Alama ya nyota na mwezi misikitini humaanisha nini?

Alama ya nyota na mwezi misikitini humaanisha nini?

Jambo usilo lijua JARIBU kuliuliza kina unachokiona msikitini kina maana take Young
 
Hizi alama hazihusiani na uislamu.Ila zimeanzishwa na wasomi wa Geografia,ili kuonyesha msikiti.Ndio wajenzi wengi wakazitumia ili iwe wepesi zaidi,kwa aliyesoma shule,akiona alama hizi ajuwe ni msikiti na kufuatia na wasiosoma shule,kwa kueleweshwa kwa wanaofajamu.
Ndio maana ukaona hakuna muislamu anayevaa alama hiyo,shingoni,kama wanavyovaa wanaotumia msalaba,wala kuikuta alama hiyo ndani ya msikiti.
Ni alama ya kumrahisishia asiyefahamu jengo linahusika na shughuli gani.Kuna misikiti mingi tu haina alama hiyo.Ni misikiti michache kwa mapendekezo ya wajenzi.
 
Hizi alama hazihusiani na uislamu.Ila zimeanzishwa na wasomi wa Geografia,ili kuonyesha msikiti.Ndio wajenzi wengi wakazitumia ili iwe wepesi zaidi,kwa aliyesoma shule,akiona alama hizi ajuwe ni msikiti na kufuatia na wasiosoma shule,kwa kueleweshwa kwa wanaofajamu.
Ndio maana ukaona hakuna muislamu anayevaa alama hiyo,shingoni,kama wanavyovaa wanaotumia msalaba,wala kuikuta alama hiyo ndani ya msikiti.
Ni alama ya kumrahisishia asiyefahamu jengo linahusika na shughuli gani.Kuna misikiti mingi tu haina alama hiyo.Ni misikiti michache kwa mapendekezo ya wajenzi.
mkuu inamaana hadi msikiti mkubwa na maarufu kama wa mecca unahitaji kutambulishwa na hizo alama?
saudi.jpg
 
Alama ya nyota na mwezi, na, ile picha ya farasi mwenye sura ya mwanamke,ni upuuzi na uzushi mtupu!
Sijui ile jumuia yetu, (ambayo ni jumuia ya chama chetu pia) wanasemaje?
 
Allah alitokea wapi?

Uislamu unajinadi kwamba Allah ndiye Mungu yuleyule aliyejishughulisha ya Wayahudi tokea nyakati za Ibrahimu katika Agano la Kale. Je, jambo hilo ni kweli?

Uislamu ulianza na Muhammad kwenye miaka 600 baada Kristo. Je, kabla yake imani za Waarabu zilikuwaje? Je, yako mambo yoyote kutoka kwenye imani hizo ambayo yaliingia kwenye Uislamu? Kwa maneno mengine, je, Uislamu hauna upagani ndani yake?

Fuatana nami kwenye makala haya marefu yanayochambua chimbuko la Uislamu ili tuweze kuona iwapo upo uhusiano wowote kati ya Uislamu na upagani uliokuwa ukitawala miongoni mwa jamii za Waarabu kabla ya kutokea kwa Muhammad?


Asili Ya Allah

Jamii za wanadamu KOTE duniani zimekuwa na kawaida ya kujiuliza ni wapi ulimwengu huu umetokea, nini maana ya maisha na wapi watu huenda baada ya kufa. Matokeo yake, kila jamii ilifikia kuamini kuwa kuna aliye na nguvu (au walio na nguvu) kuliko wanadamu wote ambao ndio wanapaswa kuabudiwa na kuombwa msaada pale matatizo yanapotokea.

Hawa wenye nguvu wakajulikana kwa majina mbalimbali kwenye jamii tofauti. Vilevile, kila jamii ilianzisha utaratibu maalum wa kuwasiliana na hawa wenye nguvu, yaani miungu.

