Ahmed Rajab: Laana iliyoipiga CHADEMA

Mimi ningewashangaa sana viongozi wa Chadema kujadilia hoja za clandestine waraka wakati chama kina taratibu zake za kujadilia masuala. Hata Zitto na Kitila hawakutaka hoja zao zijadiliwe. Walitaka zifanyiwe kazi clandestinely kwa kuwanunua wafuasi mikoani. Huu ni mchezo wa CCM. Tusiupe nafasi ndani ya Chadema.

utaratibu ukoje?? ebu weka vifungu vya katiba vinavyoruhusu hivyo

chama gani kuanzia chacha wangwe kuna tuhuma za ubadhirifu, upendeleo na kutokuwa active kwenye higher politics kwa lengo la kuiondoa ccm?? ule waraka umeusoma?? umechukua kitu gani??

wewe Jasusi, kuna siku umehoji ubadhirifu wa mbowe?? nipe any post plz

kama hujafanya hivyo jua wewe ni mnafiki, na kinachokusumbua juu ya zitto ni wivu na chuk binafsi.

hivi unatofauti gani na mwana CCM anayempenda kikwete sana?? au anayempenda Nape na Mwigulu regardless their scandals and weakness?? ebu nipe tofauti>>>>

walewale

hili swala la zitto limewanajisisha wengi sana
 
Hoja si hoja tu hata kama imetolewa kwa chini chini? Wangewanunua vipi wafuasi kwa hoja zilizojificha? Si lazima ingebidi zitoke wazi? Chama imara hakilazimishi hoja zote zilitolewe kwa kufuata taratibu kilichojiwekea maana mara nyingi hizi taratibu zina stiffle debate. Chama imara kinaruhusu wanachama wake kukijadili na kutofautiana nacho katika fora zozote ambazo wataona zinafaa. Kusisitiza taratibu si demokrasia bali ni mfumo wa hicho hicho chama mnachokibeza. Kama kweli mnajiamini kwa nini msizijadili hoja za wakina Kitila badala ya kununa na kubaki kuwatukana? Si yale yale ya " zidumu fikra sahihi za......?"

Amandla..........

I wonder kama kuna siku atatokea 'Obama' na 'Hilary Clinton' wa chadema so different thinkings and views in one part, yet they are one........ and won
 
Sasa CDM baya lipi hapo? Mtu anaye kukosoa anakupenda Mara dufu kuliko mtu anayekusifia ambae anakuchukia Mara dufu nae!

Any way CDM ni chama kinachopendwa kusifiwa kila kukicha! Hakina kasoro ni CCM tu wenye kasoro.
 
Ahamed Rajabu amesimama kwa msukumo wa kiroho katika andishi lake,

Msukumo huo ndio turufu waitumiao wale anaojaribu kuwatetea,

Siasa za Ahamed Rajabu ni za kimimi hata kule viungani alikosimamia,

Ahamed ni mwanagistoria na sio mchambuzi wa siasa, na namtaka afahamu kuwa, uchambuzi wa siasa za mlengo wa kati hukinzana na historia tenge,

Namshauri mzee wangu abaki kuwa mwanahistoria na muamini wa Hizbu tu
 
hakuna kundi, mikakati ni kawaida kuwa na makundi....it happens naturally.

kama uwezo wako wa kufikiri na reference unaleta ya yule diktetta Nyerere aliyekuwa hana demokrasia

nakupa pole kubwa sana

so una copy na ku paste toka kwa Nyerere??

huna hoja, umeishiwa na wewe ni wa kugopwa kama ukoma

from now onwards, sikuchukuliaa kama senior bali kama senior mjinga kabisa kupata kuonekana ndani ya JF............

Reference ni Nyerere?? aliyekuwa anapigiwa kura za mtu na kivuli?? mpaka leo CCM HAMNA DEMOKRASIA yet kwa akili zako unataka chadema kiwe kama ccm...what a joke..

what does that makes you??

so dissapointed na mfano wa Nyerere, I would have slapped you

Matusi na vitisho vya nini?

Amandla....
 
Ahamed Rajabu amesimama kwa msukumo wa kiroho katika andishi lake,

Msukumo huo ndio turufu waitumiao wale anaojaribu kuwatetea,

Siasa za Ahamed Rajabu ni za kimimi hata kule viungani alikosimamia,

Ahamed ni mwanagistoria na sio mchambuzi wa siasa, na namtaka afahamu kuwa, uchambuzi wa siasa za mlengo wa kati hukinzana na historia tenge,

Namshauri mzee wangu abaki kuwa mwanahistoria na muamini wa Hizbu tu

Mnarudi pale pale. Unakimbilia kumchafua Ahmed badala ya kujadili hoja zake!
Kweli iko kazi.

Amandla....
 
