Alipokufa Sokoine hapakuwepo mitandao ya kijamii lakini kuna Wanasiasa wawili walisingiziwa kuhusika. Hii tabia ilianza zamani

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,944
141,919
Kwa wale wahenga akina Pascal Mayalla, Mrangi, Mmawia na mzee Mgaya mtakumbuka baada ya aliyekuwa waziri mkuu hayati Sokoine kufa kwa ajali ya gari Morogoro kuna wanasiasa wawili walisingiziwa kuhusika na kifo chake.

Wakati ule hapakuwepo mitandao ya kijamii lakini uzushi ule ulisambaa nchi nzima.

Ninachotaka kusema hii tabia mbaya ya kusingiziana mambo mabaya na hasa ya kuuwa ni lazima ikemewe vikali.

Hata alipokufa makamu mwenyekiti wa CHADEMA Hayati Chacha Wangwe kuna watu walisingiziwa kuhusika na hata akina Mwita Waitara wakapigwa mawe kule Tarime.

Nampongeza sana Rais Samia kwa kukemea tabia hii hadharani.

Kazi Iendelee
 
Jo zinakurudi au nawe ni katika lile kundi kubwa la vinyonga?


giphy.gif
 
Naona unajaribu kutetea kundi lenu la kina MWANA HARAKATI WA HURU.
 
Mtu kafa kwa COVID-19. Yupo 6 metres deep. Watakaoiga tabia yake soon nao watamfuata huko chini, asema Bwana wa majeshi!
Chapter closed.
 
Back
Top Bottom