Ahmed Rajab: Laana iliyoipiga CHADEMA

assadsyria3

JF-Expert Member
Apr 9, 2013
6,881
2,000
rajab.jpg

Barazani kwa Ahmed Rajab | Ahmed Rajab | Toleo la 327 27 Nov 2013

Ni rahisi kubomoa ‘Ikulu’ kuliko kuimarisha kwako

KAMA wiki tatu hivi zilizopita rafiki yangu mmoja ambaye ni mwanasiasa wa Kenya ingawa yeye mwenyewe huenda akakataa kuitwa mwanasiasa, aliniuliza swali lililonishangaza. Aliniuliza: “Hivi huko kwenu hakuna chama chochote kingine cha siasa isipokuwa CCM?”

Swali hilo, kama nilivyosema, lilinishangaza kwa sababu nilikuwa na hakika kwamba muulizaji alijuwa jawabu la swali lake. Yeye si mtu asiyeijuwa Tanzania na siasa zake. Hivyo, nikaamua kumjibu kwa kumuuliza yeye swali: “Kwa nini waniuliza hivyo?”

“Kwa sababu,” alinijibu, “umeishika CCM. Umeiandama.”

Nikamwambia kwamba CCM ni chama kinachostahili kuandamwa kwa sababu ya vituko vyake. Baadaye nikamsomea baadhi ya madhambi ya chama chicho.

Si kwamba nataka kumfurahisha lakini leo naona itanilazimu walau kidogo kukitupia macho Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na viongozi wake wa juu. Si dhamira yangu leo kukitupia macho CHADEMA kwa kuzichambua shutuma za udugu na udini zinazokikabili chama hicho.

Nikiangalia kwa juu juu naona kwamba shutuma za udini hazina mashiko makubwa lakini zile za udugu zina nguvu na zimekuwa kama laana iliyokipiga chama hicho. Kinachojitokeza hapa katika CHADEMA ni ukosefu wa demokrasia halisi ndani ya chama. Udugu usingeweza kushamiri lau pangelikuwako na taratibu madhubuti za kidemokrasia.

Ninalazimika kukitupia macho chama hicho kwa sababu vituko vya hivi majuzi vya chama hicho vinanilazimisha kufanya hivyo.

Kwanza alijiuzulu nafasi yake ya Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA, Said Arfi, ambaye ni mbunge anayeliwakilisha Jimbo la Mpanda Mjini. Arfi alisema kuwa aliamua kujiuzulu nafasi hiyo kwa sababu alichoka kuchaguliwa viongozi na waasisi wa chama hicho.

Siku chache baadaye, Tundu Lissu, ambaye ni mwanasheria wa CHADEMA alitangaza kwamba chama kimewavua nyadhifa zao zote za kichama Zitto Kabwe, aliyekuwa naibu katibu mkuu wa CHADEMA, Dakta Kitila Mkumbo, aliyekuwa mjumbe wa kamati kuu ya CHADEMA na Samson Mwigamba, aliyekuwa mwenyekiti wa chama hicho kwa Mkoa wa Arusha.

Hatua zote hizo zinaashiria kwamba kumechafuka ndani ya CHADEMA na hali ya mambo huko si shwari asilan. Ni wazi kwamba chama hicho kinakabiliwa na matatizo makubwa, ambayo ikiwa busara haitotumiwa kuyatanzua, yanaweza yakakisababisha chama hicho kikadhoofika au hata kikapasuka, ingawa sidhani kwamba hili la pili linaweza likatokea katika kipindi cha hivi karibuni.

CHADEMA ni chama kizito katika siasa za Tanzania. Ni chama ambacho wafuasi wake wengi na hata wasio wafuasi wake wanaamini kwamba endapo kitajiandaa vyema kinaweza kikajinyakulia ushindi katika Uchaguzi Mkuu uliopangwa ufanywe Oktoba 2015.

Fursa yake ya kuupata ushindi huo itazidi kuwa nzuri endapo chama hicho kitashirikiana rasmi na vyama vingine vya upinzani nchini humo. Hilo ndilo tumaini la wenye kutamani kukiona Chama cha Mapinduzi (CCM) kinang’olewa madarakani 2015.

