Aliyekuwa Rais wa Tanzania, Hayati Dkt. John Magufuli azikwa Chato mkoani Geita

Mmmh
IMG-20210325-WA0088.jpg
 
Aliyepo Karibu na Kwaya Master hapo Uwanja wa Magufuli amuambie waimbe wimbo wa Kweli Ni Huzuni.
 
Kuongoza nchi sio jambo rahisi sana.

nawaza mtu ana mke na watoto wawili ila hawezi kuongoza familiya migogoro kibao,sembuse magufuli kuongoza hili linchi looote? Lawama zote kwake?
Wewe unaeshindwa kuongoza familiya usimame kumuhukumu magufuli?

Nahisi magufuli kaishi maisha magumu pale ikulu, wabaya wake wote wenda waliishi nae.
Sisi hatuwezi kujua ni makubwa gani alikuwa akiyapitia ila mtu anamuhukumu tu.

Wacheni akahukumiwe mbinguni ila sisi ambao tuko hai tukae kimya. Kile kiti cha urais sio chepesi kukikalia ukawa na amani ya moyo.

Kinachomponza magufuli ni the so called " employer's liabbility. Yaan sometimes analazimika kubeba dhambi za watu wengine.

Kila binadamu ana napungufu yake hivyo basi itoshe kusema that man was a good person.

Ameniuma sana coz nahisi alipitia mengi ambayo yalikuwa nje ya uwezo wake.

Hizi movie tunazoziona zinatosha kujua Rais au mfalme anapitia maisha gani magumu wakati akiwatumikia watu wake.

Lala salama magufuli huko uendako hakuna majungu, matusi, lawama.ni kusinzia tu.
Katika maisha ya baadae (kuzaliwa upya) ningependa nije nikuzae uwe kati ya watoto wangu nitakaojaliwa.

R.I.P J.P.M
Na katika hao watoto utakao wazaa naomba hawa nao wawepo.

1. Ben Saanane.

2. Yule mwandishi wa habari gazeti la mwananchi.

3. Wale walio fungwa kwenye viroba

Nk nk nk.
 
Hizi redio kuna wakatoliki lakini ni wajinga hawachambui na ku clarify vizuri.

Kinachotokea ni hiki.

Kwanza kutakuwa na misa kama kawaida. Misa huwa inaisha mkishamaliza kukomunika halafu padri anasema NENDENI NA AMANI.

Hiyo misa ndiyo itasomwa na askofu Nyaisonga.

Kisha baada ya misa maiti hupelekwa makaburini kuzikwa. Kabla ya kuzikwa huwa pale mskaburini huwa kuna taratibu fulani za mazishi. Hizi ndizo zinaitwa ibada na nduzo zitaongozwa na askofu NiweMugizi.

Kwa hiyo Sala ya mazishi itaongozwa na Askofu Niwemugizi au Raisi wa Baraza la Maaskofu (TEC)?.. Maana nimesikiliza East Africa Radio asubuh hii wamesoma ratiba ya leo na wamesema Sala itaongozwa na Rais wa TEC
 
Misa takatifu ya kumuombea hayati Magufuli inaongozwa na Rais wa TEC baba askofu mkuu Nyaisonga.

RIP Magufuli!
 
Misa takatifu ya kumuombea hayati Magufuli inaongozwa na Rais wa TEC baba askofu mkuu Nyaisonga.

RIP Magufuli!
Niwemugizi atakuwepo kama kawa kuchagiza hapa na pale wakati wa ibada ya kumsindikiza aliyemnyang'anya passoport na kuhoji uraia wake.

Halafu inaonekana bado upo Kihesa milimani umeganda kwenye tv yako ya chogo unaangalia tbc kama mm huku ukijidai kuleta uchambuzi uchwara hapa jukwaani
 
Na katika hao watoto utakao wazaa naomba hawa nao wawepo.

1. Ben Saanane.

2. Yule mwandishi wa habari gazeti la mwananchi.

3. Wale walio fungwa kwenye viroba

Nk nk nk.
Kabisa Mungu akipenda nao ni wazae tena wazaliwa mapacha wa kiume.
 
Back
Top Bottom