Ahmed Rajab: Laana iliyoipiga CHADEMA

Ahmed Rajab: Laana iliyoipiga CHADEMA

Mimi si muumini sana wa hii demokrasia inayopigiwa debe na wajanja fulani akiwemo huyu mwandishi. Mafanikio ya demokrasia yeyote inategemia vitu vingi sana ikiwemo, katiba, mahakama, utamaduni, elimu, imani nk nk. Nchi za magharibi zinafakiwa vizuri sana kuliko nchi nyingine zikiwemo za Asia na mbaya zaidi Africa ambako demokrasia hakuna kabisa, kwa sababu wanazozijua wao ikiwemo kutokubali kutolewa madarakani kwa sababu ya madhambi yao au kutokuachia unono.
Kwa Chadema katika wakati huu ambao ni tete kama chama kutokana na kukabiliwa na upinzani na njama za wa wazi kutoka CCM, Serikali pamoja na dola yake yote, itakuwa kichekesho leo ukiniambia wawe na demokrasia ya kusimulia wakati serikali iliyopo haiimani kiasi cha kuelekeza nguvu zote kuufutilia mbali upinzani nchini.
Mimi sijui na siko ndani ya kundi la maamuzi la Chadema. Ila napenda kukuhakikishia wamekuwa ni wavumilivu sana tena sana kutokana na hujuma ambazo wamekuwa wakifanyiwa kiasi inahitaji mioyo ya misumari. Na hizi harakati za kupunguza kasi zimefanikiwa sana kwa sababu ni kweli Chadema wamekuwa derailled na huu ujinga wa akina Zitto na kundi lake. Ni uwazi usiopingika wao ni wasaliti. Na dawa ya usaliti ni kutoswa tu bila kuangalia usoni. Nimekuwa nikiwaaambia rafiki zangu. Huu ni wakati wa kuachana na Zitto na wenzake sasa. Kwa sababu upinzani hivi sasa ni kama Movement, WIMBI or kimbunga, halimjui Zitto or Mbowe. Watu wanataka mabadiliko. Leo hii Zitto nje ya Chadema is nothing ni chui wa karatasi. Watu wanakusanyika kusikia umbea. Akifukuzwa itasemwa ni msaliti wa movement. Kwisha.
Nakumbuka enzi ya Frelimo Nachingwea or Mazimbu kule Morogoro namna walisati walivyokuwa wanafanywa. Bila hivyo Chadema na upinzani utaendelea kuchezeshwa Mdundiko na wajanja. Mwandishi acha ngonjera please
 
Tuweni makini watu kwa sasa, maana hichi nikipindi cha waandishi kujenga Majumba na kununua Magali.
 
Kama ilivyokuwa ada, badala ya kujibu hoja mnaporomosha matusi.

Badala ya kujibu hoja za wakina Kitila mnaishia kufukuzana. Sijaona mahali ambapo wakina Kitila na baadae Zitto wamekisaliti chama chao. Nilichokiona ni kuwa wao kwa uchungu na mapenzi waliyonayo na chama chao wameelezea udhaifu wa uongozi uliopo.Huo uongozi, umetuthibitishia wengine mapungufu yao kwa kukimbilia kuwaadhibu badala ya kutafakari waliyoandika ili wajenge chama chao. Katika sakata lote hili waliojipunguzia heshima ni wakina Slaa, Lissu, Mnyika na sio wakina Zitto na Kitila. Kama Chadema mnayoitaka ndio hiyo ya akina Kim Il Sung basi heri hiki chama kilichopo. Yasije tukuta ya Kenya na Zambia.

Amandla.....
 