Kinachowasikitisha wapenzi wa CHADEMA ni kusikia shutuma za udugu na udini au kama zile zilizotolewa na Kabwe dhidi ya wakuu wa chama. Yeye hakuutaja udugu wala udini lakini aliyoyaelezea yanaonyesha kwamba wakuu wenzake wa CHADEMA hawaelewi nini hasa maana ya demokrasia na kama wanaielewa basi wanaikiuka misingi yake kwa makusudi.

Ikiwa shutuma zote hizo ni za kweli basi wakuu na wafuasi wa CHADEMA wana kazi kubwa. Na kazi yenyewe ni ya kuimarisha demokrasia ndani ya chama chao.

Uimairishwaji huo hauwezi kutokea kwa mkupuo mmoja. Unahitaji mchakato, mchakato wa kuimarisha demokrasia. Mchakato wa namna hiyo hauwezi kuwa mchakato ulio mwepesi au ulio nadhifu. Ni mchakato ulio mgumu na kama si mchafu basi una mazongezonge mengi.

Wala tusitarajie kuzuka miujiza katika mchakato wa aina hiyo wa kuiona demokrasia imeshamiri ghafla bin vu. Mchakato wa kuimarisha demokrasia ndani ya vyama, hasa vya upinzani, unahitaji uvumilivu wa hali ya juu hasa katika nchi kama za kwetu ambako mfumo wa demokrasia ya vyama vingi ni mchanga.

Aghalabu katika nchi kama zetu taasisi za kidemokrasia huwa dhaifu na zisizoweza kutekeleza mambo kama ipasavyo. Nadhani hiyo ndiyo moja ya sababu zinazozifanya serikali zetu ziwe na shida za kupata mafanikio ya kiuchumi au hata ya kijamii.

Lakini sio taasisi za kidemokrasia pekee zilizo na udhaifu huo katika nchi kama za kwetu. Hata vyama vya siasa navyo vimeambukizwa ugonjwa huo.

Ni rahisi kwa vyama vya upinzani, kwa mfano, kuyalenga makombora yao ya lawama kwa vyama vinavyotawala kuliko kujichunguza vyenyewe na kuangalia iwapo vina sifa za uwajibikaji au za kujenga demokrasia.

Vyama vya upinzani katika nchi zenye demokrasia changa mara kwa mara vimethibitisha kwamba ni rahisi kubomoa kwa mwenzako, hasa ikiwa kwake ni Ikulu, kushinda kujenga kwako.

Jambo ambalo mara nyingi tunalisahau ni kwamba demokrasia haihusiki tu na haki za kisiasa na za kiraia bali pia inahusika na taratibu au njia za kuzifikia haki hizo. Wa mwanzo wanaopaswa kulikumbuka hili ni viongozi wa vyama vya siasa, na hasa vile vya upinzani.

Iwapo kweli wanataka kujenga demokrasia wataposhika hatamu za utawala basi lazima tangu sasa wakiwa wapinzani waanze kujizoesha kutumia taratibu za kidemokrasia ili kufikia uamuzi wa ndani ya chama.

Na uamuzi huo ukishakatwa watumie njia au taratibu nyingine za kidemokrasia za kutekeleza uamuzi husika. Huko ndiko kujenga utamaduni wa kidemokrasia.

Demokrasia kwa hakika inaweza kuwa njia ambayo kwayo watawala (na hata viongozi wa vyama) huchaguliwa na uamuzi hukatwa katika mazingira ya ushindani wa kutaka kura za wananchi. Kuna mambo fulani, bila ya shaka, ambayo lazima yawepo kuhakikisha kwamba uchaguzi ni wa haki na umefanywa kwa uwazi.

Muhimu miongoni mwa hayo ni Tume ya Uchaguzi iliyo huru na isiyopendelea upande wowote. Kazi yake iwe ni kuhakikisha kwamba ushindani au mchuano wa kisiasa katika uchaguzi unafanyika kwa haki na bila ya wapigaji kura kusumbuliwa na yeyote yule.

