Alex Massawe kakamatwa!

Alex Massawe kakamatwa!

Serikali ingekuwa na wanasheria wazuri tayari huyu jamaa hukumu ya kifo ilikuwa inamhusu sana pamoja na mwenzake papa msofe, hata kama ya kifo isingewahusu basi kifungo cha muda mrefu kingewahusu lakini kwa sababu ya ofisi ya mwanasheria wa serikali kupeleka wanasheria wasiokuwa na uzoefu kupingana na watu kama kina Marando si ajabu tukasikia hana kesi ya kujibu.

Suala siyo uzoefu hapo. Ni pesa. Pesa inavuruga kila kitu na mwenye akili anakuwa --------
 
ndo mana mimi nawambia watu mimi tajiri wanakataa kisa naendesha Suzuki swift...lakini ni ya kwangu sijakopa wala sijazulumu....sasa haya majamaa yanajidai yana hela halafu kumbe yameipata kwa shortcut namna hii...bongo wenye kujua kuatafuta hela na kutengeneza utajiri wachache sana...
 
Hiyo story ya huyo alex masawe ni noma jamaa ni kama mafia flan,ingia kwenye interest zake akuangamize
 
hivi wewe wafikir leo wamempata si bahati mbaya tu kwamba wamempata?? imagine aliweza kusafiri kwa hati bandia mara ngapi akiwa anatafutwa??

inaelekea kuna syndicate kubwa sana ndani yake. mm toka nazaliwa niko shule ya msingi moshi huko huyu bwana anajulikana ni mwizi kajenga ghorofa la kifahari mailisita mferejini toka miaka ya 90 imagine miaka hiyo anajenga hilo ghorofa ilijulikana kwamba ni mpigaji lakin hakuwah hata kutaifishiwa hilo ghorofa liko na ni zuri tafikiri hekalu. kafugwa sana huyu bwana bahati mbaya wenzie wote wameshakufa waliokuwa wapigaji wenzie akina BENSON et al yaani basi tu hi nchi ukiwa mwizi unapendwa ukiwa raia mwema unanyanyasika.
Kwa hii post mkuu kama nakutambua hivi. Wewe wa pale mferejini na sasa ni mganga eeh? Aika-mbee!!
 
Ile ndio kazi yake haswa!sasa ataachaje,pale alipoanza fadhili majambazi miaka ya 90 ni baada ya kupata fedha nyingi kwa mkono wake ndipo baadaye akawa mtu wa michongo lakini kabla ya hapo alikuwa anashika moto mwenyewe,waulizeni wazee wajanja wa manzese watakuambieni!

Sikuzote nasema watambue kuwa Mungu yupo!
Na ipo siku isiyo na jina....
 
chezea shetani weye!
ili baadae aje ajitape Mungu kambariki wakati alikuwa muuaji, ni hivi shetani habebeki hata sikumoja hata umfanyie nini lazima aje akugeuke uaibike kama yeye.

U a very very very ryt mkuu!!!
 
Suala siyo uzoefu hapo. Ni pesa. Pesa inavuruga kila kitu na mwenye akili anakuwa --------

kwa hili pia me naamini serikali haitakubali kuivua nguo interpol,so pesa zake hapa lazima ziwe zinanuka na sio kunukia,haki lazma itatendeka kwakuwa si polisi wa tz waliomkamata,ni polisi wa kimataifa
 
ile 2006 aliposhikiliwa baada ya JK kuingia madarakani na baadaye kuachiwa kwa kusemwa atakuwa chini ya uangalizi nilijua ataacha uhalifu kumbe hamna kitu!
watu kama hawa wameiteka system nzima ya jeshi la polisi na ndo sababu wametamba kwa muda mrefu.
 
kwanza nianze kuhakikisha hii habari kuwa ni kweli hata east africa radio wameirusha mda si mrefu. Alex massawe anakabiliwa na tuhuma za mauwaji ya mfanyabiashara ambayo pia papaa msofe anahusika. Habari zilizopo ni kuwa mfanyabiashara aliyeuliwa alikopa fedha (inasemekana ni kama mil 200, ila sina uhakika na hii amount) kutoka kwa alex massawe na akaweka bond nyumba yake iliyopo maeneo ya magomeni. Akamkabidhi alex masawe hati ya nyumba ikiwa ni sehemu ya mkataba wa mkopo huo. Mfanyabiashara alipotaka kurizudisha zile fedha alex massawe akawa anapiga chenga hataki kuzipokea kwa madhumuni ya kuupitisha muda riba iwe kubwa jamaa ashindwe kulipa halafu ajihalalishie kuichukua nyumba. Marehemu akawa mjanja akaenda kuiwakilisha zile fedha kwa mwanasheria aliyewafungia mkataba wa mkopo. Baada ya alex massawe kuona anazidiwa ujanja ndo akaanza kutumia mabavu na kumuuzia ile nyumba papaa msofe ilihali akijua hana umiliki halali. Baada ya mfanyabiashara kuuawawa, papaa msofe ndo akawa anaighasi familia ya marehemu kuwa hiyo nyumba kashauziwa hivyo watoke na atakuja kuwatoa kwa nguvu. Mke wa marehemu akaenda moja kwa moja kwa said mwema na kuilezea habari nzima nzima tangu makubaliano ya mkopo na kuuliwa kwa mumewe na vitisho anavyopata toka kwa wauwaji wa mumewe. Kifupi hili ndo saga lenyewe na kesi ya papa msofe ilikuwa haiwezi kwenda popote hadi alex massawe atapopatikana kwa sababu ni mtuhumiwa mkuu pia kwenye kesi hii.
duh!! Ama kweli ndani ya nchi hii kila mtu ni intelijensi. Hadi habari za uvunguni mwa kitanda cha mtu zinajulikana??!! Good.

 
Wapewe hukumu hata ya kufungwa maisha au mahakama ichukue uamuz mgumu
 
Huyu ni msure wake ,na christopher nae kwa mara ya mwisho alikamatwa ameiba gari la JWTZ like son like father

Sent from my BlackBerry 9700 using Jamii Forums

Hee!kweli roho hii ipo kazini,wasipotubu itaendelea vizazi na vizazi
 
hivi wewe wafikir leo wamempata si bahati mbaya tu kwamba wamempata?? imagine aliweza kusafiri kwa hati bandia mara ngapi akiwa anatafutwa??

inaelekea kuna syndicate kubwa sana ndani yake. mm toka nazaliwa niko shule ya msingi moshi huko huyu bwana anajulikana ni mwizi kajenga ghorofa la kifahari mailisita mferejini toka miaka ya 90 imagine miaka hiyo anajenga hilo ghorofa ilijulikana kwamba ni mpigaji lakin hakuwah hata kutaifishiwa hilo ghorofa liko na ni zuri tafikiri hekalu. kafugwa sana huyu bwana bahati mbaya wenzie wote wameshakufa waliokuwa wapigaji wenzie akina BENSON et al yaani basi tu hi nchi ukiwa mwizi unapendwa ukiwa raia mwema unanyanyasika.
gfsonwin naelewa but nadhani lengo na nia yake ilikuwa si aje akamatwe bahati ikiisha. My question is still valid hakujua kuwa vile vimashine vya alama za vidole siyo toys za watoto? Hata hao alokuwa anawahonga alipaswa ajue kuwa wanamlia pesa zake na wana mipaka pia.
 
Last edited by a moderator:
Kuna kitu nimegundua

media ni mahakama inayojitosheleza. Kama media haipogii kelele kitu basi ujui kitapotea .. Familia zijitahidi kuripoti miendelezo ya kesi kwenye media, wakikaa kimya tu imekula kwao.. This is tz..
 
duh!! Ama kweli ndani ya nchi hii kila mtu ni intelijensi. Hadi habari za uvunguni mwa kitanda cha mtu zinajulikana??!! Good.


Mkuu hizi mbona zilishavuja long time tangu walivyomuua jamaa (marehemu). Familia ya marehemu, polisi hata baadhi ya waandishi wa habari za mahakamani wanazo hizi.
 
hahhahhah! umenifanya nicheke kwa sauti mweeh!
hawa ni washenzi tu hawana maan yyte hawa wameshaiba sana mpaka wamejenga maghorofa vijijini. huyu jamaa ni mshenzi sana muulize mtu yte anayetokea moshi maeneo ya mferejini atakwambia alivyo mshenzi. lakini kalelewa utafikiri lulu.
Nikweli kajenga bonge la kasiri hapo mferejini Alex massawe nilifamiana nae wakati huo mzee wangu anamuuzia hilo eneo wakati huo hapo kukiwa na
Machine ya kusagia maindi,
Alex bana kibosho wa mjini handsome
 

Attachments

  • 1423657841603.jpg
    1423657841603.jpg
    10 KB · Views: 891
Back
Top Bottom