Ugonjwa wa Pumu (Bronchial Asthma): Chanzo, dalili na tiba | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ugonjwa wa Pumu (Bronchial Asthma): Chanzo, dalili na tiba

Discussion in 'JF Doctor' started by JamiiForums, Apr 10, 2009.

 1. JamiiForums

  JamiiForums Official Robot Staff Member

  #1
  Apr 10, 2009
  Joined: Nov 9, 2006
  Messages: 5,090
  Likes Received: 2,222
  Trophy Points: 280
  Utangulizi
  Ugonjwa wa pumu ni ugonjwa ambao huathiri sehemu ya kupitisha hewa kwenda kwenye mapafu ya binadamu zinazojulikana kitaalamu kama bronchioles. Mtu mwenye pumu huwa na mcharuko mwili sugu (chronic Inflammation) kwenye mirija yake ya

  kupitishia hewa (bronchioles tubes) hali ambayo husababisha kuvimba kwa kuta za mirija hii, kujaa kwa ute mzito (mucus) na kupungua kwa njia ya kupitishia hewa, hali ambayo humfanya muathirika kushindwa kuvuta na kutoa hewa

  nje na hivyo kupumua kwa shida sana. Hali hii inaweza kudumu kwa muda mfupi au mrefu kiasi cha kuhitaji tiba ili kumuwezesha mgonjwa kupata nafuu.
  Kutokana na kuwepo kwa msuguano na uzuiaji wa kupitisha hewa wakati wa kupumua hwa nje, pumu hujulikana pia kama obstructive lung disease . Mtu aliye na pumu, huwa nayo kipindi chote cha maisha yake.

  Makundi ya Pumu


  Pumu inaweza kugawanywa katika makundi mawili;

  • Pumu ya ghafla (Acute asthma): Wagonjwa wanaopatwa na kundi hili la pumu huwa na hali ya kawaida katika njia zao za hewa isiyobadilika kati ya shambulizi moja na jingine.
  • Pumu sugu (Chronic Asthma): Kundi hili la pumu huwa na tabia ya kuwa na njia nyembamba za kupitisha hewa na kadiri jinsi mgonjwa anavyoendelea kupata matukio zaidi ya pumu, njia za hewa huzidi kuwa nyembamba zaidi.


  Aina za ugonjwa wa pumu

  Bila kujalisha mgonjwa anaingia katika kundi gani, ugonjwa wa pumu unaweza kugawanywa katika aina kuu nne, ambazo ni 1.Pumu inayobadilika (brittle asthma): Kulingana na tabia ya kujirudia rudia kwa matukio ta ugonjwa huu na madhara yake kwa mgonjwa, aina hii ya pumu inaweza kugawanywa zaidi katika aina nyingine mbili, ambazo ni

  • Aina ya kwanza ya pumu inayobadilika (type 1 brittle asthma) ni pumu yenye tabia ya kuwa na matukio na mashambulizi ya kubadilika kila mara japokuwa mgonjwa anaweza kuwa anapata matibabu kadhaa.
  • Aina ya pili ya pumu inayobadilika (type 2 brittle asthma) ni pumu ambayo mgonjwa anatokea kupata shambulizi la ghafla (asthmatic attack) wakati hapo awali ugonjwa wake uliweza kuthibitiwa kwa matibabu.
  2.Pumu hatari isiyobadilika (status asthmaticus): Hii ni aina ya pumu iliyo hatari zaidi kwa mgonjwa. Pamoja na

  matumizi ya dawa kadhaa,zikiwemo vitanua njia za hewa (bronchodilators) na vipoza mcharuko mwili (steroids), mgonjwa wa aina hii ya pumu anaweza asipate nafuu ya haraka, na anaweza kupoteza maisha.
  3.Pumu

  inayosababishwa na mazoezi
  (Exercise Induced Asthma): Hali hii husababishwa na ufanyaji wa kupitiliza wa mazoezi ya viungo. Kwa kawaida wakati wa kufanya mazoezi mtu hupumua kwa kutumia pua na kupitia mdomoni. Hata hivyo wakati

  mwingine hutokea hewa aivutayo huingia ndani ikiwa haijapozwa vya kutosha puani na hivyo kusababisha ongezeko la mtiririko wa damu katika mishipa inayosambaza damu katika mirija ya kupitisha hewa. Hali hii husababisha kuvimba