Pamoja na ushindani wa kisiasa kuna suala la uwajibikaji. Huu ni msingi mwingine muhimu wa demokrasia. Mpaka sasa tumekuwa tukizungumzia mchakato na sio matokeo. Tusitaraji kuwa mfumo wa kidemokrasia utaleta manufaa kwa sababu tu mfumo huo ni wa kidemokrasia.

Ili uwe kweli wa kidemokrasia mfumo wa kidemokrasia unahitaji uwe na taratibu za uwajibikaji na nyenzo za kuwachunguza wakubwa. Hayo ni lazima yawepo ili kuwazuia hao wakubwa wasiyatumie vibaya madaraka yao.

Chama kilichozoea kuendesha shughuli zake kimabavu au kwa njia zisizo za uwazi au zisizo za kidemokrasia hakiwezi kuaminika kwamba kipatapo madaraka kitaweza kuendesha nchi kidemokrasia hata kama kinaweza kikaleta maendeleo.

- See more at: Raia Mwema - Laana iliyoipiga CHADEMA
 
lukatony

JF-Expert Member
Mar 25, 2011
650
1,000
Huyu mzee ni mtu huru kimawazo kabisa,kila anayeleta ukweli mnasema lumumba,badilikeni hata kama mnaipenda chadema,mbona sie wengine hatuipendi ccm,na bado tunasema mbowe na dr slaa ni wa kuogopwa,hawafai kwa namna yeyote ile na sababu mara kibao tunazitoa,jengeni demokrasia tuikomboe nchi yetu,vinginevyo ccm itatoka lakin cdm kitakuwa kibaya kuliko ccm,ipo cku.
 
samaki2011

JF-Expert Member
Dec 17, 2013
1,775
0
Mmeishiwa kila siku mnatunga utumbo tu, hivi mnapoteza muda wenu kuitetea ccm ambayo hadi leo mmeshakufa mko mochwari mmebaki kwenda kuzikwa!!!!!!!!

Hovyo kabisa leteni hoja za maana. Kwanza mtoa hoja ushalipa bili ya umeme au huna habari kwamba serikali ya chama chako imekupandishia billi?
 
lukatony

JF-Expert Member
Mar 25, 2011
650
1,000
Mmeishiwa kila siku mnatunga utumbo tu, hivi mnapoteza muda wenu kuitetea ccm ambayo hadi leo mmeshakufa mko mochwari mmebaki kwenda kuzikwa!!!!!!!!

Hovyo kabisa leteni hoja za maana. Kwanza mtoa hoja ushalipa bili ya umeme au huna habari kwamba serikali ya chama chako imekupandishia billi?Pendeni kusoma wapuuzi nyie,unamjua Ahmed Rajab,au unaropoka tu?mnaboa sana na hapo katoa mawazo huru na kwa sababu yanayofanywa na ccm yanaboa kwake vile vile,laiti angekuwa huru mngemwita majina yote ya buku 7
 
mwekundu

JF-Expert Member
Mar 4, 2013
21,859
2,000
Mwandishi msaliti,unatuonea gere kwa sababu una matazamo tofauti na sisi na una hoji mambo ambayo ni sawa na kulila tunda liliokatazwa!!
 
Adharusi

JF-Expert Member
Jan 22, 2012
14,224
2,000
Mmeishiwa kila siku mnatunga utumbo tu, hivi mnapoteza muda wenu kuitetea ccm ambayo hadi leo mmeshakufa mko mochwari mmebaki kwenda kuzikwa!!!!!!!!

Hovyo kabisa leteni hoja za maana. Kwanza mtoa hoja ushalipa bili ya umeme au huna habari kwamba serikali ya chama chako imekupandishia billi?

