Tatizo lenu mnapata habari kutoka kwenye magazeti ya udaku! Anayeongoza kwa kulipwa pesa nyingi kwenye ringtones ni ROSE MUHANDO, wa pili ndio Diamond.
However, your opinion is not my reality. Kwa maisha ya kibongo hata Diamond angecheza uchi jukwaani, hawezi kuwa na more than a billion, hebu rejea uzi wangu, jamaa amekaririwa akisema ana "more than a billion", that means sio 1 billion net. Acheni kuja na analysis zenu uchwara kujaribu kutushawishi hapa...
Sasa nani kasema Diamond ndie anaongoza kwenye ring tones?! vp wangu? Ina maana kusema kapata zaidi ya 20m inamaanisha kwamba ndo anaongoza?! I know, kwa batch ya mwisho, Rose Mhando ndo katengeneza abt 26m wakati Diamond 22m...so, hoja yako ya kwanza hapa hapakuwa kwake! By the way, ikiwa mtu anaweza kutengeneza karibu 100m a year just for ringtones, unashangaa nini kusikia ana zaidi ya 1bn?!
Jambo la pili ni kutafuta ubishi usio na maana kukana kwamba kwa sasa Diamond ndie anaongoza hapa nchini kwa kupiga show nyingi!! Hutaki unaacha, lakini Diamond ndie msanii anayelipwa mkwanja mrefu zaidi kwenye show!! Leo jaribu kumpa mchongo wa show kama hujapigwa kalenda coz' hata time table yake ya show ipo occupied!! Piga ua, Diamond huwezi kumpa show kwa chini ya 5m, huo ndio ukweli wenyewe! Wengine ambao huwezi kuwapa show chini ya hiyo offer ni AY!
Kama nilivyosema, karibu kila wiki Diamond huwa anapiga show...na wakati mwingine ni more than one show a week! Hutaki, unaacha! Diamond kapiga show karibu katika kila nchi inayotuzunguka....kama hili nalo hutaki, endelea kubishana! Diamond anafanya matangazo, huko nako anavuta mpunga!!
Diamond amekuwapo kwenye game for almost three years now; na tangu aingie kwenye game, ameendelea kuwa top....hajashuka! Sizani kama kuna mwanamuziki mwingine ambae amekaa kwenye game akiwa top kwa muda mrefu namna hii!!! Hata kama hutaki, Bongo flavor inalipa....si kwa kuambiwa; myself nilishakuwa mdau sana kwenye hizi anga back then!! Unawafahamu wanaume Family(ile original). Wale jamaa kama wangekuwa na management ya ukweli...management iliyokuwa well organised na iliyoenda shule; wale jamaa hapa tunapooongea wangekuwa billionaires lakini ni wajanja ndo wamefaidika wakati walipokuwa top! Ingawaje Fella anaonekana ndo kafaidika zaidi, lakini Fella nae kapigwa sana na wajanja!!
By the way, kwangu unashangaza jinzi unavyotoka povu mara oh, tatizo lenu mnapata habari kutoka kwenye magazeti ya udaku; mara oh, analysis zenyewe uchwara....mara oh, hata akicheza uchi hawezi kupata more than a billion...come on men!! mbona jambo dogo sana hili wangu?! Yaani hata suala la mtu binafsi unalishupalia hivyo?!