  kwa kuta za mirija hiyo na muhusika kupata shambulizi la pumu. Aina hii ya pumu yaweza kudhibitiwa na dawa. Inashauriwa sana kwa watu wenye matatizo kama haya kupasha moto misuli kwa mazoezi mepesi (warming up) kabla

  ya kuanza mazoezi mazito na ya muda mrefu.
  4.Pumu inayosababishwa na aina ya kazi afanyayo muhusika (Occupational Induced Asthma): Wakati fulani, mazingira ya kazi yanaweza kusababisha kutokea kwa pumu hata kwa baadhi ya wafanyakazi wasio na tatizo hili. Mara nyingi aina hii huweza kuwatokea watu wanaofanya kazi kwenye viwanda vya kutengeneza matairi, vigae, rangi, kemikali mbalimbali, mbolea, chuma, unga na mbao.

  Pumu husababishwa na nini?


  Kuna mambo kadhaa yanayoweza kusababisha kutokea kwa pumu au yanayohusishwa na shambulizi lake. Mambo hayo ni pamoja na

  1. Matatizo ya kinasaba: Matatizo ya kinasaba yamehusishwa na kutokea kwa karibu asilimia 90 ya ugonjwa wa pumu hususani kipindi cha utoto.
  2. Uvutaji wa sigara au tumbaku kipindi cha ujauzito pia unahusishwa na kusababisha pumu kwa mtoto atakayezaliwa.
  3. Maendeleo ya kiuchumi: Ugonjwa wa pumu umeonekana sana kwenye nchi zilizoendelea kiuchumi ikilinganishwa na nchi zenye maendeleo na hali duni ya kiuchumi.
  4. Magonjwa ya mapafu kama bronchitis
  5. Vyanzo vya mzio (allergens)kama vile vumbi, vinyesi vya wanyama na baadhi ya vyakula.
  6. Uchafuzi wa mazingira kama moshi na baadhi ya harufu kali.
  7. Baadhi ya kemikali kwenye maeneo ya kazi hasa kwenye viwanda kama vya rangi, chuma, sementi na vigae.
  8. Baadhi ya wagonjwa wanaotumia dawa za kushusha shinikizo la damu zilizo katika jamii ya beta-blockers kama vile propanolol wapo katika hatari ya kupata shambulio la ugonjwa wa pumu.
  9. Magonjwa kwenye mfumo wa kupumua yasabishwayo na baadhi ya virusi na bakteria kama vile rhinovirus, Chlamydia pneumonia au Bordetella pertusis.
  10. Matumizi ya mapema sana ya baadhi ya dawa hasa antibiotiki kwa watoto yanaweza kubadilisha mfumo wa kinga ya mwili dhidi ya magonjwa na hivyo kumfanya mtoto kuwa katika hatari ya kupata pumu.
  11. Ongezeko la msongo wa mawazo huweza kusababisha pumu na matatizo katika mfumo wa upumuaji
  12. Upasuaji wakati wa kujifungua (caesarian section): Tafiti kadhaa zimeonesha kuwa kujifungua kwa njia ya upasuaji huongeza uwezekano wa kupata pumu kwa vile njia hiyo yaweza kuathiri mfumo wa kinga ya mwili dhidi ya maradhi.
  Vihatarishi vya ugonjwa wa pumu

  Uwezekano wa kupata ugonjwa wa pumu huongezeka iwapo mtu

  1. Atakuwa na magonjwa ya mzio kama vile magonjwa ya ngozi (eczema) au homa isababishwayo na aina fulani ya vumbi (hay fever)
  2. Atavuta chavu (pollen) kutoka kwenye maua au miti
  3. Atajihusisha na uvutaji sigara
  4. Ana historia ya ugonjwa wa pumu au mzio kwenye familia
  5. Utumiaji wa dawa aina ya aspirin
  6. Ana msongo wa mawazo
  7. Ana uambukizi wa magonjwa ya virusi kamarhinovirus
  8. Mazoezi
  9. Anaishi sehemu zenye baridi
  10. Ana matatizo katika njia yake ya chakula (Gastroesophageal reflux disease au GERD)