Vijana fuata mkumbo,sijui kama wamesoma makala yote,AR ajaitetea CCM,yeye kazungumza udhaifu wa CDM
 
Sakhalala

JF-Expert Member
May 2, 2011
572
500
Rajab namheshimu sana kama great thinker wa kweli ila kwa hili sikubaliani naye kabisa, na haya ni maoni yangu kama alivyoyatoa yeye. Ninaamini katika demokrasia na ninafahamu nini maana ya demokrasia, lakini ninaona sio mara zote unaachia demokrasi kama kiongozi na kiongozi aliye bora ni lazima aangalie mazingira yakoje na kundi la watu wake likoje kabla ya kuachia demokrasia kutamalaki.
Tunasoma katika historia juu ya akina Stalin, akina Mao, akina Mousolin na tuliaminishwa kuwa walikuwa madikteta lakini mazingira ya wakati ule ya ushindani wa kisiasa na kiuchumi kati ya mataifa yalilazimu viongozi wawe hivyo kwani ilikuwa rahisi tu kuhujumiwa na taifa lingine kwa maslahi ya kiuchumi - hasa utafutaji wa rasilimali za dunia. Leo hi ukiziangalia China, Urusi zimeweza kujinasua katika ubabe wa MArekani kwa sababu ya kuhakikisha hawaachii demokrasia kiholela ambayo ingemuwezesha MArekani kupenyeza mamluki wake ambao wangetumika kuhujumu jitihada za Warusi na Wachina kusonga mbele kimaendeleo na hivyo kukwaza ushindani wa mataifa hayo kwa Marekani. NA sasa China imeanza kuachia demokrasia kidogo kidogo baada ya kuona mahali walipofikia kimaemdeleo MArekani haiwezi kuwa kitisho tena.
Kwa maana hiyo ninaona na uongozi wa CHADEMA unafuata mfano huo wa viongozi waanzilishi wa mataifa haya makubwa sasa. PAsipo kufanya hivyo kwa kipindi hiki cha mpito CCM mpinzani mkubwa wa CHADEMA ambayo haitapenda kuona Chadema ikisimama na kutoa upinzani wenye nguvu na kukipokonya madaraka ya kuongoza nchi. Chadema wakiachilia kiholela demokrasia wanaweza kujikuta wana mapandikizi wa CCM kama ilivyokuwa NCCR na hatimaye ikafa kama vinywa vya viongozi fulani wa CCM walivyokuwa wanajigamba kuwa Chadema ingekufa kabla ya 2014.
Tunaamini kuwa ili Chadema ikue na kufikia hatua ya kuiondoa madarkani CCM ni lazima kuachia demokrasia kidogo kidogo kwa kuwachunguza vilivyo wote wanaoutaka uongozi. Kwanini CCM ndio ipige kelele sana juu ya demokrasia ndani ya Chadema, wakati kwao hakuna demokrasia kama tulivyotegemea kwani tunaambiwa Uenyekiti ndani ya chama hiki hauogombaniwui na ye yote na hii ilimgharimu Shibuda wakati fulani - nadhani hapa Shibuda anaweza kutukumbusha yaliyomkuta alipoonyesha nia ya kugombea uenyekiti wa chama kitaifa.
Chadema mwendo ni huo huo watoto wa mjini wanasema ''mdogo mdogo''. Itakapofika wakati muafaka achieni demokrasia itamalki ndani ya Chama lakini kwa sasa ni lazima muwe makini sana.
 
Adharusi

JF-Expert Member
Jan 22, 2012
14,224
2,000
Ni rahisi kwa vyama vya upinzani, kwa mfano, kuyalenga makombora yao ya lawama kwa vyama vinavyotawala kuliko kujichunguza vyenyewe na kuangalia iwapo vina sifa za uwajibikaji au za kujenga demokrasia.-Ahmed Rajabu
 
Kembaki

Member
Aug 25, 2010
63
95
Kama chadema ni chama cha ukanda basi ccm ni chama cha kidini soini tatizo sisi tutachukuliana nao hivyohivyo kama tuavyochukuliana na ccm

mbona hatuwwachi ccm kwasababu zaudini

Angalia Rais, makamu, katibu mkuu,kamanda mkuu, mkuu wa usalama wa nchi, makatibu wakuu,mawaziri, mikoani na wiayani (dini hiyo hiyo) kwani dini nyingne hazina watu
tafuteni ajenda nyingine na siyo ukanda
 