Una akili ya kushikiwa mpumba_u wewe na tatizo lako kubwa ni kutojitambua labda iko siku utatia akili kichwani na kuona kile ambacho kwa sasa umeamua kuwa kipofu na hivyo kutoona kasoro zozote.

yaani aliyebaki wewe kumpinga ni mama yako tu

kila anayesema ukweli haukosi kumpa jina, ukweli utasimama daima

haukulitegema hili eeeh

pole we
 
Huyu mzee ni mtu huru kimawazo kabisa,kila anayeleta ukweli mnasema lumumba,badilikeni hata kama mnaipenda chadema,mbona sie wengine hatuipendi ccm,na bado tunasema mbowe na dr slaa ni wa kuogopwa,hawafai kwa namna yeyote ile na sababu mara kibao tunazitoa,jengeni demokrasia tuikomboe nchi yetu,vinginevyo ccm itatoka lakin cdm kitakuwa kibaya kuliko ccm,ipo cku.

Kukosoana ni jambo la kawaida na jema kwa anaekosolewa pia. But anayeikosoa CDM kwa kufanya personal attack kwa viongozi wa juu binafsi naona kama ni mnafiki na asiyekitakia chama mema. Na ukiona mtu anaikosoa CDM kwa kutumia chorus zile zile zinazotumika na wapinzani wao CCM, ni wazi kwamba utahoji kama kweli ana nia njema au ni unafiki tu...
 
Kama ilivyokuwa ada, badala ya kujibu hoja mnaporomosha matusi.

Badala ya kujibu hoja za wakina Kitila mnaishia kufukuzana. Sijaona mahali ambapo wakina Kitila na baadae Zitto wamekisaliti chama chao. Nilichokiona ni kuwa wao kwa uchungu na mapenzi waliyonayo na chama chao wameelezea udhaifu wa uongozi uliopo.Huo uongozi, umetuthibitishia wengine mapungufu yao kwa kukimbilia kuwaadhibu badala ya kutafakari waliyoandika ili wajenge chama chao. Katika sakata lote hili waliojipunguzia heshima ni wakina Slaa, Lissu, Mnyika na sio wakina Zitto na Kitila. Kama Chadema mnayoitaka ndio hiyo ya akina Kim Il Sung basi heri hiki chama kilichopo. Yasije tukuta ya Kenya na Zambia.

Amandla.....

Kwa yeyote anayeamini kuwa Zitto
anapigania demokrasia ndani ya Chadema naomba aangalie matendo
yake. Demokrasia si kuunda makundi
ndani ya chama. Demokrasia si kupinga viongozi wenzako clandestinely. Demokrasia si kujiona wewe ni bora kuliko wengine ndani ya chama. Hizi zote ni sifa za Zitto. Na kwangu mimi hizi ni dalili za dikteta.
 
Dikteta hapingi mtu kwa kujificha. Hata hivyo, kwa hatua walizochukua hao viongozi inaonyesha wazi kuwa hawataki kupingwa clandestinely au otherwise. Zitto ni ambitious. Ana ego. Hakuna asiejua hilo lakini tangu lini hili limekuwa dhambi? Leo mnataka kumtosa kwa sababu anajisikia na sio kwa sababu hoja zake hazina msingi? Kwa sababu amekataa kuwa kondoo na kusimamia principles zake? Kweli kuna kazi.

Mimi ningewaheshimu hao viongozi kama wangesimama na kupangua hoja zote zilizokuwa kwenye waraka wa wakina Kitila. Wangetuambia kwa nini chama ambacho tulitegemea kingejitofautisha na ulafi wa baadhi wa viongozi wa sasa kinang'ang'ania trappings zile zile (mashangingi, posho za ajabu ajabu, mahelikopta n.k.). Wangetuonyesha kuwa sio profligate kama hao wanaotaka kuchukua nafasi yao.

Tofauti na unavyodai, chama chochote chenye demokrasia kina vikundi ndani yake. Hakuna chama cha kidemokrasia ambacho wanachama wake wanakubaliana sera zake kwa asilimia mia. Hakuna. Ikiwa hivyo basi ni cha kidikteta.

Kwa walichokifanya kwa hawa critics wao wa ndani basi hakuna matumaini. Hatuhitaji wakina Kim il Sung wengine.

Amandla......
 
