30 - 36 years old: An Official Thread

30 - 36 years old: An Official Thread

Nipo katika umri huo, yapo ambayo nimetimiza na lipo ambalo sijatimiza,
Bado sijakata tamaa naendelea kumuomba Mola anijalie nitimize
 
I'm in that age. Ni umri wa pressure hasa Kama uoiokuwa nao au kusoma nao wengi wamefanikiwa. Pressure ya ndugu inaongezeka...Kama hujaoa wanataka uoe kwa haraka...hawajali struggle yako bali wanataka mafanikio yako..Kama una partiner naye anataka uharakishe mpande madhabahuni awe safe....kama upo nyumbani ni hatari zaidi.....

Wanaosema life begins at 40 huwaamini tena...wakati mwingine unaona hata ibada haziendi...it's mid life crisis ya hatari...Ila mapambano yaendeleee
 
Huo umri ni sawa umeshakosa magoli mengi sana, sasa imefika dk 95 umepewa penalt halafu ukimwangalia keeper ni kama kaenea kwenye goal galafu kama anarukaruka hivi kuziba hata vipengo vidogo.
Haha hatari
 
Tangu nifikishe miaka 30 naona mabadiliko ya mwili na roho

-nilikuwa siwezi kulala mchana saivi nalala mda wowote

-nilikuwa siwezi kukaa sehem moja kwa mda mrefu, saivi nakaa.

Na mengine mengi
Sure man, kabisaa on point, huu umri ni wa aina yake
 
kwa jinsi mambo yalivyo sjui nitafute washirika tufungue kanisa?..kwa maana bila connection mjini unaweza fikia kulamba miguu watu ila chati yako ipande kama kina mwijaku... ndo nawewe upate clown athlete yakufichia aibu..hakuna kitu kibaya kama sytsem zote zinakutema at the age of 30 going ahead..yaani hata zile za ukarani unatoswa, za makazi inatoswa..na una gamba la yudism zuri ila ndo huna sifa za kujichetua kwa kina ridhwani ama kwa gsm
Hatari boss tupambane tu
 
Me kinacho niuma nisha pita kidogo hiyo age30 but still sina mtoto, sina mke wala hata mchumba wa kuzugia, hata nikipata vipesa nabaki kuvitapanya tu kwa kuwa moyoni nisha jiwekea kuwa me furaha yangu ni kuwa na mtoto hata kama nitakosa mari za kutupwa(utajiri) ila hata mtoto wa kusingiziwa bado.
Usiji stress bro, kuwa na mtoto pale utakapokuwa tayari, usiwe pressured na umri ila uwe triggered,
 
Hapo naweza kukuelewa Sasa Mkuu, pambana,usichoke, mzee wangu katoboa Ana Miaka 40,kabla ya hapo ilikua ile vijana wanaita Apache alolo Yani hakuna kitu
Mshahara wake wakati Ana Miaka 30 ilikuwa ni laki 7 take home!!! We utatoboa tu Mkuu
Alitoboa at 40, coz alipambana from 20s to 30s, big up to your pops
 
Shemeji pole Sana,Cha muhimu ni kimoja tu,uzeeni tusiishi kwa tabu,Kuna member Fulani humu aliwahi kusema ni heri ataabike sahivi ila uzeeni aishi vizuri
Cha msingi tukifikisha 50 tusiwaze pesa ya kula Wala kulipia Kodi
Sure tupambane na tusave b4 40s, ili ikifika hizo 40s na 50s, tusiishi kwa pressure saaana
 
I'm in that age. Ni umri wa pressure hasa Kama uoiokuwa nao au kusoma nao wengi wamefanikiwa. Pressure ya ndugu inaongezeka...Kama hujaoa wanataka uoe kwa haraka...hawajali struggle yako bali wanataka mafanikio yako..Kama una partiner naye anataka uharakishe mpande madhabahuni awe safe....kama upo nyumbani ni hatari zaidi.....

