Nalipongeza Jeshi la Tanzania kwa kushirikiana na interpol kwa kumuweka Huyu mfanyibiashara maarufu mikononi, ila angalizo - money can buy anything!
Ingependeza Kama wangepewa interview live ili ijulikane Nani hasa aliyefanya Yale mauaji ya Yule Kijana Na kutoa utata Wa Papa Msofe kuendekea kuwekwa ndani
Serikali ingekuwa na wanasheria wazuri tayari huyu jamaa hukumu ya kifo ilikuwa inamhusu sana pamoja na mwenzake papa msofe, hata kama ya kifo isingewahusu basi kifungo cha muda mrefu kingewahusu lakini kwa sababu ya ofisi ya mwanasheria wa serikali kupeleka wanasheria wasiokuwa na uzoefu kupingana na watu kama kina Marando si ajabu tukasikia hana kesi ya kujibu.
ni kweli kwamba amekamatwa na hata kamishana wa makosa ya jinai wamesema tayari wanafanya utaratibu wa kumsafirisha ili kuja kusomewa makosa yake. kwangu mimi hawa matajiri wafanya biashara ambao wanapata hela zao kwa njia za utata sijui kwann nchi imeendelea kuwalea mpaka wa leo. mbaya zaid wachaga wengi hii kwao ni kawaida yaani watu wana hela ambazo hazijulikani uhakika wake na zimepatikana vipi kumbe wizi tu.
hivi wewe wafikir leo wamempata si bahati mbaya tu kwamba wamempata?? imagine aliweza kusafiri kwa hati bandia mara ngapi akiwa anatafutwa??
inaelekea kuna syndicate kubwa sana ndani yake. mm toka nazaliwa niko shule ya msingi moshi huko huyu bwana anajulikana ni mwizi kajenga ghorofa la kifahari mailisita mferejini toka miaka ya 90 imagine miaka hiyo anajenga hilo ghorofa ilijulikana kwamba ni mpigaji lakin hakuwah hata kutaifishiwa hilo ghorofa liko na ni zuri tafikiri hekalu. kafugwa sana huyu bwana bahati mbaya wenzie wote wameshakufa waliokuwa wapigaji wenzie akina BENSON et al yaani basi tu hi nchi ukiwa mwizi unapendwa ukiwa raia mwema unanyanyasika.
ni kweli kwamba amekamatwa na hata kamishana wa makosa ya jinai wamesema tayari wanafanya utaratibu wa kumsafirisha ili kuja kusomewa makosa yake. kwangu mimi hawa matajiri wafanya biashara ambao wanapata hela zao kwa njia za utata sijui kwann nchi imeendelea kuwalea mpaka wa leo. mbaya zaid
wachaga wengi hii kwao ni kawaida yaani watu wana hela ambazo hazijulikani uhakika wake na zimepatikana vipi kumbe wizi tu.
hahhahhah! umenifanya nicheke kwa sauti mweeh!
hawa ni washenzi tu hawana maan yyte hawa wameshaiba sana mpaka wamejenga maghorofa vijijini. huyu jamaa ni mshenzi sana muulize mtu yte anayetokea moshi maeneo ya mferejini atakwambia alivyo mshenzi. lakini kalelewa utafikiri lulu.
Mfanyabiashara maarufu nchini, Alex Massawe ambaye alikuwa anatafutwana Polisi wa Tanzania kwa muda mrefu, amekatwa Dubai, Falme za Kiarabu (UAE). Mkuu wa la Shirika la Polisi laKimataifa (Interpol), Tawi la Tanzania, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP), Gustav Babilealiliambia gazeti hili jana kwamba Massawe alikamatwa kati ya Juni 20 na 25 mwaka huu kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Dubai akitokea Afrika Kusini. Babile alisema hivi sasa walikuwa wanaandaa taratibu za kumrudisha nchini ambako amekuwa akisakwa kwa muda mrefu. Ombi la kuleta mhalifu nchini kutoka nje ya nchi (extradition request), lina hatua ndefu. Unajua kuna mlolongo wa taratibu za kutekeleza ili Massawe aletwe. Kwanza lazima Polisiwa Tanzania watoe tangazo kwa Interpol kuhusu kumsaka mtu huyo ili aletwe, alisema Babile. Alisema Massawe alikamatwa wakati akifanyataratibu za ukaguzi baada yakuwasili UAE. Habari zilizofikia gazeti hili mapema kutoka Dubai zilieleza kuwa Massawe alikamatwa na maofisa wa usalama wa UAE kutokana na alama zake za vidole na kuonyesha kuwa alikuwamo kwenye orodha ya watu waliokuwa wanasakwa na Interpol. Massawe ambaye anamiliki majumba na biashara ya utalii katika Miji ya Arusha, Dar es Salaam na Moshi, inadaiwa kwamba alikutwa na pasi tatu bandia za kusafiria zilizokuwa na majina tofauti wakati alamazake za vidole zilionyesha anaitwa Alex Massawe. Maofisa wa Usalama wa