Dikteta hapingi mtu kwa kujificha. Hata hivyo, kwa hatua walizochukua hao viongozi inaonyesha wazi kuwa hawataki kupingwa clandestinely au otherwise. Zitto ni ambitious. Ana ego. Hakuna asiejua hilo lakini tangu lini hili limekuwa dhambi? Leo mnataka kumtosa kwa sababu anajisikia na sio kwa sababu hoja zake hazina msingi? Kwa sababu amekataa kuwa kondoo na kusimamia principles zake? Kweli kuna kazi.

Mimi ningewaheshimu hao viongozi kama wangesimama na kupangua hoja zote zilizokuwa kwenye waraka wa wakina Kitila. Wangetuambia kwa nini chama ambacho tulitegemea ulafi wa baadhi wa viongozi wa sasa kinang'ang'ania trappings zote hizo (mashangingi, posho za ajabu ajabu, mahelikopta n.k.). Wangetuonyesha kuwa sio profligate kama hao wanaotaka kuchukua nafasi yao.

Kwa walichokifanya kwa hawa critics wao wa ndani basi hakuna matumaini. Hatuhitaji wakina Kim il Sung wengine.

Amandla......

Na mimi ningemheshimu Zitto kama angeleta hoja zake zijadiliwe kwenye vikao badala ya kuanzisha makundi ya upinzani ndani ya Chadema. Mwalimu aliwafukuzilia mbali akina Fortunatus Masha kwa sababu hizi hizi.
 
Mtoa mada,hii signature yao uliyoandika hapo chini ya kwamba "PADRE NI MWIKO KUOA AU KUTAMAN MWANAMKE,AU KUZINI NA MKE WA MTU AU NA MWANAMKE YEYOTE UMEMAANISHA NINI??UCHOCHEZ AU NIN HASA??HOJA YAKO IMESOMEKA LAKINI,MANTA'HOFFU..,JIBU SWALI LANGU PLEASE
 
Hihi cdm ina siku ya pili toka baba wa gombe aitabirie kufa kabla ya mwaka huu.
 
Na mimi ningemheshimu Zitto kama angeleta hoja zake zijadiliwe kwenye vikao badala ya kuanzisha makundi ya upinzani ndani ya Chadema. Mwalimu aliwafukuzilia mbali akina Fortunatus Masha kwa sababu hizi hizi.

Sasa kinawazuia nini kuzijadili wakati ziko wazi? Hivi nani aliweza kuleta hoja za kupingana na Mwalimu wazi wazi aka-survive? Hatuna historia ya demokrasia katika vyama vyetu na ndio maana watu wanaogopa kutoa hoja zao wazi wazi. Chadema wangeheshimika zaidi kama wangezichukua hoja za wakina Kitila na Zitto na kuzijadili wazi wazi bila kuwabeza walioziibua. Hii ingeonyesha kuwa palikuwa hakuna haja ya kujificha maana Chadema ni chama cha kidemokrasia na kila mwanachama ana haki sawa. Kilichotokea ni kuonyesha kuwa wanafuata principles za Animal Farm, wanyama wote wana haki sawa lakini wengine wana haki kuliko wengine. Chadema imekuwa kama TANU na CCM ya Mwalimu. Huko hatutaki kurudi.

Amandla.....
 
Mimi ningewashangaa sana viongozi wa Chadema kujadilia hoja za clandestine waraka wakati chama kina taratibu zake za kujadilia masuala. Hata Zitto na Kitila hawakutaka hoja zao zijadiliwe. Walitaka zifanyiwe kazi clandestinely kwa kuwanunua wafuasi mikoani. Huu ni mchezo wa CCM. Tusiupe nafasi ndani ya Chadema.
 
Kama ilivyokuwa ada, badala ya kujibu hoja mnaporomosha matusi.

