hebronipyana
JF-Expert Member
- Oct 15, 2010
- 265
- 78
Mkuu Mkuruka,hii nd'o nilitaka niitumie kumjibu kitila mkumbo na pumba zake kwenye ya magazeti ya kila wiki.Tatizo walilonalo mashabiki wa akina Zitto ni kuwa huwezi kuachia demokrasia kwenye vyama kwenye nchi ambayo chama kilicho madarakani serikali yake ipo tayari kuwanunua wapinzani kwa kiasi kikubwa cha pesa ili kuwavuruga,utaratibu wa Chadema nimeupenda sana na nd'o maana nawasupport waweze kuingia madarakani kwasababu wameonyesha wanaweza.Tatizo moja dogo ninaloliona wapunguze makanjanja wa kichaga kwenye nafasi wasizozistahili hapo makao makuu.Rajab namheshimu sana kama great thinker wa kweli ila kwa hili sikubaliani naye kabisa, na haya ni maoni yangu kama alivyoyatoa yeye. Ninaamini katika demokrasia na ninafahamu nini maana ya demokrasia, lakini ninaona sio mara zote unaachia demokrasi kama kiongozi na kiongozi aliye bora ni lazima aangalie mazingira yakoje na kundi la watu wake likoje kabla ya kuachia demokrasia kutamalaki.
Tunasoma katika historia juu ya akina Stalin, akina Mao, akina Mousolin na tuliaminishwa kuwa walikuwa madikteta lakini mazingira ya wakati ule ya ushindani wa kisiasa na kiuchumi kati ya mataifa yalilazimu viongozi wawe hivyo kwani ilikuwa rahisi tu kuhujumiwa na taifa lingine kwa maslahi ya kiuchumi - hasa utafutaji wa rasilimali za dunia. Leo hi ukiziangalia China, Urusi zimeweza kujinasua katika ubabe wa MArekani kwa sababu ya kuhakikisha hawaachii demokrasia kiholela ambayo ingemuwezesha MArekani kupenyeza mamluki wake ambao wangetumika kuhujumu jitihada za Warusi na Wachina kusonga mbele kimaendeleo na hivyo kukwaza ushindani wa mataifa hayo kwa Marekani. NA sasa China imeanza kuachia demokrasia kidogo kidogo baada ya kuona mahali walipofikia kimaemdeleo MArekani haiwezi kuwa kitisho tena.
Kwa maana hiyo ninaona na uongozi wa CHADEMA unafuata mfano huo wa viongozi waanzilishi wa mataifa haya makubwa sasa. PAsipo kufanya hivyo kwa kipindi hiki cha mpito CCM mpinzani mkubwa wa CHADEMA ambayo haitapenda kuona Chadema ikisimama na kutoa upinzani wenye nguvu na kukipokonya madaraka ya kuongoza nchi. Chadema wakiachilia kiholela demokrasia wanaweza kujikuta wana mapandikizi wa CCM kama ilivyokuwa NCCR na hatimaye ikafa kama vinywa vya viongozi fulani wa CCM walivyokuwa wanajigamba kuwa Chadema ingekufa kabla ya 2014.
Tunaamini kuwa ili Chadema ikue na kufikia hatua ya kuiondoa madarkani CCM ni lazima kuachia demokrasia kidogo kidogo kwa kuwachunguza vilivyo wote wanaoutaka uongozi. Kwanini CCM ndio ipige kelele sana juu ya demokrasia ndani ya Chadema, wakati kwao hakuna demokrasia kama tulivyotegemea kwani tunaambiwa Uenyekiti ndani ya chama hiki hauogombaniwui na ye yote na hii ilimgharimu Shibuda wakati fulani - nadhani hapa Shibuda anaweza kutukumbusha yaliyomkuta alipoonyesha nia ya kugombea uenyekiti wa chama kitaifa.
Chadema mwendo ni huo huo watoto wa mjini wanasema ''mdogo mdogo''. Itakapofika wakati muafaka achieni demokrasia itamalki ndani ya Chama lakini kwa sasa ni lazima muwe makini sana.