  Dalili za ugonjwa wa pumu


  Dalili za ugonjwa wa pumu ni pamoja na

  1. Kuishiwa na pumzi na kupumua kwa shida (shortness of breath)
  2. Kutoa sauti kama mtu anayepiga miluzi wakati wa kupumua (wheezing)
  3. Kukohoa sana (chronic cough) hasa nyakati za usiku au asubuhi. Aidha kikohozi huambatana na kutoa makohozi mazito, yasiyo na rangi au yenye rangi ya njano.
  4. Kubana kwa kifua.
  5. Kwa mtu aliyepata shambulizi kubwa la pumu (severe asthmatic attack) anaweza kushindwa kuzungumza na pia kuwa na hali kama ya kuchanganyikiwa.
  Vipimo na Uchunguzi [​IMG]

  Pamoja na daktari kutaka kufahamu historia ya mgonjwa, anaweza pia kuamua kufanya vipimo vifuatavyo ambavyo vitamsaidia kufahamu chanzo na madhara ya ugonjwa wa pumu kwa muathirika.

  1. Kipimo cha damu (complete blood count) msisitizo ukiwa kwenye wingi wa seli za damu aina ya eosinophils ambazo uhusika na kuwepo kwa shambulio la mzio.
  2. Kipimo cha kuchunguza uwezo wa mgonjwa kutoa hewa nje mara baada ya kuivuta (spirometery). Aina hii ya uchunguzi hufanyika kabla ya mgonjwa kupewa dawa kwa kutumia nebulizer.
  3. Kipimo cha kuchunguza kiwango cha hewa ya oksijeni kilichopo kwenye damu ya mgonjwa (oximetry).
  4. Kipimo cha kuchunguza uwezo wa mgonjwa kupumua hewa nje wakati wa shambulizi la pumu (Peak flow meter).
  5. X-ray ya kifua kwa ajili ya kutofautisha pumu na magonjwa mengine yenye dalili za kufanana kama vile ugonjwa wa moyo (congestive heart failure), magonjwa sugu ya kuziba kwa njia za hewa (COPD kama vile chronic bronchitis na emphysema) na magonjwa mengine ya kuzaliwa kama vile cystic fibrosis.
  6. Kipimo cha mzio cha ngozi (skin allergy test) kwa ajili ya kutambua aina ya mzio inayomsababishia mgonjwa shambulizi la pumu.

  Matibabu ya Pumu

  Kwa ujumla matibabu ya pumu hujumuisha kuepuka visababishi vya ugonjwa huu na matumizi ya madawa kwa walio na hali mbaya. Aidha, kwa wanaopata ugonjwa huu kwa sababu ya msongo wa mawazo hupewa ushauri nasaha kwa ajili ya

  kusaidia kutatua matatizo yanayowakabili. Vilevile inashauriwa kwa wenye tatizo hili, kuwa na dawa karibu muda wote kwa ajili ya matumizi pindi shambulizi litakapotokea. Pia inashauriwa sana kuepuka mazingira na hali za baridi ambazo

  huweza kuchochea kutokea kwa shambulio la ugonjwa huu. Matibabu ya kutumia dawa hujumuisha matumizi ya dawa za kusaidia kupunguza na kuondoa makohozi (expectorants), dawa zinazosaidia kutanua mirija ya hewa (bronchodilators), dawa za kuondoa mcharuko mwili kama vile cortisone ya drip (hasa wakati wa dharura) au nebulizer, na dawa za kuzuia

  mzio (antihistamine drugs).
  Hata hivyo, kuna matibabu ya ziada kulingana na hali ya mgonjwa pamoja na kundi na aina ya pumu inayomuathiri mgonjwa. Kwa wagonjwa wenye pumu ya ghafla na wenye hali mbaya (acute asthma) matibabu hujumuisha matumizi ya dawa za kutanua mirija ya hewa (bronchodilators) pamoja na kuongezewa hewa ya

  oksijeni, dawa za kutuliza mcharuko mwili (steroids) pamoja na dawa za kutuliza kukakamaa kwa misuli ya mwili (intravenous muscle relaxants). Aidha kwa vile mara nyingi shambulizi hili laweza kuwa la hatari sana, mgonjwa hulazwa

  hospitali na huongezewa hewa ya oksijeni, na kwa wagonjwa wasioweza kupumua kabisa, husaidiwa kufanya hivyo kwa kutumia mashine maalum iitwayo (mechanical ventilator).
  Kwa wagonjwa wenye pumu sugu, jambo la muhimu ni

