz nahisi alipitia mengi ambayo yalikuwa nje ya uwezo wake.

Hizi movie tunazoziona zinatosha kujua Rais au mfalme anapitia maisha gani magumu wakati akiwatumikia watu wake.

Lala salama Magufuli huko uendako hakuna majungu, matusi, lawama ni kusinzia tu.
Katika maisha ya baadae (kuzaliwa upya) ningependa nije nikuzae uwe kati ya watoto wangu nitakaojaliwa.

R.I.P J.P.M
 
RAIS Samia Suluhu Hassan leo ataongoza waombolezaji kumzika Rais wa Serikali ya Awamu ya Tano, John Magufuli...
RIP jabari, Jembe tutakumisi Sana tunajua magenge ya kifisadi yanajiandaa.Mh Samia kuwa macho na hayo magenge usikubali kuyumbishwa ss tuko nyuma yako.
 
Kwa hiyo Sala ya mazishi itaongozwa na Askofu Niwemugizi au Rais wa Baraza la Maaskofu (TEC)?.. Maana nimesikiliza East Africa Radio asubuh hii wamesoma ratiba ya leo na wamesema Sala itaongozwa na Rais wa TEC
 
Hatimaye mwamba kulazwa leo milele. Sitakusahau kamwe kwa yote uliyotenda.
 
Back
Top Bottom