Hii topic imeonesha lack
of financial exposure ya watu wengi sana hapa JF. Inashangaza kusoma
comment za watu hapa wakiona shilingi bilioni moja ya Tanzania kuwa ni
hela kuuuubwa sana.
Nimecheka mmoja amediriki kusema eti kuwa na bilioni moja hapa bongo
unakuwa mmoja wa tycoon!
Ndugu zangu bilioni moja ya kibongo sio hela ndefu kiivyo. Watu wengi tu
hapa Dar wana ukwasi wa kiwango hicho na wengine wanaendesha corolla
kama kawa.
Angalia bei za apartments/nyumba/viwanja na mashamba hapa Dar ndo utajua
kuwa shilingi yetu haina thamani na hiyo kufanya shilingi bilioni moja
kuwa pesa ya kawaida sana.
Vijumba vya national housing vyenyewe vinauzwa mpaka mil 200 tena kwenye
high density areas, Kweli mnaona sh. bilioni moja ni kubwa?
Sijaona hiyo interview ya Diamond so siwezi jua kama alisema ana cash
bank au utajiri wake kwa ujumla. Lakini hapana shaka his net worth is at
least over a bilioni shillings.
Alitoa project zake za nyumba sita anazijenga, baadhi kwenye prime areas
kama kinondoni, Pili kamaliza kumjengea mama yake nyumba ya sh mil 260
kimara n.k. So siwezi shangaa akisema utajiri wake ni bilioni au zaidi.
Source zake za mapato ni verifiable, show anazifanya (anasema analipwa
tsh 10 mil kwa show moja), ana sponsorship deals na Voda, Cocacola n.k,
mapato ya ring tones tumeambiwa kwa wasanii wa bongo flava yeye ndo
anaongoza kwa kuingiza mkwanja mrefu zaidi. Ruge alisema kaingiza zaidi
ya mil 27 kutoka push mobile na kampuni nyingine aliingiza mil 24 katika
miezi mitatu iliyoishia March mwaka huu.
Na amefanya show back to back for over three years, msisahau pia kuwa
Diamond ni msanii wa kwanza kufanya show ya peke yake kwa kiingilio cha
elfu 50 na ticket zote kuisha mpaka kuomba ziongezwe zingine.
So kwa madafu yetu haya, sishangai bwana mdogo kuwa na ukwasi huo. In
fact, ningeshangaa sana angesema mpaka sasa hajafikisha utajiri
huo.