Ukitoa mfano wa yeyote kati ya hao utaona life style yao na Diamond ni tofauti! Wasanii wengi kinachowaangusha na anasa... watu wanapenda kumtolea mfano Mr. Nice... life style ya Mr. Nice na Diamond ni tofauti! Wakati Mr. Nice alikuwa ni mtu wa Club, pombe na yeye, Diamond ni mtu wa nyumbani!
But all in all, why should you anticipate people's downfall? Ikiwa kuna wasanii kibao hata mbele ambao hufilisika, unataka kuniambia hakuna wasanii ambao hata baada ya kuacha muziki bado maisha yao yanakuwa mazuri? Kwanini hamtaki kuwatumia hao kama chachu au mifano ya kuwapa watu moyo na badala yake chachu yenu inakuwa ni wale waliofilisika na kuonesha ndo basi tena wengine wote watafilisika?
Haya, sie ni walamba viatu, tuambie wewe msema ukweli! Unatumia vigezo gani katika kutetea hu unaoita ukweli? Kwavile mtu kajenga nyumba ya millions of TSZ ndo atafilisika, au? Au kwavile washroom kuna gold plated accessories, au? Kwaavile alisema akaunti yake ina more than 1 billion, au? Hoja yenu hasa ni nini?? Manake ningewaona mnaongea hoja za maana endapo labda tungemuona baada ya kuonesha nyumba, anatuonesha migari ya bei mbaya, leo ana gari hili, kesho ana gari lile... tungeona hoja zenu zinaingia akilini, labda tungesikia analeta yacht na mambo mengine kama hayo! Hoja yenu hasa nyie wasema ukweli tofauti na sie walamba viatu ni ipi hasa?