Badala ya kujibu hoja za wakina Kitila mnaishia kufukuzana. Sijaona mahali ambapo wakina Kitila na baadae Zitto wamekisaliti chama chao. Nilichokiona ni kuwa wao kwa uchungu na mapenzi waliyonayo na chama chao wameelezea udhaifu wa uongozi uliopo.Huo uongozi, umetuthibitishia wengine mapungufu yao kwa kukimbilia kuwaadhibu badala ya kutafakari waliyoandika ili wajenge chama chao. Katika sakata lote hili waliojipunguzia heshima ni wakina Slaa, Lissu, Mnyika na sio wakina Zitto na Kitila. Kama Chadema mnayoitaka ndio hiyo ya akina Kim Il Sung basi heri hiki chama kilichopo. Yasije tukuta ya Kenya na Zambia.

Amandla.....
Muu tumewazoea hao ma-F4F wa CHADEMA.
HATA makala hii iliyoandikwa na A Rajab juu ya nepotism ndani ya CHADEMA watasema ni mpango wa Lumumba.
Akili yao inaishia kulaumu tu na si kuchukua nchi.
 
Mimi ningewashangaa sana viongozi wa Chadema kujadilia hoja za clandestine waraka wakati chama kina taratibu zake za kujadilia masuala. Hata Zitto na Kitila hawakutaka hoja zao zijadiliwe. Walitaka zifanyiwe kazi clandestinely kwa kuwanunua wafuasi mikoani. Huu ni mchezo wa CCM. Tusiupe nafasi ndani ya Chadema.

Hoja si hoja tu hata kama imetolewa kwa chini chini? Wangewanunua vipi wafuasi kwa hoja zilizojificha? Si lazima ingebidi zitoke wazi? Chama imara hakilazimishi hoja zote zilitolewe kwa kufuata taratibu kilichojiwekea maana mara nyingi hizi taratibu zina stiffle debate. Chama imara kinaruhusu wanachama wake kukijadili na kutofautiana nacho katika fora zozote ambazo wataona zinafaa. Kusisitiza taratibu si demokrasia bali ni mfumo wa hicho hicho chama mnachokibeza. Kama kweli mnajiamini kwa nini msizijadili hoja za wakina Kitila badala ya kununa na kubaki kuwatukana? Si yale yale ya " zidumu fikra sahihi za......?"

Amandla..........
 
Kwa yeyote anayeamini kuwa Zitto
anapigania demokrasia ndani ya Chadema naomba aangalie matendo
yake. Demokrasia si kuunda makundi
ndani ya chama. Demokrasia si kupinga viongozi wenzako clandestinely. Demokrasia si kujiona wewe ni bora kuliko wengine ndani ya chama. Hizi zote ni sifa za Zitto. Na kwangu mimi hizi ni dalili za dikteta.

ushaishiwa
 
Kama ilivyokuwa ada, badala ya kujibu hoja mnaporomosha matusi.

Badala ya kujibu hoja za wakina Kitila mnaishia kufukuzana. Sijaona mahali ambapo wakina Kitila na baadae Zitto wamekisaliti chama chao. Nilichokiona ni kuwa wao kwa uchungu na mapenzi waliyonayo na chama chao wameelezea udhaifu wa uongozi uliopo.Huo uongozi, umetuthibitishia wengine mapungufu yao kwa kukimbilia kuwaadhibu badala ya kutafakari waliyoandika ili wajenge chama chao. Katika sakata lote hili waliojipunguzia heshima ni wakina Slaa, Lissu, Mnyika na sio wakina Zitto na Kitila. Kama Chadema mnayoitaka ndio hiyo ya akina Kim Il Sung basi heri hiki chama kilichopo. Yasije tukuta ya Kenya na Zambia.

Amandla.....

Thanks sir
 
Na mimi ningemheshimu Zitto kama angeleta hoja zake zijadiliwe kwenye vikao badala ya kuanzisha makundi ya upinzani ndani ya Chadema. Mwalimu aliwafukuzilia mbali akina Fortunatus Masha kwa sababu hizi hizi.

hakuna kundi, mikakati ni kawaida kuwa na makundi....it happens naturally.

kama uwezo wako wa kufikiri na reference unaleta ya yule diktetta Nyerere aliyekuwa hana demokrasia

nakupa pole kubwa sana

so una copy na ku paste toka kwa Nyerere??

huna hoja, umeishiwa na wewe ni wa kugopwa kama ukoma

from now onwards, sikuchukuliaa kama senior bali kama senior mjinga kabisa kupata kuonekana ndani ya JF............