MBEBA MAONO KAJA

JF-Expert Member
Dec 24, 2013
367
250
KUWENI MAKINI NA PROPAGANDA ZA CCM KWA CHADEMA ETI NI CHA UKANDA, MNAKUMBUKA ILIVYO KIFANYA CUF NA MAJAMBIA? KAMA CHADEMA NI UKANDA BASI MSIGWA,WENJE, ZZK,PROF,NYERERE WOTE WAWILI, NA WABUNGE WOTE WASIO WACHAGA WANA DAMU YA KICHAGA? VP KUHUSU MAKAMBA WOTE? KAWAWA WOTE? MWINYI WOTE? SOKOINE BINTI? SIOI JE?KARUME? NAPE NNAUYE ? HAPO CCM HAKUNA UNDUGU NA UDINI? PROPAGANDA ZA KIZUSHI SANA.

NIMEWAKILISHA!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!:A S crown-1::usa2::llama:
 
MBEBA MAONO KAJA

JF-Expert Member
Dec 24, 2013
367
250
kama chadema ni chama cha ukanda basi ccm ni chama cha kidini soini tatizo sisi tutachukuliana nao hivyohivyo kama tuavyochukuliana na ccm

mbona hatuwwachi ccm kwasababu zaudini

angalia rais, makamu, katibu mkuu,kamanda mkuu, mkuu wa usalama wa nchi, makatibu wakuu,mawaziri, mikoani na wiayani (dini hiyo hiyo) kwani dini nyingne hazina watu
tafuteni ajenda nyingine na siyo ukanda
watanzania wenzangu hayo mauozo ya magamba hamuyaoni isipokuwa kudanganywa ukanda chadema, mapanga cuf, tuamke tujitambue
 
BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,997
2,000
Njemba imeshakula ubwabwa wa MACCM basi ikaamua kuandika pumba zake, nasikia iko safarini kuwahi ubwabwa mwingine Zenj kusherehekea miaka 50 ya mapinduzi ikishapata ubwabwa za Zenj itaandika article nyingine kuhusu CHADEMA na Zenj. Mtu mzima hovyoooooooo!!!! Mxyuuuuuuuuuuuuuu
 
Umslopagazi

JF-Expert Member
May 16, 2013
1,463
2,000
Hiyo siyo kweli kusini tupo vizuri, kanda ya ziwa pia hizo propaganda hazina mashiko tena. Salama ya CCM ni kutekeleza ilani yao na ahadi walizotoa ili kurudisha imani ya wananchi kwao. Huwezi kusafirisha meno ya tembo na kuendesha operesheni TOKOMEZA watu siyo wajinga tena.

Kusini gani mmejiimarisha wewe?
 
kivava

JF-Expert Member
Apr 2, 2013
5,777
2,000
[QUOTE=lukatony;82544 unamjua Ahmed Rajab,au unaropoka tu? Je chama chake cha CUF siyo cha kidini/kikanda? Uamsho yake j
 
jogi

JF-Expert Member
Sep 25, 2010
25,586
2,000
Huyu mzee ni mtu huru kimawazo kabisa,kila anayeleta ukweli mnasema lumumba,badilikeni hata kama mnaipenda chadema,mbona sie wengine hatuipendi ccm,na bado tunasema mbowe na dr slaa ni wa kuogopwa,hawafai kwa namna yeyote ile na sababu mara kibao tunazitoa,jengeni demokrasia tuikomboe nchi yetu,vinginevyo ccm itatoka lakin cdm kitakuwa kibaya kuliko ccm,ipo cku.