Lakini jambo moja ni dhahiri, kwamba UKIACHA JAMII YA WAYAHUDI PEKE YAO, jamii zote za wanadamu zilizobakia duniani – iwe ni Afrika, Ulaya, Asia, n.k. - zimeanzia kwenye ibada za kipagani. Jamii hizi ziliabudu miungu mbalimbali. Na miungu hii iliwakilishwa na vitu kama vile milima, miti mikubwa, jua, mwezi, majoka makubwa, sanamu, wafalme, n.k. Kwa mfano, Warumi walikuwa na miungu kama vile artemi, jupiter, minerva, atlas, n.k. Tazama hapa. Wagiriki walikuwa na miungu kama vile chronos, dionysus, eros, ares, appolo, hermes, poseidon, n.k. Tazama hapa. Wahindi wana miungu kama vile durga, ganesha, garusha, brahma, n.k. Tazama hapa. Imani hizi za kipagani ziliweza hata kukua sana na kuenea maeneo mengi. Kwa mfano, imani ya ubudha ni imani ya kipagani lakini iliweza kuenea sehemu kubwa sana ya Asia – India, Japan, Sri Lanka, Uchina, n.k.

Kwa hiyo, jamii za Kiarabu, kama ilivyo kwa wanadamu wengine, vilevile hazikuwa tofauti. Jamii hizi nazo zilikuwa zina ibada zao za kipagani.

Waarabu walikuwa wakiabudu kile ambacho kinajulikana leo kama “star family”, au “familia ya nyota.” Tazama hapa. Inaitwa ‘familia ya nyota’ kwa sababu walichukulia miungu yao kwa tabia za kibinadamu. Mwezi ulichukuliwa kuwa ni mungu mwanamume na jua kama mke wa mwezi. Kisha hawa walizaa watoto. Kwa mfano, waliaminika kuwa walikuwa na mabinti watatu waliojulikana kwa majina ya al-lat, al-uzza na manat.

Ndiyo maana hata quran ikasema: Have you considered Al-Lat and Al- Uzzah, and another, the third (goddess) Manat? (Sura 53:19-20).

Yaani: Mmemwona Al-Lat na Al – Uzza, na mwingine, wa tatu (mungu mke) Manat?

Na hata Muhammad alikuwa akiabudu miungu hii kabla ya kuanzisha Uislamu. Tunasoma kutoka Hisham al-Kalbi, Kitab al-Asnam (Book of Idols), uk.17 kwamba:


'We have been told that the Apostle of Allah once mentioned al-Uzza saying, "I have offered a white sheep to al-'Uzza, while I was a follower of the religion of my people."

Yaani:
Tulishaambiwa kwamba Mtume wa Allah aliwahi kumtaja al-Uzza akisema, “Nilitoa kondoo mweupe kwa al-Uzza, wakati nilipokuwa nikifuata dini ya watu wangu.” Watu wake ni Waquresh.

Jina Allah linatokana na al-llah. Al ni kama neno la Kiingereza, yaani article ‘a’; na ilah ni mungu. Kwa hiyo, al-ilah maana yake ‘a god’ au tu mungu kwa Kiswahili – maana Kiswahili hakina neno linalofanana na ‘a’.

Kwa sababu lugha huenda ikibadilika, ndipo jina hili likafupishwa na akuwa ‘allah’. Ni kama unavyoona kwenye Kiswahili utasikia mtu akisema ‘mambo ndo ivo bwana.’ Kumbe ‘ndo ivo’ ni kifupi cha ‘ndiyo hivyo’. Huenda miaka hamsini au mia ijayo watu hawatajua kuwa kumbe asili ya ‘ndo ivo’ ni maneno ‘ndiyo hivyo.’

Sasa, allah alikuwa ni nani? Allah alikuwa ni mungu mwezi, ambaye tumesema mke wake alikuwa ni jua na watoto (mabinti zao) walikuwa ni al-lat, al-uzza na manat. Hawa ndio walik uwa wakichukuliwa kuwa ni miungu wakuu miongoni mwa mamia ya miungu iliyokuwa ikiabudiwa na Waarabu kabla ya Uislamu – kipindi ambacho Waislamu hukiita ‘Jahiliyah’.

Na jina hili ‘Allah’ ni jina la kiume (masculine); na ndiyo maana binti yake mmoja akaitwa ‘al-lat’, ambalo ni jina la kike (feminine). Ni kama unavyoona Francis na Fortunatus ni wanaume lakini Francisca na Fortunata ni wanawake – japo majina haya asili yake ni ileile. Ndivyo ilivyo kwa Allah na al- Lat. Yote ni jina lilelile, tofauti tu kwamba moja ni la kiume na jingine la kike.