Reference ni Nyerere?? aliyekuwa anapigiwa kura za mtu na kivuli?? mpaka leo CCM HAMNA DEMOKRASIA yet kwa akili zako unataka chadema kiwe kama ccm...what a joke..

what does that makes you??

so dissapointed na mfano wa Nyerere, I would have slapped you
 
Rajab namheshimu sana kama great thinker wa kweli ila kwa hili sikubaliani naye kabisa, na haya ni maoni yangu kama alivyoyatoa yeye. Ninaamini katika demokrasia na ninafahamu nini maana ya demokrasia, lakini ninaona sio mara zote unaachia demokrasi kama kiongozi na kiongozi aliye bora ni lazima aangalie mazingira yakoje na kundi la watu wake likoje kabla ya kuachia demokrasia kutamalaki.
Tunasoma katika historia juu ya akina Stalin, akina Mao, akina Mousolin na tuliaminishwa kuwa walikuwa madikteta lakini mazingira ya wakati ule ya ushindani wa kisiasa na kiuchumi kati ya mataifa yalilazimu viongozi wawe hivyo kwani ilikuwa rahisi tu kuhujumiwa na taifa lingine kwa maslahi ya kiuchumi - hasa utafutaji wa rasilimali za dunia. Leo hi ukiziangalia China, Urusi zimeweza kujinasua katika ubabe wa MArekani kwa sababu ya kuhakikisha hawaachii demokrasia kiholela ambayo ingemuwezesha MArekani kupenyeza mamluki wake ambao wangetumika kuhujumu jitihada za Warusi na Wachina kusonga mbele kimaendeleo na hivyo kukwaza ushindani wa mataifa hayo kwa Marekani. NA sasa China imeanza kuachia demokrasia kidogo kidogo baada ya kuona mahali walipofikia kimaemdeleo MArekani haiwezi kuwa kitisho tena.
Kwa maana hiyo ninaona na uongozi wa CHADEMA unafuata mfano huo wa viongozi waanzilishi wa mataifa haya makubwa sasa. PAsipo kufanya hivyo kwa kipindi hiki cha mpito CCM mpinzani mkubwa wa CHADEMA ambayo haitapenda kuona Chadema ikisimama na kutoa upinzani wenye nguvu na kukipokonya madaraka ya kuongoza nchi. Chadema wakiachilia kiholela demokrasia wanaweza kujikuta wana mapandikizi wa CCM kama ilivyokuwa NCCR na hatimaye ikafa kama vinywa vya viongozi fulani wa CCM walivyokuwa wanajigamba kuwa Chadema ingekufa kabla ya 2014.
Tunaamini kuwa ili Chadema ikue na kufikia hatua ya kuiondoa madarkani CCM ni lazima kuachia demokrasia kidogo kidogo kwa kuwachunguza vilivyo wote wanaoutaka uongozi. Kwanini CCM ndio ipige kelele sana juu ya demokrasia ndani ya Chadema, wakati kwao hakuna demokrasia kama tulivyotegemea kwani tunaambiwa Uenyekiti ndani ya chama hiki hauogombaniwui na ye yote na hii ilimgharimu Shibuda wakati fulani - nadhani hapa Shibuda anaweza kutukumbusha yaliyomkuta alipoonyesha nia ya kugombea uenyekiti wa chama kitaifa.
Chadema mwendo ni huo huo watoto wa mjini wanasema ''mdogo mdogo''. Itakapofika wakati muafaka achieni demokrasia itamalki ndani ya Chama lakini kwa sasa ni lazima muwe makini sana.

umenena vema kabisa na huo ndio ukweli unaotakiwa kujulikana kwa watanzania wote demokrasia inaweza kuwa chanzo cha mamluki ni vyema kuwa makini na matumizi yake
 
Back
Top Bottom