Haya ndiyo maneno. Kukifadhili CHADEMA si lazima kuwa hawatataka kukifisadi hapo baadae. Kama ulivyosahihisha upotoshaji kuhusu Fuso basi mngefanya hivyo hivyo kuhusu tuhuma nyingine. Vizuri zaidi, msiishie hapo. Wanachama waambiawe gharama za kuendesha Chadema hapo awali zilikuwa ngapi na Mbowe na Ndesamburo walitoa ngapi.Waambiwe pia hiyo platform truck ilikuwa ya aina gani na ilinunuliwa wapi kwa gharama gani. Waambiwe makubaliano ya ulipaji yalikuwaje. Waelezwe kiasi ambacho CHADEMA wanapata kila mwaka na matumizi yake. Wapewe mahesabu ya mapato, madeni na matumizi yaliyokuwa audited. Wakifanya hivi watajiongezea credibility kama viable alternative kwa utawala uliokuwepo hivi sasa.
Amandla.......
Inapokuja kwa mapato na matumizi Hakuna chama kilicho transparent kama Chadema. Hakuna!