Mojawapo ya jamii iliyokuwa ikimwabudu sana Allah ilikuwa ni jamii ya Waquresh, ambayo ndiyo jamii alikotokea Muhammad.

Watu wasioelewa wanadhani kuwa Allah alijulikana baada ya Muhammad kutokea. Na wengine nao watasema kuwa Allah alijulikana tangu wakati wa Ibrahimu kama anavyojulikana leo. Kama hilo lingekuwa ni kweli, inabidi wajiulize ilikuwaje Allah wa Ibrahimu akapotea hadi ikawa kwamba kuna Allah wa kipagani?

Mathalani, inafahamika wazi kwamba baba yake Muhammad hakuwa mwislamu bali alikuwa mpagani.

Sitashaangaa endapo baadhi ya Waislamu watasema kuwa baba wa Muhammad alikuwa mwislamu. Hata hivyo, huyu mtu alikufa kabla hata ya Muhammad kuzaliwa. Na je, Muhammad mwenyewe anasema nini kuhusiana na baba yake?

Tunasoma hivi:

Anas reported: Verily, a person said: Messenger of Allah, where is my father? He said: (He) is in the Fire. When he turned away, he (the Holy Prophet) called him and said:Verily my father and your father are in the Fire. (Sahih Muslim, Book 001, Number 0398).

Yaani:
Imeripotiwa na Anas: Hakika, mtu mmoja alisema: Mjumbe wa Allah, baba yangu yuko wapi? Akasema: Yuko motoni. Alipogeka kuondoka, (Mtume mtakatifu) akamwita na kusema: Hakika baba yangu na baba yako wako Motoni.

Na swali ambalo tungependa wajiulize ni kuwa, kwa nini baba yake Muhammad, ambaye alikuwa mpagani aliitwa ‘Abdullah’?

Na kwa kuwa ‘Abdullah’ maana yake ni ‘mtumwa wa Allah’, hii ni ishara ya wazi kwamba wapagani wa kipindi cha jahiliyah walikuwa wakimwabudu Allah hadi kufikia kuwapa watoto wao majina kwa heshima ya Allah – kama ambavyo Wayahudi nao walikuwa wakiwapa watoto wao majina kwa heshima ya Mungu wa Ibrahimu, Isaka na Yakobo.

Kwa mfano:
Yoshua – Yahwe ni wokovu;
Yothamu – Yahwe ni mkamilifu;
Yehoahazi – Yahwe ameshikilia;
Hezekia – Yahwe ametia nguvu;
Elisha – Mungu ni wokovu, n.k.

Jibu liko wazi. Allah alikuwa ni mungu wa kipagani aliyeabudiwa kabla ya Uislamu kuja. Na mungu huyu alikuwa ni ‘mungu mwezi’, yaani ‘al-ilah’. Jina lake jingine aliitwa ‘hubal.’ Mungu huyu wa kipagani aliabudiwa kote mashariki ya kati; wala si kwa Waarabu peke yake.

Hili ni jambo ambalo limeshathibitishwa tena na tena na wanaakiolojia – ambao hufukua masalia ya vitu vya kale – hawa wameshafukua vitu vingi sana ambavyo vinaonyesha jinsi kuabudu mwezi na jua na nyota kulivyokuwa kumeshamiri sana katika eneo la mashariki ya kati.

Na ndiyo maana baba yake Muhammad, yaani Abdullah, alikoswakoswa kuchinjwa na babu wa Muhammad, yaani Abdul Muttalib. Abdul Muttalib alitaka kumchinja mwanawe huyo kama sadaka kwa Allah. Lakini mjomba wake Abdullah akamwokoa na hatimaye walichinjwa ngamia 100 badala yake. Na ifahamike kwamba machinjo hayo yalifanyikia kwenye kaaba (hili tutaliangalia huko mbeleni).

Tunaambiwa kwamba:
An arrow showed that it was 'Abdullah to be sacrificed. 'Abdul-Muttalib then took the boy to Al-Ka'bah with a razor to slaughter the boy. Quraish, his uncles from Makhzum tribe and his brother Abu Talib, however, tried to dissuade him. They suggested that he summon a she-diviner. She ordered that the divination arrows should be drawn with respect to 'Abdullah as well as ten camels. … the number of the camels (finally) amounted to one hundred. (Ibn Hisham 1/151-155; Rahmat-ul-lil'alameen 2/89, 90).