Wanaosema life begins at 40 huwaamini tena...wakati mwingine unaona hata ibada haziendi...it's mid life crisis ya hatari...Ila mapambano yaendeleee
Sure boss. Pressure iko juu, ila hakuna kukata tamaa

Wanaosema Life begins at 40, hawakosei lakini wana mis interpret

Life begins at 40, after what you prepared at 20s n 30s.

Sasa chezea life in your 20s 30s alafu upambane kuishi at 40, yani hio kati ya watu 10 ni moja tu atatusua.
 
Dingi ni dingi,yaani dingi ndiyo full kujali na kunipa moyo mwanaume mwenzie,nikiona upumbavu wa sijui Nani Kama mama,natukana kinoma moyoni yaani,wanawake wengi wangese Sana yaani!!..honestly simpendi,ndiyo maana sijampa binti yoyote jina lake na sitompa
Noma sana!
 
Hakuna umri ambao ni very crucial kama 30-36 yrs old.

Ni umri wa mixed feelings: Depression, Anxiety, Kujuta, Furaha, ninge zinakuwa nyingi.

Mara nyingi (sio mara zote) huu ni umri ambapo hali ulio nayo kisaikolojia, physicallity (unene, wembamba etc), kihisia na kijitihada ndio itakuwa nguzo maishani mwako hadi uzee.

Ni umri wa kujiuliza hapo ulipo ndipo ulipo taka kuwa kipindi cha ndoto, matarajio, maombi na mipango wakati una umri wa miaka 16-25.

Maswali kama
■Una mke/mme
■Umeshatoka kwa wazazi
■Umepanda cheo
■Ume/una jenga nyumba,
■Una/ume nunua gari,
■Unamiliki kiwanja
■Wazazi unawahudumia,
■Umepanda cheo
■Hali yako kifedha
■Akiba na assets
■Biashara na uwekezaji wako
■Umeacha utoto.

Ni thread ya kushare changamoto, matunda, ushauri, kuelimishana na jinsi ya ku handle huu umri kwa wale tulioteleza, kuchelewa ili tujinasue b4 its very late

Karibuni.
Wewe unavyo?
 
Nilipokua

Nilipokua kwenye huo umri,mipango ikavurugika,nikarudi home,wa kwanza kunionesha dharau ni bi mkubwa,akawafundisha na watoto wa wadogo zangu pale home kunidharau,hakutosheka..akawa ananijengea dharau kwa watu mitaani,usiombe huo msongo wa mawazo,nikaanza kubeti nipate hela niondoke,mungu siyo benard Morrison network yangu ikalipa,kwa Sasa Nina kipato kuliko kunguni yoyote kwenye ukoo,na huwa sijui Cha kumfanya no mkubwa..Ila bado Nina grudge nae
Samehe tu maana huenda dharau zake zilikuongezea nguvu kupambana lazima uliwaza usiku na mchana.
Ukifanikiwa washukuru waliokusupport ila washukuru zaidi haters maana ndo wanakuongezea kujituma.
 
Hakuna formula ya Maisha! Acheni kutia watu pressure. Njia yako si njia ya mwingine, wakati wako siyo wakati wa kila mtu.

Vinginevyo mapacha wangekuwa wanalingana kwa viwango vya mafanikio. Watu wafanye yaliyo sawa tu.

Unajaribu kuwambia watu hapa kwamba usipofanya hayo ulisema katika umri huo huwezi tena kuyafanya?! Nonsense.

Kuna watu wametoka vyuoni at the age of 25yrs wakapata kazi yao ya kwanza wakiwa at the age of 40 years! Na wana life adorable.

Na wengi waliopata kazi at 25- 30, bado ni useless people.


Acheni kudhani mnajua maisha, acheni kuyageneralize. Life is too personal and unique to everyone of us.
Ni mwongozo tu na maoni, ukisoma hivi unaangalia ni wapi ulipo kuyokana na maoni yake, nini ufanye kama hujafanya ili walau ufike stage fulani katika maisha.

Ni kweli maisha hayana kanuni, lakini kuna namna ukienda tofauti utajishangaa mwenyewe badae.

Ni vizuri kukumbushana.
 
Back
Top Bottom