Alama ya nyota na mwezi misikitini humaanisha nini?

Red Giant

JF-Expert Member
Mar 9, 2012
15,658
20,889
4103820712_cb6440ff56.jpg
mosque-architecture-oriental-half-moon-crescent-sun-mood-dusk-twilight-BWK9PX.jpg
 
Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.
Kwa hakika alama na ishara hizo hazina umuhimu wala maana yoyote katika kuwekwa katika Misikiti au sehemu nyingine zozote. Kwani wakati wa Mtume (Swalla-Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Maswahaba zake (Radhiya-Allaahu 'anhum) alama
kama hizo zilikuwa hazipo.
Baada ya hapo huenda Waislamu wakaamua kuwa wawe na ishara kama vile Mayahudi
na Manaswara, kwani Mayahudi wana ile ishara ya nyota ya Daudi ambayo ina pembe sita na Manaswara wana ishara ya kuwa na msalaba. Kwa kuwa sisi huwa tarehe zetu za siku na miezi yetu hufuata mwezi, basi baadhi ya Waislam wakaona kuwa waweke hiyo alama ya mwezi kama nembo, lakini kiuhakika haina maana yoyote ya kisheria.
Na Allah Anajua zaidi.
 
Haimaanishi jambo lolote,wamejiwekea wenyewe tu kama mapambo kwenye baadhi ya misikiti
Think twice. Ni alama ya kishetani. Hata Katoliki wanazo sana. Dini ya kweli ni ile isiyokuwa na alama, maana Mungu wa Moses hakuwahi kuhimiza wachonge sanamu wala kitu chochote chenye mfano wa Mungu. Hizo alama zinamuwakilisha shetani na siyo Mungu.
 
Ha ha ha, kumekucha ,
Kuna baadhi ya pipo walisema ni mungu mwezi
Ila pia kuna jamaa mmoja ustadh aliwah kuniambia hio alama haipaswi kuwepo msikitini ila kwa kuwa sio upabde wangu alinipa maelezo mengi ila yote yamevapour
 
Ni alama ya mungu mwezi
Usiongee usiyoyajua. Hiyo alama ilikuwa adopted wakati wa Ottoman Empire na haihusiani chochote na uislam. Uislam ni kuabudu Mungu mmoja pekee aliyeumba mbingu na ardhi hana watoto, wajomba wala wajukuu, hajazaa wala kuzaliwa.

Imekuwa common place watu kuiga hii design mpaka sasa waliowengi (hata baadhi ya waislam wenyewe) wanadhani na sign ya uislam iliopo toka kipindi cha Mtume Muhammad (Rehma na Amani zimshukie juu yake) lakini hapana. Katafute kitabu chochote cha hadith (statement ya Mtume S.A.W) unitafutie hata invented hadith inayosema nyota na mwezi na alama ya uislam halafu niletee.

Ndio maana mpaka leo bendera ya uturuki ina the same symbol ya nyote na mwezi from the Ottomans, wengi wanadhani waturuki wamecopy from Islam but its actually vice versa and many scholars don't recommend hata iwepo maana kuna watu watafikiri kama unavyofikiri wewe

I hope umeelewa
 
Think twice. Ni alama ya kishetani. Hata Katoliki wanazo sana. Dini ya kweli ni ile isiyokuwa na alama, maana Mungu wa Moses hakuwahi kuhimiza wachonge sanamu wala kitu chochote chenye mfano wa Mungu. Hizo alama zinamuwakilisha shetani na siyo Mungu.
hehh!!
 
Kwahiyo alama hizo ni mapambo tu,??
 
Kumbe uislam umechakachuliwa namna hii. Sasa wale wanaoshupaa kila siku hapa kuwa uislam upo vile vile kama alivyouleta mtume ina maana hii story yako hawaijui au?

Na hii argument yako inamaanisha allah kashindwa kuulinda uislam wake usiongezewe alama za kituruki..hahahah
 
Think twice. Ni alama ya kishetani. Hata Katoliki wanazo sana. Dini ya kweli ni ile isiyokuwa na alama, maana Mungu wa Moses hakuwahi kuhimiza wachonge sanamu wala kitu chochote chenye mfano wa Mungu. Hizo alama zinamuwakilisha shetani na siyo Mungu.
Hizo alama first of all hazimo ndani ya msikiti ,pili baadhi tu wameweka nje ,pia hazipo kwenye sunna au Quran ,..point wanaotoa ni utambulisho kuwa sehem Fulani kuna msikiti mfano nikienda sao Paolo kwenye matembezi yng ya kuutafuta msikiti nikiona kiashirio hicho bas ntajua sehem fulan kuna msikiti ,

Tatu ni haraam kwenye nyumba yeyote kubandikwa picha au sanamu lolote mafundisho yanasema hvy kama unasema mafundishi ya mussa yanapinga masansmu basi uislamu&mussa wamefungana kimafundisho sabb according to Islam nyumba yenye sanamu au picha malaika haingii
 
Back
Top Bottom