Maana yake:

Mshale ulionyesha kwamba Abdullah ndiye aliyetakiwa kutolewa kafara. Kwa hiyo, Abdul Muttalib alimchukua yule kijana hadi kwenye Al-Kaaba pamoja na wembe kwa ajili ya kumchinja. Qura aish, mjomba wake kutoka kabila la Makhzum na kaka yake Abu Talib, hata hivyo, walijaribu kugeuza mawazo yake. Walipendekeza kwamba amwite mwaguzi wa kike. Huyo aliagiza mishale ya uaguzi ichorwe baina ya Abdullah na ngamia kumi … hatimaye idadi ya ngamia ikafikia mia moja.

Ndiyo maana Mungu wa Biblia alikuwa akiwaonya sana wana wa Israeli juu ya tabia za kipagani za jamii zilizowazunguka kuhusiana na masuala ya kuabudu familia ya nyota au jeshi la mbinguni. Kwa mfano, anasema:

….. tena usije ukainua macho yako hata mbinguni, na ulionapo jua, na mwezi, na nyota, jeshi la mbinguni lote pia, ukashawishiwa na kuviabudu, na kuvitumikia, ambavyo Bwana, Mungu wako amewagawanyia watu wote chini ya mbingu zote. (Kumbukumbu la Torati 4:19).


Ikiwa ameonekana katikati yako, ndani ya malango yako mojawapo, upewayo na Bwana, Mungu wako, mtu mume au mke afanyaye yaliyo maovu machoni pa Bwana, Mungu wako, kwa kuvunja maagano yake,….. naye amekwenda kutumikia miungu mingine na kuiabudu, au jua, au mwezi, au vilivyo katika jeshi la mbinguni vyo vyote, nisivyoagiza mimi (Kumbukumbu la Torati 17:2-3).


Kwa maana akapajenga tena mahali pa juu alipopaharibu Hezekia baba yake; akamjengea Baali madhabahu, akafanya Ashera kama alivyofanya Ahabu mfalme wa Israeli. Akajiinama mbele ya jeshi lote la mbinguni na kulitumikia. (2 Wafalme 21:3).


Akajenga madhabahu kwa ajili ya jeshi lote la mbinguni katika behewa mbili za nyumba ya Bwana. (2 Wafalme 21:5).


Akawaondosha wale makuhuni walioabudu sanamu, ambao wafalme wa Yuda waliwaweka ili kufukiza uvumba katika mahali pa juu, ndani ya miji ya Yuda, na katika kila mahali, pande zote za Yerusalemu; na hao pia waliomfukizia uvumba Baali, na jua, na mwezi, na sayari, na jeshi lote la mbinguni. (2 Wafalme 23:5).



… nao wataitawanya mbele ya jua, na mwezi, na jeshi lote la mbinguni, walivyovipenda, na kuvitumikia, na kuandamana navyo, na kuvitafuta, na kuviabudu haitakusanywa pamoja tena, wala kuzikwa; itakuwa ni samadi juu ya uso wa nchi. (Yeremia 8:2).

…. na nyumba za Yerusalemu, na nyumba za wafalme wa Yuda, zilizotiwa unajisi, zitakuwa kama mahali pa Tofethi; naam, nyumba zote ambazo juu ya dari zake wamelifukizia uvumba jeshi lote la mbinguni, na kuwamiminia miungu mingine sadaka za kunywewa. (Yeremia 19:13).


…. na wale walisujudiao jeshi la mbinguni juu ya dari za nyumba; na hao waabuduo, waapao kwa Bwana na kuapa pia kwa Malkamu (Zefania 1:5).

...............................................
Katika mwaka 570 BK, mwaka uleule ambao Muhammad alizaliwa, alikuwapo mtawala mmoja wa dola ya Aksum ya Ethiopia ambaye alikaa Yemen. Huyu aliitwa Abrahah al- Ashram. Inaelezwa kwamba alikuwa na wivu na mji wa Makka kwa jinsi ambavyo watu wengi walikuwa wakienda kuhiji (yaani hija ya kipagani), hivyo na yeye naye akajenga kanisa kubwa kule Sanaa, Yemen akitarajia kuvuta watu wengi, jambo ambalo halikutokea.