Nchi haikombolewi kwa kugombania kujenga demokrasia ndani ya chama. wenzio wamakudanganya kuwa wewe ni msomi. POLE MWAKWETU.
 
simbilisi

JF-Expert Member
Dec 26, 2012
792
0
Njemba imeshakula ubwabwa wa MACCM basi ikaamua kuandika pumba zake, nasikia iko safarini kuwahi ubwabwa mwingine Zenj kusherehekea miaka 50 ya mapinduzi ikishapata ubwabwa za Zenj itaandika article nyingine kuhusu CHADEMA na Zenj. Mtu mzima hovyoooooooo!!!! Mxyuuuuuuuuuuuuuu

yaani aliyebaki wewe kumpinga ni mama yako tu

kila anayesema ukweli haukosi kumpa jina, ukweli utasimama daima

haukulitegema hili eeeh

pole we
 
simbilisi

JF-Expert Member
Dec 26, 2012
792
0
Nchi haikombolewi kwa kugombania kujenga demokrasia ndani ya chama. wenzio wamakudanganya kuwa wewe ni msomi. POLE MWAKWETU.

unajua ulichoandika?? una miaka mingapi?? nisije nikachambua hilo kumbe umeiba laptop ya baba
 
EMINEMU

Member
Dec 2, 2013
76
95
Rajab namheshimu sana kama great thinker wa kweli ila kwa hili sikubaliani naye kabisa, na haya ni maoni yangu kama alivyoyatoa yeye. Ninaamini katika demokrasia na ninafahamu nini maana ya demokrasia, lakini ninaona sio mara zote unaachia demokrasi kama kiongozi na kiongozi aliye bora ni lazima aangalie mazingira yakoje na kundi la watu wake likoje kabla ya kuachia demokrasia kutamalaki.
Tunasoma katika historia juu ya akina Stalin, akina Mao, akina Mousolin na tuliaminishwa kuwa walikuwa madikteta lakini mazingira ya wakati ule ya ushindani wa kisiasa na kiuchumi kati ya mataifa yalilazimu viongozi wawe hivyo kwani ilikuwa rahisi tu kuhujumiwa na taifa lingine kwa maslahi ya kiuchumi - hasa utafutaji wa rasilimali za dunia. Leo hi ukiziangalia China, Urusi zimeweza kujinasua katika ubabe wa MArekani kwa sababu ya kuhakikisha hawaachii demokrasia kiholela ambayo ingemuwezesha MArekani kupenyeza mamluki wake ambao wangetumika kuhujumu jitihada za Warusi na Wachina kusonga mbele kimaendeleo na hivyo kukwaza ushindani wa mataifa hayo kwa Marekani. NA sasa China imeanza kuachia demokrasia kidogo kidogo baada ya kuona mahali walipofikia kimaemdeleo MArekani haiwezi kuwa kitisho tena.
Kwa maana hiyo ninaona na uongozi wa CHADEMA unafuata mfano huo wa viongozi waanzilishi wa mataifa haya makubwa sasa. PAsipo kufanya hivyo kwa kipindi hiki cha mpito CCM mpinzani mkubwa wa CHADEMA ambayo haitapenda kuona Chadema ikisimama na kutoa upinzani wenye nguvu na kukipokonya madaraka ya kuongoza nchi. Chadema wakiachilia kiholela demokrasia wanaweza kujikuta wana mapandikizi wa CCM kama ilivyokuwa NCCR na hatimaye ikafa kama vinywa vya viongozi fulani wa CCM walivyokuwa wanajigamba kuwa Chadema ingekufa kabla ya 2014.
Tunaamini kuwa ili Chadema ikue na kufikia hatua ya kuiondoa madarkani CCM ni lazima kuachia demokrasia kidogo kidogo kwa kuwachunguza vilivyo wote wanaoutaka uongozi. Kwanini CCM ndio ipige kelele sana juu ya demokrasia ndani ya Chadema, wakati kwao hakuna demokrasia kama tulivyotegemea kwani tunaambiwa Uenyekiti ndani ya chama hiki hauogombaniwui na ye yote na hii ilimgharimu Shibuda wakati fulani - nadhani hapa Shibuda anaweza kutukumbusha yaliyomkuta alipoonyesha nia ya kugombea uenyekiti wa chama kitaifa.
Chadema mwendo ni huo huo watoto wa mjini wanasema ''mdogo mdogo''. Itakapofika wakati muafaka achieni demokrasia itamalki ndani ya Chama lakini kwa sasa ni lazima muwe makini sana.

mkuu nimeipenda sana hii japo mimi ni ccm
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom