A failed assassination plot against Dr. Ulimboka...

A failed assassination plot against Dr. Ulimboka...

Wanajamvi

Nimesikia kuwa J Kikwete anategemea kwenda kumuona Dr Ulimboka Mchana huu

Stay tuned

Asikanyage kabisa huko,ni kitu gani kinampeleka huko?
Kama kumuua wameshindwa waendelee na mipango yao mingine Ulimboka haitaji kuonwa na wao,
Mficheni kabisa wasimuone.
 
hata mimi nakubaliana na wanaosema kwamba kuna watu walioathirika na msimamo wa Dr. Ulimboka ndiyo wameendesha zoezi hilo la kinyama kwa sababu tu ya namna zoezi hilo linavyosimuliwa.
hivi jamani kama serikali ingetaka kumuua kwa kutumia inteligency system waliyonayo hawangeweza kuja na mbinu za old stone age. eti askali wamkamate Leaders club na kumpeleka mpaka mabwepande na kumpiga wakimwacha hoi. hao ni thugs tu/majambazi wanaojifunza au vibaka hawa wakawaida.
kama ni system wangemuua kimya kimya na tungeambiwa ni stroke tu au ajali nk
 
Ningekuwa ndugu wa Ulimboka ningekataa kata kata huyo rais mnafiki kumuona ndugu yangu.
 
Really? Narudia tena; sio lazima JK amalize miaka mitano ya mwisho 2015.
 
Awali ya yote yatupasa kumpa pole na kumuombea apone haraka dakatari wetu huyu bwana Ulimboka na walaaniwe kwa nguvu zote wale wote waliohusika kwa namna moja ama nyingine.

Wengi wetu kwa asilimia kubwa tumekuwa na imani kuwa, utekelezaji wa jambo hilo ni njama au mkakati wa serikali kupunguza kasi ya harakati za madaktari katika kudai haki zao.

Tunapoihusisha moja kwa moja serikali kwa upande mmoja wa mbele, hebu tugeuke nyuma na kuangalia upande wa pili.

Bila shaka Dk Ulimboka alikuwa na maadui wa hatari wenye chuki binafsi naye hasa kipindi cha vugu vugu hili la migomo ya madaktari. Kuna watu waliopoteza madaraka yao matamu kutokana na kadhia hii, upo uwezekano wa kupanga njama za kulipiza kisasi.

Kutumika polisi si kitu mbele ya pesa. Ukiwa na fungu la kutosha ukitaka kuwatumia polisi njaa kwa ajili ya uhalifu unawatumia bila shida. Ikiwa wapo ambao hufanya ujambazi na kupora mali za watu, itakuwa hawa wa kukodiwa! Tugawanye fikra na mitazamo yetu, wakati tunaitupia jicho la mashaka serikali.

Tuangalie na upande wa pili, wale waliomwaga unga kutokana na harakati hizi tunawachukuliaje? Hapa mhalifu halisi anaweza kujificha chini ya kivuli cha serikali.

Mwisho napenda niwapongeza madaktari wote waliotoa kichapo kwa mtu anayedhaniwa kuwa alikuwa mmoja wa wateka nyara.

Mungu msaidie Dk Ulimboka apone haraka ili aendelee na harakati zake.

Kama unakiri polisi wametumika then hakuna namna ya kuiondoa serikali kwan polisi sio chombo huru kama LHRC
 
Lakini kwani kwa mgomo huu wa pili wanapoteza nini kama tayari walishapoteza madaraka yao.
kwa mtizamo wangu naona walioko madarakani ndio waliotenda wakiogopa kupoteza madaraka.

Eh mungu mrudishie afya yake huyu kijana..
Na laana iwaendee wale wote waliohusika kupanga na kutenda hicho kitendo!
 
Wanajamvi

Nimesikia kuwa J Kikwete anategemea kwenda kumuona Dr Ulimboka Mchana huu

Stay tuned
Kuna nini nyuma ya pazia? Mbona hajawahi kwenda kuwaona wagonjwa wanaotaabika bila matibabu kwa sababu ya mgomo wa madakitari, toka hii migomo iaanze?.
 
wanagoma na mwisho wa mwezi wanaenda na ATM kudraw Bank fedha zetu walipa kodi huku wagonjwa wetu wanakufa hospitali. hii ni halali? kwanini waendelee kulipwa mwezi huu? kwanini serikali haigomi kuwalipa kwa kususa kwao? hawatendi haki hata kidogo.
Hata wewe unatumia kodi zetu kuleta ***** kwenye maswala ya msingi. Kama wewe ulikimbilia kusoma HKL acha wenzio waliosoma wadai haki zao na zako. Na wao pia ni walipa kodi
 
Hasiruhusiwe kumwona ,haende kutatua matatizo ya watoto yapo mengi huko vijijini hawana madawati.hakachangishe pesa ili kujenga zahanati.Hasijifanye mwema hapa.please please hasiingie ndani.Yeye ni rais sawa ,lakini hii nchi ni ya wananchi.Alikuwepo Mkapa yupo wapi???????.HASIINGIE MOI NA HATUTAKI APEKEKWE INDIA PIA.MADAKTARI BINGWA WAPO HAPO KAMA DAWA TUWASILIANA TUNALETA.LAZIMA TUWAADABISHE HAO MAGAMBA SASA HIVI.
 
Hawakutaka kumuua Ulimboka ila walitaka kumkolimba Ulimboka huo ndiyo masamiati unaostahili kutumika
 
Nitafurahi sana kama akipopolewa mawe hapo Muhimbili

Sasa wewe unania mabay sana unataka kuliingiza taifa katika ghalama zingine kubwa za kukodi mandege ya kubeba WAPAMBE WA kwenda kumuuguza ughaibuni na kuendelea kuwatwisha wa TZ mzigo.
 
Mnafiki tu Kikwete., Mi nitatafsiri kama Anaenda kumkejeli. CUZ HE KNOWS EXACTLY WHAT HAPPENS.
 
Mgomo ni mojawapo ya mwisho kabisa kudai haki. Kama wametumia njia za awali zikashindikana, wana haki kugoma. Aidha, kugoma hakumnyimi mtumishi haki ya mshahara, hata akisimamishwa kazi, ataendelea kupokea hadi pale atakapokutwa na hatia ya kumwondolea utumishi.
mh! ati?
 
Sisi wengine tuliotoka family za madaktari tunajua unafiki wa hawa viumbe madaktari.
Nimecheza tiari bado kwenye korido za OPD ,MCH,nimeishi miaka miaka yote ya utoto hadi ujana wangu mita chache tu toka hospitali kwenye kotas.
Nafahamu vyema jinsi madaktari wanavyoiba madawa,na vitu kama dripwater,bandeji etc na kwenda kuviuZA kwenye hosptali za binafsi.jinsi wanavyokula rushwa ili kuhudumia wagonjwa,HAWANIDANGANYI CHOCHOTE.
Wanapogoma hivi sasa na kuacha watu masikini wasio na uwezo wa kwenda private wafe HAIKUBALIKI.
Huyu Ulimboka(MY ALMIGTHY GOD REST HIM IN HELL) hapaswi kuonewa huruma KAMWE.
 
Back
Top Bottom