Una akili ya kushikiwa mpumba_u wewe na tatizo lako kubwa ni kutojitambua labda iko siku utatia akili kichwani na kuona kile ambacho kwa sasa umeamua kuwa kipofu na hivyo kutoona kasoro zozote.

Haaa haaa

BAK mimi najitambua,

sijawa mtumwa wa kupenda tu bila sababu

Mbowe is too local, ni kweli,

ebu sema, operation tokomeza, tanesco n.k Mbowe kafanya nini?? why you guys dont see even a sunrise and sunset??

Mbowe hawezi uongozi, ila njaa zenu na hela yake inamfanya awe na wafuasi wengi.

narudia UKWELI UTASIMAMA DAIMA

where are thinkers in CDM?? I see only zitto hata kama mtamfukuza
 
Mimi kwa kweli simfwasi wa chama chochote cha siasa na haitatokea kuwa mwanachama wa chama cha siasa bali mimi nimfwasi wa siasa zetu naukiwa mfwasi basi utakuwa mfwasi wa siasa za chama fulani na mimi nimfwasi wachama cha cdm nilipenda cdm nikiwa kutkana na sera zake za democrasia lakni naona democrasia imekuwa democrasi kwani shutuma zote zinazo tolewa kwa kina kabwe na wenzake kwa kweli sijaziona ubaya wake kwni waraka wakina kitila ulikuwa wa democrasia sijaona sehemu kunakotaja neno mapinduzi sasa kwenye chama labda kama kuna mengine ambao sisi wafwasi hatuyajuwi naomba muyatowe tuweze kuyajadili nakuona ubaya wao ningependa kama viongozi wangeujadili waraka huo nakuuchambuwa wakatuwaminisha kuwa ulikuwa uhaini ndani ya chama lakni naona tu matusi na kashfa ndizo tunazowaminishwa kuw zzt ni muhaini sijajuwa uhaini waina gani wa democrasia au wamapinduzi
 
Huyu mzee ni mtu huru kimawazo kabisa,kila anayeleta ukweli mnasema lumumba,badilikeni hata kama mnaipenda chadema,mbona sie wengine hatuipendi ccm,na bado tunasema mbowe na dr slaa ni wa kuogopwa,hawafai kwa namna yeyote ile na sababu mara kibao tunazitoa,jengeni demokrasia tuikomboe nchi yetu,vinginevyo ccm itatoka lakin cdm kitakuwa kibaya kuliko ccm,ipo cku.

Daa kwel Mh.Mbowe Na Dr.SLAA ni watu wa kuogopwa kwa ustawi wa ccm na serikal yake dhalimu, hasa ukifikiria harakati zao za kutetea wananch wa tanzania..
 
Kusema flani ni mdini huwa kwa mtu mwenye mapenzi na taifa lake ni kitu chauma sana ila ukweli huwezi kufichika chadema kina ubaguzi wa kidini kupita maelezo.
 
Mwandishi huyu nimemfahamu kupitia makala kadhaa alizoandika hasa zile za John Okello na uhusika wake kwenye mapinduzi matukufu ya Zanzibar ambayo mwandishi huyu aliifanyia upotoshaji mkubwa!

Na baada ya kupitia kwenye mada hii nimegundua kuwa mwandishi huyu anaendeleza upotoshaji ule ule ambao amekuwa akiufanya.
Anasema CDM ni cha chama chenye udugu na si chenye udini kwa sababu anajua fika watu tutachambua muundo wa serikali ya CCM na secretarieti yake jinsi udini ulivyotamalaki!Kwa hiyo hapo kwenye udini hawezi gusa,anaujua Moto wake!

Na kwenye issue ya udugu,nani asiyejua CCM ni chama cha BMW(Baba Mama na Watoto).Nani asiyejua kuwa chama hiki ni zao la familia zile za akina Mkapa,Mwinyi,Kikwete,Sita,Lowassa,Nchimbi,Kawawa,na kadha wa kadhaa?Ina maana miaka 50 ya kuongoza nchi bado hakuna hata watu wengine wanaoweza kuongoza CCM zaidi ya familia zilezile?
Au ndio deffencive mechanism yenu ya kuutetea udugu CCM?

Na je umewahi kupeleleza makabila ya wajumbe wa Kamati kuu ya CDM?Je kuna hata harufu ya udugu au ukabila pale?Kama hujaiangalia kaiangalie!

Na pia eti unaongelea demokrasia!Demokrasia ipi iliyo kwenye Chama chako,wakati kila siku mwenyekiti anapita bila kupingwa kwa hofu ya kunyang'anywa tonge mdomoni?Sasa kama nyie chama tawala wenye uzoefu wa miaka 50 madarakani mmefanya hivyo sie je mnaotutumia mpaka mapandikizi ili Chama kife tufanyeje?

Mie bado ninasema,ukisikia kelele nyingi za wanaCCM ujue 'umewashika pabaya'!Kwa hiyo naiomba kamati kuu iendeleze mwendo uleule wa kung'oa VIRUS wote wanaotishia uhai wa chama!Gharama ya kukijenga chama baada ya hawa mapandikizi kukidhoofisha itakuwa kubwa zaidi kuliko gharama ya kuwafukuza!
 
Mmeishiwa kila siku mnatunga utumbo tu, hivi mnapoteza muda wenu kuitetea ccm ambayo hadi leo mmeshakufa mko mochwari mmebaki kwenda kuzikwa!!!!!!!!

Hovyo kabisa leteni hoja za maana. Kwanza mtoa hoja ushalipa bili ya umeme au huna habari kwamba serikali ya chama chako imekupandishia billi?

pumba tu, mkiambiwa kweli mnaona watu wapuuzi. Huvi unamjua Ahmed Rajab? Hiyo gharama kubwa ya umeme itatuumiza mm na ww tu. Mtu akiikosoa cdm, kwenu mnamuona ccm tu. Sio siri cdm ndio tumaini letu sisi wapenda mageuzi, ila lazima waangalie pale wanapojikwaa!!
 
Rajab namheshimu sana kama great thinker wa kweli ila kwa hili sikubaliani naye kabisa, na haya ni maoni yangu kama alivyoyatoa yeye. Ninaamini katika demokrasia na ninafahamu nini maana ya demokrasia, lakini ninaona sio mara zote unaachia demokrasi kama kiongozi na kiongozi aliye bora ni lazima aangalie mazingira yakoje na kundi la watu wake likoje kabla ya kuachia demokrasia kutamalaki.
Tunasoma katika historia juu ya akina Stalin, akina Mao, akina Mousolin na tuliaminishwa kuwa walikuwa madikteta lakini mazingira ya wakati ule ya ushindani wa kisiasa na kiuchumi kati ya mataifa yalilazimu viongozi wawe hivyo kwani ilikuwa rahisi tu kuhujumiwa na taifa lingine kwa maslahi ya kiuchumi - hasa utafutaji wa rasilimali za dunia. Leo hi ukiziangalia China, Urusi zimeweza kujinasua katika ubabe wa MArekani kwa sababu ya kuhakikisha hawaachii demokrasia kiholela ambayo ingemuwezesha MArekani kupenyeza mamluki wake ambao wangetumika kuhujumu jitihada za Warusi na Wachina kusonga mbele kimaendeleo na hivyo kukwaza ushindani wa mataifa hayo kwa Marekani. NA sasa China imeanza kuachia demokrasia kidogo kidogo baada ya kuona mahali walipofikia kimaemdeleo MArekani haiwezi kuwa kitisho tena.
Kwa maana hiyo ninaona na uongozi wa CHADEMA unafuata mfano huo wa viongozi waanzilishi wa mataifa haya makubwa sasa. PAsipo kufanya hivyo kwa kipindi hiki cha mpito CCM mpinzani mkubwa wa CHADEMA ambayo haitapenda kuona Chadema ikisimama na kutoa upinzani wenye nguvu na kukipokonya madaraka ya kuongoza nchi. Chadema wakiachilia kiholela demokrasia wanaweza kujikuta wana mapandikizi wa CCM kama ilivyokuwa NCCR na hatimaye ikafa kama vinywa vya viongozi fulani wa CCM walivyokuwa wanajigamba kuwa Chadema ingekufa kabla ya 2014.
Tunaamini kuwa ili Chadema ikue na kufikia hatua ya kuiondoa madarkani CCM ni lazima kuachia demokrasia kidogo kidogo kwa kuwachunguza vilivyo wote wanaoutaka uongozi. Kwanini CCM ndio ipige kelele sana juu ya demokrasia ndani ya Chadema, wakati kwao hakuna demokrasia kama tulivyotegemea kwani tunaambiwa Uenyekiti ndani ya chama hiki hauogombaniwui na ye yote na hii ilimgharimu Shibuda wakati fulani - nadhani hapa Shibuda anaweza kutukumbusha yaliyomkuta alipoonyesha nia ya kugombea uenyekiti wa chama kitaifa.
Chadema mwendo ni huo huo watoto wa mjini wanasema ''mdogo mdogo''. Itakapofika wakati muafaka achieni demokrasia itamalki ndani ya Chama lakini kwa sasa ni lazima muwe makini sana.

Wewe ni great thinker. Hoja zako nimezikubali, achana na hawa mandondocha wa maccm ambao lengo lao ni kuhakikisha Chadema haiwi na viongozi wenye msimamo wa dhati. Wanajifanya wanaijua demokrasia saana! watueleze ni lini mwenyekiti wa ccm alishindanishwa ndani ya chama chao. Poor maccm!
 
rajab.jpg

Barazani kwa Ahmed Rajab | Ahmed Rajab | Toleo la 327 27 Nov 2013

Ni rahisi kubomoa ‘Ikulu’ kuliko kuimarisha kwako

KAMA wiki tatu hivi zilizopita rafiki yangu mmoja ambaye ni mwanasiasa wa Kenya ingawa yeye mwenyewe huenda akakataa kuitwa mwanasiasa, aliniuliza swali lililonishangaza. Aliniuliza: “Hivi huko kwenu hakuna chama chochote kingine cha siasa isipokuwa CCM?”

Swali hilo, kama nilivyosema, lilinishangaza kwa sababu nilikuwa na hakika kwamba muulizaji alijuwa jawabu la swali lake. Yeye si mtu asiyeijuwa Tanzania na siasa zake. Hivyo, nikaamua kumjibu kwa kumuuliza yeye swali: “Kwa nini waniuliza hivyo?”

“Kwa sababu,” alinijibu, “umeishika CCM. Umeiandama.”

Nikamwambia kwamba CCM ni chama kinachostahili kuandamwa kwa sababu ya vituko vyake. Baadaye nikamsomea baadhi ya madhambi ya chama chicho.

Si kwamba nataka kumfurahisha lakini leo naona itanilazimu walau kidogo kukitupia macho Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na viongozi wake wa juu. Si dhamira yangu leo kukitupia macho CHADEMA kwa kuzichambua shutuma za udugu na udini zinazokikabili chama hicho.

Nikiangalia kwa juu juu naona kwamba shutuma za udini hazina mashiko makubwa lakini zile za udugu zina nguvu na zimekuwa kama laana iliyokipiga chama hicho. Kinachojitokeza hapa katika CHADEMA ni ukosefu wa demokrasia halisi ndani ya chama. Udugu usingeweza kushamiri lau pangelikuwako na taratibu madhubuti za kidemokrasia.

Ninalazimika kukitupia macho chama hicho kwa sababu vituko vya hivi majuzi vya chama hicho vinanilazimisha kufanya hivyo.

Kwanza alijiuzulu nafasi yake ya Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA, Said Arfi, ambaye ni mbunge anayeliwakilisha Jimbo la Mpanda Mjini. Arfi alisema kuwa aliamua kujiuzulu nafasi hiyo kwa sababu alichoka kuchaguliwa viongozi na waasisi wa chama hicho.

Siku chache baadaye, Tundu Lissu, ambaye ni mwanasheria wa CHADEMA alitangaza kwamba chama kimewavua nyadhifa zao zote za kichama Zitto Kabwe, aliyekuwa naibu katibu mkuu wa CHADEMA, Dakta Kitila Mkumbo, aliyekuwa mjumbe wa kamati kuu ya CHADEMA na Samson Mwigamba, aliyekuwa mwenyekiti wa chama hicho kwa Mkoa wa Arusha.

Hatua zote hizo zinaashiria kwamba kumechafuka ndani ya CHADEMA na hali ya mambo huko si shwari asilan. Ni wazi kwamba chama hicho kinakabiliwa na matatizo makubwa, ambayo ikiwa busara haitotumiwa kuyatanzua, yanaweza yakakisababisha chama hicho kikadhoofika au hata kikapasuka, ingawa sidhani kwamba hili la pili linaweza likatokea katika kipindi cha hivi karibuni.

CHADEMA ni chama kizito katika siasa za Tanzania. Ni chama ambacho wafuasi wake wengi na hata wasio wafuasi wake wanaamini kwamba endapo kitajiandaa vyema kinaweza kikajinyakulia ushindi katika Uchaguzi Mkuu uliopangwa ufanywe Oktoba 2015.

Fursa yake ya kuupata ushindi huo itazidi kuwa nzuri endapo chama hicho kitashirikiana rasmi na vyama vingine vya upinzani nchini humo. Hilo ndilo tumaini la wenye kutamani kukiona Chama cha Mapinduzi (CCM) kinang’olewa madarakani 2015.

Kinachowasikitisha wapenzi wa CHADEMA ni kusikia shutuma za udugu na udini au kama zile zilizotolewa na Kabwe dhidi ya wakuu wa chama. Yeye hakuutaja udugu wala udini lakini aliyoyaelezea yanaonyesha kwamba wakuu wenzake wa CHADEMA hawaelewi nini hasa maana ya demokrasia na kama wanaielewa basi wanaikiuka misingi yake kwa makusudi.

Ikiwa shutuma zote hizo ni za kweli basi wakuu na wafuasi wa CHADEMA wana kazi kubwa. Na kazi yenyewe ni ya kuimarisha demokrasia ndani ya chama chao.