uwanja wa ndege walimuuliza kuwa wewe ndiye Alex Massawe? Alikanalakini alielezwa kuwa alama za vidole vinaonyesha anaitwa hivyo, kilidokeza chanzo cha habari hizi kwa simu kutoka Dubai. Hata hivyo, Babile alisema hakuwa na taarifa za Massawe kukutwa na pasi bandia za kusafiria. Uvumi wa Aprili Mapema Aprili 27, mwaka huu kulikuwa na habari kwamba Massawe amekamatwa katika mji mmojawapo ulioko katika Pwani ya Afrika Kusini. Habari hizo za kukamatwa kwa Massawe, ambaye pia hufadhili masuala ya kisiasa na michezo, zilisambaa kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii ya Facebook, Twitter na Jamii Forum. Kulikuwa kuna mkanganyiko wa taarifa huku wengine wakidai alinaswa akiwa ndani ya boti huko Afrika Kusini, wengine wakidai alikamatwa wakati akijaribukuingia Msumbiji akitokea Malawi. Akizungumzia hilo Babile alisema huo ulikuwa ni uzushi na baada ya kuzisikia taarifa hizo walifuatilia katika maeneo aliyohusishwa kukamatwa na kubaini kwamba hapakuwa na ukweli wowote. Kwa nini Massawe anatafutwa Aprili 4 mwaka huu, mfanyabiashara huyo alitajwa mahakamani katikakesi ya mauaji ya mfanyabiashara Onesphory Kituly ambaye aliuawa katika mazingira ya kutatanisha Novemba 6, 2011 akiwa nyumbani kwake Magomeni, Dar es Salaam. Katika kesi hiyo ambayo mshtakiwa wa kwanza ni mfanyabiashara maarufu, Abubakar Marijani Papaa Msofe na mshtakiwa mwingine, Makongoro Joseph Nyerere alitoa malalamiko mbele ya Hakimu Mkazi, Agnes Mchome baada ya Wakili wa Serikali, Mwanaisha Kombo kudai upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika na kuomba tarehe mpya ya kuitaja. Mshtakiwa huyo, aliomba jalada la kesi yao lipelekwe mahakamani hapokwa ajili ya kulifanyia kazi na kutuhumu kuwa ndugu wa marehemu Kituly hawataki maendeleo ya kesiyao hadi Massawe akamatwe. By: MCL
hivi wewe wafikir leo wamempata si bahati mbaya tu kwamba wamempata?? imagine aliweza kusafiri kwa hati bandia mara ngapi akiwa anatafutwa??
inaelekea kuna syndicate kubwa sana ndani yake. mm toka nazaliwa niko shule ya msingi moshi huko huyu bwana anajulikana ni mwizi kajenga ghorofa la kifahari mailisita mferejini toka miaka ya 90 imagine miaka hiyo anajenga hilo ghorofa ilijulikana kwamba ni mpigaji lakin hakuwah hata kutaifishiwa hilo ghorofa liko na ni zuri tafikiri hekalu. kafugwa sana huyu bwana bahati mbaya wenzie wote wameshakufa waliokuwa wapigaji wenzie akina BENSON et al yaani basi tu hi nchi ukiwa mwizi unapendwa ukiwa raia mwema unanyanyasika.
Dar es Salaam. Mfanyabiashara maarufu nchini, Alex Massawe ambaye alikuwa anatafutwa na Polisi wa Tanzania kwa muda mrefu, amekatwa Dubai, Falme za Kiarabu (UAE).
Mkuu wa la Shirika la Polisi la Kimataifa (Interpol), Tawi la Tanzania, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP), Gustav Babile aliliambia gazeti hili jana kwamba Massawe alikamatwa kati ya Juni 20 na 25 mwaka huu kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Dubai akitokea Afrika Kusini.
Babile alisema hivi sasa walikuwa wanaandaa taratibu za kumrudisha nchini ambako amekuwa akisakwa kwa muda mrefu.
Ombi la kuleta mhalifu nchini kutoka nje ya nchi (extradition request), lina hatua ndefu. Unajua kuna mlolongo wa taratibu za kutekeleza ili Massawe aletwe. Kwanza lazima Polisi wa Tanzania watoe tangazo kwa Interpol kuhusu kumsaka mtu huyo ili aletwe, alisema Babile.
Alisema Massawe alikamatwa wakati akifanya taratibu za ukaguzi baada ya kuwasili UAE.
Habari zilizofikia gazeti hili mapema kutoka Dubai zilieleza kuwa Massawe alikamatwa na maofisa wa usalama wa UAE kutokana na alama zake za vidole na kuonyesha kuwa alikuwamo kwenye orodha ya watu waliokuwa wanasakwa na Interpol.
Massawe ambaye anamiliki majumba na biashara ya utalii katika Miji ya Arusha, Dar es Salaam na Moshi, inadaiwa kwamba alikutwa na pasi tatu bandia za kusafiria zilizokuwa na majina tofauti wakati alama zake za vidole zilionyesha anaitwa Alex Massawe.
