30 - 36 years old: An Official Thread

Nilipokua

Nilipokua kwenye huo umri,mipango ikavurugika,nikarudi home,wa kwanza kunionesha dharau ni bi mkubwa,akawafundisha na watoto wa wadogo zangu pale home kunidharau,hakutosheka..akawa ananijengea dharau kwa watu mitaani,usiombe huo msongo wa mawazo,nikaanza kubeti nipate hela niondoke,mungu siyo benard Morrison network yangu ikalipa,kwa Sasa Nina kipato kuliko kunguni yoyote kwenye ukoo,na huwa sijui Cha kumfanya no mkubwa..Ila bado Nina grudge nae
ila ukweli mchungu mzazi huwapenda watoto wake wote kwa usawa wakiwa wadogo wakishakuwa watu wazima, wanapendwa kulingana na kipato na msaada wanaotoa.hasa hawa wakina mama zetu .
 
ujinga tu . endelea na mipango yako achana na mambo ya umri
Point sana hii; Ila wengi hawatakuelewa; Umri is nothing zaidi ya mind ya Mtu; Ndio maana kuna mtu ana 50 years ila ana utoto/mambo ya kitoto halafu kuna mtu ana 20-25 ila mind yake ni utu uzima full,

Achaneni na mambo ya Umri as long as uko hai katika ulimwengu huu na unaendelea kuishi basi achana na mambo ya umri. Mzee wa KFC ametoboa akiwa on his 60's huko. Ishu ni kuwa determined bila kujali umri wako;
 
Nipo katika umri huo bado napambana, sijatoboa bado.( Huko nyumbani nimeacha buku tatu tu mpaka jioni wife ndo anajua atavoipangilia.

Ila nimeamua kuwekeza sana mbiguni
Maana sikuhizi tunakufa mapema tena vijana na angali na ndoto zetu.

Kupanga Ni kuchagua yani nikose kokote mkuu.
Noted , muhimu sana kuangalia maisha baada ya kifo maana starehe za dunia ni udanganyifu mtu unaweza kuwa na pesa lakini ukawa na stress za kuchapiwa na kukosa amani.

Kuna mwehu humu aliwahi kukomenti eti "Mwenyezi Mungu siku ya kiama awapunguzie adhabu ya motoni na kuwaonea huruma wale walioishi Tanzania maana ugumu wake ni sawaa na kuishi motoni"sasa just imagine umeishi Tz kea kupigika kisha ukaishi kama hautofufuliwa tena kisha hatima yako iwe motoni unakuwa umepigika kote kote bora kuweka na kwengine tupate kusalimia.
 
Maisha ya dunia yakikuchapa mpaka umri huo Ni Bora kuanza kuwekeza kumjua mungu wako na kuitafuta pepo.

Sio pote pote ushindwe.

Ushindwe duniani na ushindwe kuu-wona ufalme wa mungu.

Japo swala la kutoka kimaisha halina umri Wala nini. Ni muda wowote tu haijalishi
kuitafuta pepo.

Ndo nini hiki???
 
Hakuna umri ambao ni very crucial kama 30-36 yrs old.

Ni umri wa mixed feelings: Depression, Anxiety, Kujuta, Furaha, ninge zinakuwa nyingi.

Mara nyingi (sio mara zote) huu ni umri ambapo hali ulio nayo kisaikolojia, physicallity (unene, wembamba etc), kihisia na kijitihada ndio itakuwa nguzo maishani mwako hadi uzee.

Ni umri wa kujiuliza hapo ulipo ndipo ulipo taka kuwa kipindi cha ndoto, matarajio, maombi na mipango wakati una umri wa miaka 16-25.

Maswali kama
■Una mke/mme
■Umeshatoka kwa wazazi
■Umepanda cheo
■Ume/una jenga nyumba,
■Una/ume nunua gari,
■Unamiliki kiwanja
■Wazazi unawahudumia,
■Umepanda cheo
■Hali yako kifedha
■Akiba na assets
■Biashara na uwekezaji wako
■Umeacha utoto.

Ni thread ya kushare changamoto, matunda, ushauri, kuelimishana na jinsi ya ku handle huu umri kwa wale tulioteleza, kuchelewa ili tujinasue b4 its very late

Karibuni.
Ndo maana mnakufa kwa stress kwa kujilinganisha na fulani wewe Ni wewe na hakuna Kama wewe, we pambana tu age is just a number!
 
Kwenye maisha stress haziwezi kuisha ukimaliza kusoma unaaamin ukipata kazi utaridhika lakin ukipata kazi unawaza vyeo/mali, ukijipindua unawaza mtoto ukipata mtoto unawaza atasomaje vizuri, bahat mbaya hata kaz unaweza usipate na kila unachoshika kikanguk yan kwakifup kwanzia unazaliwa had unaondka dunia hii huwez kuridhika na mahali ulipo

Binadam tumekua tunataman kila kizuri ambacho hatuna na kwa bahat mbaya huwez kupata vyote, unaweza ukapata mali ukakosa afya njema pia huwez kuridhika
 
Inategemea
Kwa mazingira yetu ya nchi za Dunia ya Tatu ni wachache ambao kwa umri huo wanakua wamefanikiwa kwa vigezo ulivoweka
Binafsi nipo katika umri huo. Nipo katika ajira mwaka WA pili naenda WA Tatu Sasa lakini bado bila bila zaidi ya mke na mtoto.
Mzunguko wetu WA kusoma tangu shule ya msingi mpaka chuo inafanya iwe ngumu kufanikiwa kwa vigezo vya mtoa Mada katika umri huo, inawezekana pia.
 
Hakuna umri ambao ni very crucial kama 30-36 yrs old.

Ni umri wa mixed feelings: Depression, Anxiety, Kujuta, Furaha, ninge zinakuwa nyingi.

Mara nyingi (sio mara zote) huu ni umri ambapo hali ulio nayo kisaikolojia, physicallity (unene, wembamba etc), kihisia na kijitihada ndio itakuwa nguzo maishani mwako hadi uzee.

Ni umri wa kujiuliza hapo ulipo ndipo ulipo taka kuwa kipindi cha ndoto, matarajio, maombi na mipango wakati una umri wa miaka 16-25.

Maswali kama
■Una mke/mme
■Umeshatoka kwa wazazi
■Umepanda cheo
■Ume/una jenga nyumba,
■Una/ume nunua gari,
■Unamiliki kiwanja
■Wazazi unawahudumia,
■Umepanda cheo
■Hali yako kifedha
■Akiba na assets
■Biashara na uwekezaji wako
■Umeacha utoto.

Ni thread ya kushare changamoto, matunda, ushauri, kuelimishana na jinsi ya ku handle huu umri kwa wale tulioteleza, kuchelewa ili tujinasue b4 its very late

Karibuni.
Hakuna formula ya Maisha! Acheni kutia watu pressure. Njia yako si njia ya mwingine, wakati wako siyo wakati wa kila mtu.

Vinginevyo mapacha wangekuwa wanalingana kwa viwango vya mafanikio. Watu wafanye yaliyo sawa tu.

Unajaribu kuwambia watu hapa kwamba usipofanya hayo ulisema katika umri huo huwezi tena kuyafanya?! Nonsense.

Kuna watu wametoka vyuoni at the age of 25yrs wakapata kazi yao ya kwanza wakiwa at the age of 40 years! Na wana life adorable.

Na wengi waliopata kazi at 25- 30, bado ni useless people.


Acheni kudhani mnajua maisha, acheni kuyageneralize. Life is too personal and unique to everyone of us.
 
Back
Top Bottom