Uimairishwaji huo hauwezi kutokea kwa mkupuo mmoja. Unahitaji mchakato, mchakato wa kuimarisha demokrasia. Mchakato wa namna hiyo hauwezi kuwa mchakato ulio mwepesi au ulio nadhifu. Ni mchakato ulio mgumu na kama si mchafu basi una mazongezonge mengi.

Wala tusitarajie kuzuka miujiza katika mchakato wa aina hiyo wa kuiona demokrasia imeshamiri ghafla bin vu. Mchakato wa kuimarisha demokrasia ndani ya vyama, hasa vya upinzani, unahitaji uvumilivu wa hali ya juu hasa katika nchi kama za kwetu ambako mfumo wa demokrasia ya vyama vingi ni mchanga.

Aghalabu katika nchi kama zetu taasisi za kidemokrasia huwa dhaifu na zisizoweza kutekeleza mambo kama ipasavyo. Nadhani hiyo ndiyo moja ya sababu zinazozifanya serikali zetu ziwe na shida za kupata mafanikio ya kiuchumi au hata ya kijamii.

Lakini sio taasisi za kidemokrasia pekee zilizo na udhaifu huo katika nchi kama za kwetu. Hata vyama vya siasa navyo vimeambukizwa ugonjwa huo.

Ni rahisi kwa vyama vya upinzani, kwa mfano, kuyalenga makombora yao ya lawama kwa vyama vinavyotawala kuliko kujichunguza vyenyewe na kuangalia iwapo vina sifa za uwajibikaji au za kujenga demokrasia.

Vyama vya upinzani katika nchi zenye demokrasia changa mara kwa mara vimethibitisha kwamba ni rahisi kubomoa kwa mwenzako, hasa ikiwa kwake ni Ikulu, kushinda kujenga kwako.

Jambo ambalo mara nyingi tunalisahau ni kwamba demokrasia haihusiki tu na haki za kisiasa na za kiraia bali pia inahusika na taratibu au njia za kuzifikia haki hizo. Wa mwanzo wanaopaswa kulikumbuka hili ni viongozi wa vyama vya siasa, na hasa vile vya upinzani.

Iwapo kweli wanataka kujenga demokrasia wataposhika hatamu za utawala basi lazima tangu sasa wakiwa wapinzani waanze kujizoesha kutumia taratibu za kidemokrasia ili kufikia uamuzi wa ndani ya chama.

Na uamuzi huo ukishakatwa watumie njia au taratibu nyingine za kidemokrasia za kutekeleza uamuzi husika. Huko ndiko kujenga utamaduni wa kidemokrasia.

Demokrasia kwa hakika inaweza kuwa njia ambayo kwayo watawala (na hata viongozi wa vyama) huchaguliwa na uamuzi hukatwa katika mazingira ya ushindani wa kutaka kura za wananchi. Kuna mambo fulani, bila ya shaka, ambayo lazima yawepo kuhakikisha kwamba uchaguzi ni wa haki na umefanywa kwa uwazi.

Muhimu miongoni mwa hayo ni Tume ya Uchaguzi iliyo huru na isiyopendelea upande wowote. Kazi yake iwe ni kuhakikisha kwamba ushindani au mchuano wa kisiasa katika uchaguzi unafanyika kwa haki na bila ya wapigaji kura kusumbuliwa na yeyote yule.

Pamoja na ushindani wa kisiasa kuna suala la uwajibikaji. Huu ni msingi mwingine muhimu wa demokrasia. Mpaka sasa tumekuwa tukizungumzia mchakato na sio matokeo. Tusitaraji kuwa mfumo wa kidemokrasia utaleta manufaa kwa sababu tu mfumo huo ni wa kidemokrasia.

Ili uwe kweli wa kidemokrasia mfumo wa kidemokrasia unahitaji uwe na taratibu za uwajibikaji na nyenzo za kuwachunguza wakubwa. Hayo ni lazima yawepo ili kuwazuia hao wakubwa wasiyatumie vibaya madaraka yao.

Chama kilichozoea kuendesha shughuli zake kimabavu au kwa njia zisizo za uwazi au zisizo za kidemokrasia hakiwezi kuaminika kwamba kipatapo madaraka kitaweza kuendesha nchi kidemokrasia hata kama kinaweza kikaleta maendeleo.

- See more at: Raia Mwema - Laana iliyoipiga CHADEMA

Naona wengi wamajadili na wengine wana jichanganya lakini hoja ya mwandishi bw. Ahmed Rajab inakosa jibu moja na la msingi kabisa, nikwamba, Kuna demokrasia ambayo inakiuka misingi ya katiba, na kama inakiuka ni utaratibu gani unatumika ili kuweza kuingia kwenye katiba?

Na kingine ni kwamba endapo mtu atakiuka misingi ya katiba aachwe tu na asichukuliwe hatua?

Kuna swala la kuingiliwa na muasisi na udugu, kama mwanasiasa na mchambuzi wa siasa aliebobea atakuwa mjinga endapo atakosa kufahamu kuwa kuna baraza la ushauri la wazee na mawazo ya watangulizi wake katika kujenga afya ya chama maana hii ni njia mojawapo ya ushirikishwaji na ni demokrasia kwani mawazo yanapoletwa hujadiriwa kwa pamoja

Kuhusu swala la udugu sijui kama mwasisi ana udugu na makamu mzee Arfi mpaka akamshawishi agombee ubunge, na kingine mwenyekiti sijui alikua na udugu gani na naibu katibu pamoja na wanafunzi wenzake wa vyuo mpaka akamfata aje ajiunge na CDM?

Kwa swala la uvumilivu mwandishi jaribu kufatilia siasa za vyama, na kwa huyu ambae amevuliwa nyadhifa zake ujiulize kwanini mwaka 2008 alitaka kuachana na siasa na chama kilichukua hatua gani na baada ya hapo nyendo zake zilikuaje?

Hitimisho ndg Ahmed Rajab nakushauri jaribu kusafisha barazani kwako kwa kuondoa majani ya miti yaliyo dondoka ili kujenga hoja zenye afya
 
rajab.jpg

Barazani kwa Ahmed Rajab | Ahmed Rajab | Toleo la 327 27 Nov 2013

Ni rahisi kubomoa ‘Ikulu’ kuliko kuimarisha kwako

KAMA wiki tatu hivi zilizopita rafiki yangu mmoja ambaye ni mwanasiasa wa Kenya ingawa yeye mwenyewe huenda akakataa kuitwa mwanasiasa, aliniuliza swali lililonishangaza. Aliniuliza: “Hivi huko kwenu hakuna chama chochote kingine cha siasa isipokuwa CCM?”

Swali hilo, kama nilivyosema, lilinishangaza kwa sababu nilikuwa na hakika kwamba muulizaji alijuwa jawabu la swali lake. Yeye si mtu asiyeijuwa Tanzania na siasa zake. Hivyo, nikaamua kumjibu kwa kumuuliza yeye swali: “Kwa nini waniuliza hivyo?”

“Kwa sababu,” alinijibu, “umeishika CCM. Umeiandama.”

Nikamwambia kwamba CCM ni chama kinachostahili kuandamwa kwa sababu ya vituko vyake. Baadaye nikamsomea baadhi ya madhambi ya chama chicho.

Si kwamba nataka kumfurahisha lakini leo naona itanilazimu walau kidogo kukitupia macho Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na viongozi wake wa juu. Si dhamira yangu leo kukitupia macho CHADEMA kwa kuzichambua shutuma za udugu na udini zinazokikabili chama hicho.

Nikiangalia kwa juu juu naona kwamba shutuma za udini hazina mashiko makubwa lakini zile za udugu zina nguvu na zimekuwa kama laana iliyokipiga chama hicho. Kinachojitokeza hapa katika CHADEMA ni ukosefu wa demokrasia halisi ndani ya chama. Udugu usingeweza kushamiri lau pangelikuwako na taratibu madhubuti za kidemokrasia.

Ninalazimika kukitupia macho chama hicho kwa sababu vituko vya hivi majuzi vya chama hicho vinanilazimisha kufanya hivyo.

Kwanza alijiuzulu nafasi yake ya Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA, Said Arfi, ambaye ni mbunge anayeliwakilisha Jimbo la Mpanda Mjini. Arfi alisema kuwa aliamua kujiuzulu nafasi hiyo kwa sababu alichoka kuchaguliwa viongozi na waasisi wa chama hicho.

Siku chache baadaye, Tundu Lissu, ambaye ni mwanasheria wa CHADEMA alitangaza kwamba chama kimewavua nyadhifa zao zote za kichama Zitto Kabwe, aliyekuwa naibu katibu mkuu wa CHADEMA, Dakta Kitila Mkumbo, aliyekuwa mjumbe wa kamati kuu ya CHADEMA na Samson Mwigamba, aliyekuwa mwenyekiti wa chama hicho kwa Mkoa wa Arusha.

Hatua zote hizo zinaashiria kwamba kumechafuka ndani ya CHADEMA na hali ya mambo huko si shwari asilan. Ni wazi kwamba chama hicho kinakabiliwa na matatizo makubwa, ambayo ikiwa busara haitotumiwa kuyatanzua, yanaweza yakakisababisha chama hicho kikadhoofika au hata kikapasuka, ingawa sidhani kwamba hili la pili linaweza likatokea katika kipindi cha hivi karibuni.

CHADEMA ni chama kizito katika siasa za Tanzania. Ni chama ambacho wafuasi wake wengi na hata wasio wafuasi wake wanaamini kwamba endapo kitajiandaa vyema kinaweza kikajinyakulia ushindi katika Uchaguzi Mkuu uliopangwa ufanywe Oktoba 2015.

Fursa yake ya kuupata ushindi huo itazidi kuwa nzuri endapo chama hicho kitashirikiana rasmi na vyama vingine vya upinzani nchini humo. Hilo ndilo tumaini la wenye kutamani kukiona Chama cha Mapinduzi (CCM) kinang’olewa madarakani 2015.

Kinachowasikitisha wapenzi wa CHADEMA ni kusikia shutuma za udugu na udini au kama zile zilizotolewa na Kabwe dhidi ya wakuu wa chama. Yeye hakuutaja udugu wala udini lakini aliyoyaelezea yanaonyesha kwamba wakuu wenzake wa CHADEMA hawaelewi nini hasa maana ya demokrasia na kama wanaielewa basi wanaikiuka misingi yake kwa makusudi.

Ikiwa shutuma zote hizo ni za kweli basi wakuu na wafuasi wa CHADEMA wana kazi kubwa. Na kazi yenyewe ni ya kuimarisha demokrasia ndani ya chama chao.

Uimairishwaji huo hauwezi kutokea kwa mkupuo mmoja. Unahitaji mchakato, mchakato wa kuimarisha demokrasia. Mchakato wa namna hiyo hauwezi kuwa mchakato ulio mwepesi au ulio nadhifu. Ni mchakato ulio mgumu na kama si mchafu basi una mazongezonge mengi.

Wala tusitarajie kuzuka miujiza katika mchakato wa aina hiyo wa kuiona demokrasia imeshamiri ghafla bin vu. Mchakato wa kuimarisha demokrasia ndani ya vyama, hasa vya upinzani, unahitaji uvumilivu wa hali ya juu hasa katika nchi kama za kwetu ambako mfumo wa demokrasia ya vyama vingi ni mchanga.

Aghalabu katika nchi kama zetu taasisi za kidemokrasia huwa dhaifu na zisizoweza kutekeleza mambo kama ipasavyo. Nadhani hiyo ndiyo moja ya sababu zinazozifanya serikali zetu ziwe na shida za kupata mafanikio ya kiuchumi au hata ya kijamii.

Lakini sio taasisi za kidemokrasia pekee zilizo na udhaifu huo katika nchi kama za kwetu. Hata vyama vya siasa navyo vimeambukizwa ugonjwa huo.

Ni rahisi kwa vyama vya upinzani, kwa mfano, kuyalenga makombora yao ya lawama kwa vyama vinavyotawala kuliko kujichunguza vyenyewe na kuangalia iwapo vina sifa za uwajibikaji au za kujenga demokrasia.

Vyama vya upinzani katika nchi zenye demokrasia changa mara kwa mara vimethibitisha kwamba ni rahisi kubomoa kwa mwenzako, hasa ikiwa kwake ni Ikulu, kushinda kujenga kwako.

Jambo ambalo mara nyingi tunalisahau ni kwamba demokrasia haihusiki tu na haki za kisiasa na za kiraia bali pia inahusika na taratibu au njia za kuzifikia haki hizo. Wa mwanzo wanaopaswa kulikumbuka hili ni viongozi wa vyama vya siasa, na hasa vile vya upinzani.

Iwapo kweli wanataka kujenga demokrasia wataposhika hatamu za utawala basi lazima tangu sasa wakiwa wapinzani waanze kujizoesha kutumia taratibu za kidemokrasia ili kufikia uamuzi wa ndani ya chama.

Na uamuzi huo ukishakatwa watumie njia au taratibu nyingine za kidemokrasia za kutekeleza uamuzi husika. Huko ndiko kujenga utamaduni wa kidemokrasia.

Demokrasia kwa hakika inaweza kuwa njia ambayo kwayo watawala (na hata viongozi wa vyama) huchaguliwa na uamuzi hukatwa katika mazingira ya ushindani wa kutaka kura za wananchi. Kuna mambo fulani, bila ya shaka, ambayo lazima yawepo kuhakikisha kwamba uchaguzi ni wa haki na umefanywa kwa uwazi.

Muhimu miongoni mwa hayo ni Tume ya Uchaguzi iliyo huru na isiyopendelea upande wowote. Kazi yake iwe ni kuhakikisha kwamba ushindani au mchuano wa kisiasa katika uchaguzi unafanyika kwa haki na bila ya wapigaji kura kusumbuliwa na yeyote yule.

Pamoja na ushindani wa kisiasa kuna suala la uwajibikaji. Huu ni msingi mwingine muhimu wa demokrasia. Mpaka sasa tumekuwa tukizungumzia mchakato na sio matokeo. Tusitaraji kuwa mfumo wa kidemokrasia utaleta manufaa kwa sababu tu mfumo huo ni wa kidemokrasia.

Ili uwe kweli wa kidemokrasia mfumo wa kidemokrasia unahitaji uwe na taratibu za uwajibikaji na nyenzo za kuwachunguza wakubwa. Hayo ni lazima yawepo ili kuwazuia hao wakubwa wasiyatumie vibaya madaraka yao.

Chama kilichozoea kuendesha shughuli zake kimabavu au kwa njia zisizo za uwazi au zisizo za kidemokrasia hakiwezi kuaminika kwamba kipatapo madaraka kitaweza kuendesha nchi kidemokrasia hata kama kinaweza kikaleta maendeleo.

- See more at: Raia Mwema - Laana iliyoipiga CHADEMA

Unajishushia heshima mwenyewe jitayarishe kwa changamoto, uroho wako wa fedha ushaanza kupewa buku 7
 
Mwandishi huyu nimemfahamu kupitia makala kadhaa alizoandika hasa zile za John Okello na uhusika wake kwenye mapinduzi matukufu ya Zanzibar ambayo mwandishi huyu aliifanyia upotoshaji mkubwa!

Na baada ya kupitia kwenye mada hii nimegundua kuwa mwandishi huyu anaendeleza upotoshaji ule ule ambao amekuwa akiufanya.
Anasema CDM ni cha chama chenye udugu na si chenye udini kwa sababu anajua fika watu tutachambua muundo wa serikali ya CCM na secretarieti yake jinsi udini ulivyotamalaki!Kwa hiyo hapo kwenye udini hawezi gusa,anaujua Moto wake!

Na kwenye issue ya udugu,nani asiyejua CCM ni chama cha BMW(Baba Mama na Watoto).Nani asiyejua kuwa chama hiki ni zao la familia zile za akina Mkapa,Mwinyi,Kikwete,Sita,Lowassa,Nchimbi,Kawawa,na kadha wa kadhaa?Ina maana miaka 50 ya kuongoza nchi bado hakuna hata watu wengine wanaoweza kuongoza CCM zaidi ya familia zilezile?
Au ndio deffencive mechanism yenu ya kuutetea udugu CCM?

Na je umewahi kupeleleza makabila ya wajumbe wa Kamati kuu ya CDM?Je kuna hata harufu ya udugu au ukabila pale?Kama hujaiangalia kaiangalie!

Na pia eti unaongelea demokrasia!Demokrasia ipi iliyo kwenye Chama chako,wakati kila siku mwenyekiti anapita bila kupingwa kwa hofu ya kunyang'anywa tonge mdomoni?Sasa kama nyie chama tawala wenye uzoefu wa miaka 50 madarakani mmefanya hivyo sie je mnaotutumia mpaka mapandikizi ili Chama kife tufanyeje?

Mie bado ninasema,ukisikia kelele nyingi za wanaCCM ujue 'umewashika pabaya'!Kwa hiyo naiomba kamati kuu iendeleze mwendo uleule wa kung'oa VIRUS wote wanaotishia uhai wa chama!Gharama ya kukijenga chama baada ya hawa mapandikizi kukidhoofisha itakuwa kubwa zaidi kuliko gharama ya kuwafukuza!

Hivi ni wapi Ahmed amesema CDM ni chama chenye undugu na si chenye udini? Hebu highlight hiyo sehemu ili tuwe ukurasa mmoja.

Pamoja na hayo, utapingaje hoja ya nepotism ya Chadema kwa kuonyesha nepotism ya CCM? Kwani ni siri kuwa baadhi ya viongozi wa Chadema wana undugu wa kuzaliwa au kuoana? Kuwapo kwa watu wenye undugu si lazima iwe imetokana na nepotism. Mnachotakiwa kufanya ni kuthibitisha kuwa wote hawa wamepata vyeo kutokana na sifa zao na sio mahusiano yao na viongozi wa juu. Mnavyozidi kukwepa kufanya hivyo ndivyo mnavyoipa uzito hoja ya nepotism.

Kuwepo kwa makabila tofauti kwenye chama vile vile si ushahidi tosha ya kutokuwepo ukabili. Kama ilivyo kwenye suala la nepotism, kama wote hao wa kabila moja wamepanda kutokana na sifa zao na si upendelewa basi hoja ya ukabila haitakuwa na mshiko. Mnashindwa nini kuthibitisha hili?

Amandla......
 
Ahmed Rajabu amesema ukweli CDM Ilianza kuonekana kuwa mbadala wa CCM, lakini kwa laana hii ya udini na ukabila au ueneo na kukosekana Demokrasia ndani ya CDM, CCM itaendelea kutawala tu hata kama siipendi CCM hii ya kisasa ya Kikwete nitasema ukweli daima fitina kwangu mwiko, labda kitokee chama kingine kitakachokuwa kimegundua viongozi wa CDM wamekosea wapi
 
Back
Top Bottom