Matokeo yake, aliamua kwenda kuvamia Makka kwa lengo la kuiharibu kaaba. Alisafiri na watu wake wengi juu ya kundi kubwa la tembo - ndiyo maana hata mwaka ule ukajulikana kama mwaka wa tembo.

Koo za Kiquresh ziliungana ili kujaribu kuikoa kaaba. Abdul Mutaleb (babu yake Muhammad) aliwaambia watu wakimbilie kujificha milimani wakati yeye na baadhi ya watu walibakia karibu na kaaba.

Lakini kwa sababu ya ukubwa na nguvu ya jeshi la yule Abrahah, Abdul Mutaleb alisema:


"The Owner of this House is its Defender, and I am sure He will save it from the attack of the adversaries and will not dishonor the servants of His House."

Yaani:
Mmiliki wa nyumba hii ndiye atakayekuwa Mlinzi wake, na nina uhakika ataiponya dhidi ya kushambuliwa na maadui na hawatawafedhehesha watumishi wa nyumba yake."

Mapokeo yanasema kwamba wakati Abrahah anasonga mbele kuiendea kaaba, lilitokea kundi kubwa la ndege ambao walianza kumdondoshea mawe kama mvua hadi wakamjeruhi. Hivyo, azma yake ya kuiharibu kaaba haikufanikiwa, badala yake akarudi kwake akiwa ameumizwa.

Sasa, swali ni kuwa, kama wakati ule Muhammad alikuwa bado kichanga, na hivyo Uislamu ulikuwa haujaanza; na pale kwenye kaaba inajulikana kwamba kulikuwa na mamia ya miungu ya kipagani; je, Mmiliki wa Nyumba anayetajwa na Abdul Mutaleb ni nani?

Ni wazi kwamba huyu ni mungu wa kipagani, yaani allah aliyekuwa akiabudiwa na kutumikiwa na Abdul Mutaleb, yaani mungu mwezi.

Na swali kubwa zaidi ni kuwa, Quran inasema katika sura Al-Fil (au Tembo) 105:1-5:


"Have you not seen how your Lord dealt with the owners of the Elephant? Did He not make their treacherous plan go astray? And He sent against them birds in flocks, striking them with stones of baked clay, so He rendered them like straw eaten up."


Yaani:


Kwani hukuona jinsi Mola wako Mlezi alivyo watenda wale wenye tembo? Kwani hakujaalia vitimbi vyao kuharibika? Na akawapelekea ndege makundi kwa makundi, Wakiwatupia mawe ya udongo wa Motoni, Akawafanya kama majani yaliyo liwa!

Swali ni kuwa:
Mambo haya yalitokea wakati Uislamu haupo, bali ulikuwa ni wakati wa upagani. Mtumishi wa mungu wa kipagani Abdul Mutaleb alisema kwamba Mmiliki wa Nyumba ile (kaaba) angeitetea.

Je, Mmiliki wa nyumba aliyetajwa na Abdul Mutaleb alikuwa yupi na Mola wako anayetajwa na Quran kwenye sura hii ni yupi? Au tuseme kulikuwa na miungu miwili iliyoshirikiana kumpiga mawe Abrahah na tembo wake?

Abdul Mutaleb hakumjua Allah wa Muhammad, kwa hiyo kwa namna yoyote ile hangeweza kumtaja huyo (kama kweli Allah wa Muhammad ni tofauti na wa Abdul Mutaleb).

Mazingira yote yanaonyesha kwamba mungu mwezi, aliyeabudiwa na Abdul Mutaleb ndiye aliyeilinda kaaba dhidi ya tembo wa Abrahah. Kwa hiyo, aya hii ya Quran haina uwezo wa kujinadi kwamba inamtaja mungu tofauti na huyo!!


Hitimisho


Kama wewe ni Mwislamu, je, haujiulizi inakuwaje kwamba mwezi ndio wenye usemi juu ya mambo mengi ya muhimu kwenu Waislamu?

Kwa nini ni lazima mwezi uonekane ndipo mfungo uanze?
Kwa nini ni lazima mwezi uonekane ndipo mfungo uishe?
Kwa nini alama kuu juu ya kila msikiti ni nusu mwezi na nyota? Ni nini asili ya vitu hivyo?
Japo nimeiona late, ila umeichambua ngoja niiweke kwenye library yangu
 
Mimi ni Mkristo Mkatoliki..nauliza haya mambo mnijibu..je nyota au Mwenzi au Jua ni alama za shetani!kama ni alama za kishetani ina maana hakuziumba Mwenyenzi Mungu?kama hakuziumba Mwenyenzi Mungu ina maana muumba Wa mbingu na nchi ni shetani?kama hizo alama ni zakishetani ina maana dunia yetu mtawala mkuu ni shetani?..ni muhimu sana kutofautisha sanamu na vitu vilivyoumbwa na Mwenyenzi Mungu Mkuu.Baba Wa viumbe vyote na mambo yote tujitaidi sana kumpa Heshima kwa Hekima na busara zake za kuumba jamani.napenda sana Kumwambia Mwenyenzi Mungu Mkuu samahani kwa mambo yote tunayokuumiza.
 
mkuu inamaana hadi msikiti mkubwa na maarufu kama wa mecca unahitaji kutambulishwa na hizo alama?
saudi.jpg
Nina uhakika umenielewa,hizi alama huwa wanapendezesha wachoraji ramani,wana Geografia,ili iwe ni utambulisho wa msikiti.Mbali ya msikiti kuwepo hapo,wapo wapigaji picha,ambao husambaza picha sehemu mbalimbali,kama wewe ulivyoitumia hiyo picha.Kwa asiyeelewa ni picha ya nini,kama ni msomi ni wepesi kwake kuelewa,hii ni picha ya nyumba ya ibada ya waislamu au msikiti.
Katika kuweka alama ya utambulisho,hakuhitaji ukubwa au udogo wa kitu,ndio maana ukaona kuna alama za 'Railways Crossing' (x) hata ikiwa kunapita mabehewa ya ukubwa gani.
 
Think twice. Ni alama ya kishetani. Hata Katoliki wanazo sana. Dini ya kweli ni ile isiyokuwa na alama, maana Mungu wa Moses hakuwahi kuhimiza wachonge sanamu wala kitu chochote chenye mfano wa Mungu. Hizo alama zinamuwakilisha shetani na siyo Mungu.
Think twice onesha andiko linalosema hayo

Wewe utakuwa mlokole
 
Sasa Wayahudi wanavyo tumia Nyota hata kwenye bendera Yao ni Pia Ushetani, jamani watanzania lini mtastaarabika? Mnakuja na hoja hazina hata maana. Kama mtu anajuwa Maana ya kitu symbol au NEMBO ndio iliwekwa tu na. Baadhi ya watu kufahamisha kuwa ni msikiti au Kanisa kumbuka kuna waislaam waarabu na kuna wakristo waarabu na makanisa Yao na.MISIKITI Yao imefanana kidogo Sasa kuutafautisha baina ya msikiti na Kanisa wanaweka NEMBO na mwezi na Nyota ni no kuashiria Kuingia Tarehe mpya ndio maana wameweka crescent Moon sio full moon na Nyota hii Heineken kila mwezi unayo Andama Lazima mwezi Hilal unaonekana na Nyota ya Jioni Venus iko juu yake Sasa kwani NYOTA NA MWEZI NI USHETANI? QURAN mara nyingi Mwenye Enzi Mungu huwa anaaapia kwa vitu alivyo viumba kama vile Nyota, Wanyama nk
 
Kwa wasomi wa Biblia watakukatalia hili na kama kuruani ilikuambia kuwa Musa hakutengeneza Sanamu basi ilikudanganya. Hata Hekalu la Mfalme Suleiman lilijazwa Sanamu mbali mbali na Utukufu wa Mungu ulishuka. ninapomkubali Muhammad ni pale anapowaasa kwenye kurani kuja kutafuta ukweli zaidi kwa watu wa Kitabu.
Asalaam Alyekum
Hizo alama first of all hazimo ndani ya msikiti ,pili baadhi tu wameweka nje ,pia hazipo kwenye sunna au Quran ,..point wanaotoa ni utambulisho kuwa sehem Fulani kuna msikiti mfano nikienda sao Paolo kwenye matembezi yng ya kuutafuta msikiti nikiona kiashirio hicho bas ntajua sehem fulan kuna msikiti ,

