Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 23,284
- 33,881
Kwa kipindi kirefu kitabu cha Abdul Sykes kilikuwa hakipatikani kwa kuwa nakala zilikuwa zimekwisha (out of print).
Hiki ni kitu cha kawaida kwa kitabu kukosekana.
Kitabu cha Abdu Sykes ni kitabu kilichozingirwa na ubishani mkubwa toka mara ya kwanza kilipochapwa kwa Kiingereza mwaka wa 1998.
Sababu kubwa ya msuguano huu ni kuwa kitabu hiki kilieleza mchango wa Waislamu katika kupigania uhuru wa Tanganyika.
Majibu yakaja nikashutumiwa kwa kile kilichoitwa udini na kuandika uongo na uchochezi na maneno mengi yakasemwa.
Hapa JF tukawa na mjadala uliochangiwa na watu karibu milioni moja na ukadumu kwa miezi sita bila kusimama hata siku moja mwandishi akikabiliana na watu wenye hamaki.
Hatimae mjadala ulifungwa na maisha yakaendelea.
Juma hili nikawatangazia jamaa hapa ukumbini kuwa kitabu cha Abdul Sykes kimeingia nchini na nikaeleza wapi kinapatikana.
Vita vikarejea upya haba jana nikishutumiwa kuwa kitabu hicho ni cha udini na kuwa kinauzwa misikitini.
Kila aliyenyanyua kalamu hicho ndicho kilichoelezwa.
Mimi niliwajibu kuwa kitabu hakiuzwi misikitini na nikaeleza maduka ambayo kitabu kinauzwa lakini hakuna aliyenisikia.
Nyimbo ikawa ni hiyo kitabu kinauzwa misikitini hili likisemwa kwa hamaki pamoja na maneno mengine yasiyopendeza.
Leo ssubuhi kwa bahati napita Maktaba nikakutana na picha ya kitabu cha Abdul Sykes picha niliyopiga kitabu kikiwa duka maarufu la vitabu Mtaa wa Samora - Mkuki na Nyota Bookshop.
Picha inazungumza maneno 1000.
Picha hiyo hapo chini ya kitabu cha Abdul Sykes kikiwa Mkuki na Nyota kinauzwa.
Naamini hili litamaliza mjadala na propaganda iliyokuwa ikienezwa dhidi yangu na kitabu changu:
"Baada ya Iddi Faiz Mafungo kwenda Tanga kupokea fedha kutoka kwa Mwalimu Kihere fedha za safari ya Julius Nyerere kwenda UNO zikawa zimekamilika.
Iddi Faiz yeye alikuwa Mweka Hazina wa Al Jamiatul Islammiya fi Tanganyika na pia Mweka Hazina wa TANU na ndiye aliyekuwa akikusanya michango ya safari ya Nyerere UNO.
Bwana Abdul akaniambia, "Abbas safari ya Nyerere UNO imewiva na atahitaji kudungwa sindano ya chanjo kwa ajili ya safari.
Mimi hawa Waingereza siwaamini hata kidogo kwa hiyo hakikisha kuwa hadungwi sindano lakini tupate cheti kuwa kapigwa sindano kwa ajili ya safari.
Hili jambo ni siri yetu sisi watu watatu mimi, wewe na Nyerere mtu yeyote asijue."
(Mazungumzo na Abbas Sykes miaka mingi kupita baada ya kitabu kuchapwa)