Maofisa wa Usalama wa uwanja wa ndege walimuuliza kuwa wewe ndiye Alex Massawe? Alikana lakini alielezwa kuwa alama za vidole vinaonyesha anaitwa hivyo, kilidokeza chanzo cha habari hizi kwa simu kutoka Dubai. Hata hivyo, Babile alisema hakuwa na taarifa za Massawe kukutwa na pasi bandia za kusafiria.
Uvumi wa Aprili
Mapema Aprili 27, mwaka huu kulikuwa na habari kwamba Massawe amekamatwa katika mji mmojawapo ulioko katika Pwani ya Afrika Kusini.
Habari hizo za kukamatwa kwa Massawe, ambaye pia hufadhili masuala ya kisiasa na michezo, zilisambaa kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii ya Facebook, Twitter na Jamii Forum. Kulikuwa kuna mkanganyiko wa taarifa huku wengine wakidai alinaswa akiwa ndani ya boti huko Afrika Kusini, wengine wakidai alikamatwa wakati akijaribu kuingia Msumbiji akitokea Malawi.
Akizungumzia hilo Babile alisema huo ulikuwa ni uzushi na baada ya kuzisikia taarifa hizo walifuatilia katika maeneo aliyohusishwa kukamatwa na kubaini kwamba hapakuwa na ukweli wowote.
Kwa nini Massawe anatafutwa
Aprili 4 mwaka huu, mfanyabiashara huyo alitajwa mahakamani katika kesi ya mauaji ya mfanyabiashara Onesphory Kituly ambaye aliuawa katika mazingira ya kutatanisha Novemba 6, 2011 akiwa nyumbani kwake Magomeni, Dar es Salaam.
Katika kesi hiyo ambayo mshtakiwa wa kwanza ni mfanyabiashara maarufu, Abubakar Marijani Papaa Msofe na mshtakiwa mwingine, Makongoro Joseph Nyerere alitoa malalamiko mbele ya Hakimu Mkazi, Agnes Mchome baada ya Wakili wa Serikali, Mwanaisha Kombo kudai upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika na kuomba tarehe mpya ya kuitaja. Mshtakiwa huyo, aliomba jalada la kesi yao lipelekwe mahakamani hapo kwa ajili ya kulifanyia kazi na kutuhumu kuwa ndugu wa marehemu Kituly hawataki maendeleo ya kesi yao hadi Massawe akamatwe
tamaa ndio zinawasumbua hawa,mtu kama alex massawe kwa fedha alizonazo asingetakiwa tena aanze kudhulumu nyumba tena ya gharama ndogo kama hiyo,wahenga hawakukosea waliposema jasiri haachi asili,yule kesha zoea kutoa roho za watu ili kujipatia kipato hvy ni ngumu sana roho yake kuachana huyo ibilisi mpaka siku anaingia kaburini.
Ile ndio kazi yake haswa!sasa ataachaje,pale alipoanza fadhili majambazi miaka ya 90 ni baada ya kupata fedha nyingi kwa mkono wake ndipo baadaye akawa mtu wa michongo lakini kabla ya hapo alikuwa anashika moto mwenyewe,waulizeni wazee wajanja wa manzese watakuambieni!
Kwanza nianze kuhakikisha hii habari kuwa ni kweli hata East Africa Radio wameirusha mda si mrefu. Alex Massawe anakabiliwa na tuhuma za mauwaji ya mfanyabiashara ambayo pia Papaa Msofe anahusika. Habari zilizopo ni kuwa mfanyabiashara aliyeuliwa alikopa fedha (inasemekana ni kama mil 200, ila sina uhakika na hii amount) kutoka kwa ALex massawe na akaweka bond nyumba yake iliyopo maeneo ya magomeni. Akamkabidhi Alex masawe hati ya nyumba ikiwa ni sehemu ya mkataba wa mkopo huo. Mfanyabiashara alipotaka kurizudisha zile fedha Alex massawe akawa anapiga chenga hataki kuzipokea kwa madhumuni ya kuupitisha muda riba iwe kubwa jamaa ashindwe kulipa halafu ajihalalishie kuichukua nyumba. Marehemu akawa mjanja akaenda kuiwakilisha zile fedha kwa mwanasheria aliyewafungia mkataba wa mkopo. Baada ya Alex massawe kuona anazidiwa ujanja ndo akaanza kutumia mabavu na kumuuzia ile nyumba Papaa msofe ilihali akijua hana umiliki halali. Baada ya mfanyabiashara kuuawawa, papaa msofe ndo akawa anaighasi familia ya marehemu kuwa hiyo nyumba kashauziwa hivyo watoke na atakuja kuwatoa kwa nguvu. Mke wa marehemu akaenda moja kwa moja kwa Said Mwema na kuilezea habari nzima nzima tangu makubaliano ya mkopo na kuuliwa kwa mumewe na vitisho anavyopata toka kwa wauwaji wa mumewe. Kifupi hili ndo saga lenyewe na kesi ya Papa msofe ilikuwa haiwezi kwenda popote hadi alex massawe atapopatikana kwa sababu ni mtuhumiwa mkuu pia kwenye kesi hii.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.