Tatu ni haraam kwenye nyumba yeyote kubandikwa picha au sanamu lolote mafundisho yanasema hvy kama unasema mafundishi ya mussa yanapinga masansmu basi uislamu&mussa wamefungana kimafundisho sabb according to Islam nyumba yenye sanamu au picha malaika haingii
 
mkuu inamaana hadi msikiti mkubwa na maarufu kama wa mecca unahitaji kutambulishwa na hizo alama?
saudi.jpg
Hawa watu huwa wana uongo uongo fulani hivi amaizing. Kwa nini wanajiografia watumie alama za mwezi na nyota? Adhana haitoshi kuelekeza msikiti ulipo? Hiyo ni ishara ya allah.
 
Usiongee usiyoyajua. Hiyo alama ilikuwa adopted wakati wa Ottoman Empire na haihusiani chochote na uislam. Uislam ni kuabudu Mungu mmoja pekee aliyeumba mbingu na ardhi hana watoto, wajomba wala wajukuu, hajazaa wala kuzaliwa.

Imekuwa common place watu kuiga hii design mpaka sasa waliowengi (hata baadhi ya waislam wenyewe) wanadhani na sign ya uislam iliopo toka kipindi cha Mtume Muhammad (Rehma na Amani zimshukie juu yake) lakini hapana. Katafute kitabu chochote cha hadith (statement ya Mtume S.A.W) unitafutie hata invented hadith inayosema nyota na mwezi na alama ya uislam halafu niletee.

Ndio maana mpaka leo bendera ya uturuki ina the same symbol ya nyote na mwezi from the Ottomans, wengi wanadhani waturuki wamecopy from Islam but its actually vice versa and many scholars don't recommend hata iwepo maana kuna watu watafikiri kama unavyofikiri wewe

I hope umeelewa
Dats gud nmependa ufafanuzi wako, but umesema "Mungu mmoja pekee aliyeumba mbingu na ardhi hana watoto,wajomba wala wajukuu en hajawahi kuzaa...[emoji15] Men so umezaliwa na nani?
 
Ubarikiwe sana PNC1 kwa kutuelimisha kwa mapana zaidi ya mada iliyopo. Uchambuzi wako wa kina haustahili kujibiwa kishabiki. Umejikita katika utafiti wa theology, archeology, historia, n.k. Anayefikiri anaweza kupinga hoja zako twamuomba ajikite katika medani hizi na atoe ushahidi. God bless yu for upholding the truth.
 
Nafikiri PNC umeeleza vizuri historia ya waraabu ila bahati mbaya hujaeleza historia ya uislamu kama ulivyoaanza 610 AD. Huyo Allah unae mzungumza na alietajwa kwenye uislam sifa zao hazifanani na ndo msingi wa uislamu, pia Allah ametajwa kwa majina 99 Allah likiwa moja wapo ndo maana unamuaona Abdullah humuoni abdulrahman
 
Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.
Kwa hakika alama na ishara hizo hazina umuhimu wala maana yoyote katika kuwekwa katika Misikiti au sehemu nyingine zozote. Kwani wakati wa Mtume (Swalla-Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Maswahaba zake (Radhiya-Allaahu 'anhum) alama
kama hizo zilikuwa hazipo.
Baada ya hapo huenda Waislamu wakaamua kuwa wawe na ishara kama vile Mayahudi
na Manaswara, kwani Mayahudi wana ile ishara ya nyota ya Daudi ambayo ina pembe sita na Manaswara wana ishara ya kuwa na msalaba. Kwa kuwa sisi huwa tarehe zetu za siku na miezi yetu hufuata mwezi, basi baadhi ya Waislam wakaona kuwa waweke hiyo alama ya mwezi kama nembo, lakini kiuhakika haina maana yoyote ya kisheria.
Na Allah Anajua zaidi.
Kwa iyo kitambo hakukuwa na nyota na mwezi....
 
Back
Top Bottom