  kuepuka visababishi vya pumu na kuendelea na matumizi ya dawa zinazosaidia katika kutanua mirija ya hewa. Kwa wagonjwa wanaopata mashambulzi ya mara kwa mara wanaweza kushauriwa na daktari kutumia dawa kadhaa zikiwemo zile zinazopunguza mcharuko mwili (mast cell inhibitors, inhaled steroids au oral steroids), pamoja na dawa za

  kutuliza kukakamaa kwa misuli ya mwili (muscle relaxants). Aidha ni vema pia kutibiwa na kuthibiti kutokea kwa magonjwa yote yahusuyo mfumo wa hewa. Matumizi ya chanjo ya magonjwa kama influenza na pneumococcal pneumonia nayo husaidia sana katika uthibiti wa kutokea kwa pumu. Ni vema pia kuepuka matumizi ya dawa za jamii ya beta-blockers kwa wagonjwa wenye shinikizo la damu na ambao pia wana pumu.

  Nini madhara ya pumu kwa mama wajawazito?


  Tafiti kadhaa zimeonesha kuwa takribani theluthi moja ya wajawazito wenye pumu hupata nafuu kipindi cha ujauzito, theluthi nyingine hupata matatizo kipindi hiki na theluthi iliyobakia huwa na hali ya kawaida kama kabla ya ujauzito.

  Kwa kawaida dalili za pumu hujirudia kama awali miezi mitatu baada ya kujifungua.
  Dalili za pumu kwa mjamzito zinaweza kuwa mbaya zaidi kuanzia wiki ya 24-36 (mwezi wa sita mpaka wa nane). Ni mara chache sana mjamzito

  anapata shambulizi la pumu wakati wa kujifungua. Inakisiwa kuwa, ni asilimia 10 tu ya wajawazito wenye pumu wanaopata shambulizi la pumu wakati wa kujifungua.
  Baadhi ya dawa zinazotumika wakati wa ujauzito na baada ya

  kujifungua huongeza madhara ya pumu, hivyo ni vizuri kumueleza daktari kwamba una pumu kabla ya kupewa dawa. Aidha na si vyema kunywa dawa kwa mazoea.
  Wanawake wenye pumu isiyoweza kuthibitiwa kipindi cha ujauzito

  hupata madhara ya kuzaa mtoto njiti (premature baby), kuzaa mtoto mwenye uzito mdogo, kifafa cha mimba, shinikizo la damu (Hypertension), na iwapo atapata shambulizi hatari wakati wa ujauzito mtoto anaweza kufa kwa kukosa hewa ya oksijeni.


  ===================================
  Ugonjwa wa Pumu ( Athma kwa watoto
  ===================================

  Nini maana ya Pumu?


  Pumu ni hali ambayo huathiri njia za hewa, njia hizi za hewa pia huitwa mirija ya kupumulia. Mirija hii huanzia kwenye njia ya hewa(trachea) hadi kwenye mapafu.

  Mchakato wa kupumua kwa watoto walio wengi ni rahisi : Watoto huingiza hewa kupitia puani au mdomoni na hewa huingia kwenye njia ya hewa(trachea) na kuelekea kwenye mapafu. Lakini Kwa watoto wenye pumu, hupumua Kwa shida Kwa sababu njia ya hewa hushindwa kupitisha hewa kwa sababu ya njia yao kuwa imehathiriwa na hali ya pumu.

  Shambulio la pumu (Asthma attack) ni nini?


  Hii ni hali ambayo hutokea wakati njia ya hewa inapo vimba na kuwa nyembamba na inakuwa vigumu kwa hewa kuingia na kutoka kwenye mapafu. Wakati mwingine njia za hewa zinapokuwa zimevimba hutoa majimaji mfano wa makamasi, hali ambayo husababisha mchakato mzima wa mabadlishano ya hewa katika mapafu kuwa mgumu na hii hali ndo inapelekea tatizo zima la mtotoanapo patwa na pumu kushindwa kupumua vizuri.

  Wakati ugonjwa huu unaanza, upumuaji kwa mtoto unaweza kuwa wa kawaida na kuonekana kama vile hakuna tatizo, Lakini kipindi ugonjwa unapoanza, unaweza kuhisi kwamba mtu anapumua kupitia kwenye mrija. Mtoto mwenye pumu anaweza kutoa mlio kama wa filimbi (anapopumua), kukohoa, na kusikia kifua kubana.

  Wakati shambulio la ugonjwa wa pumu(asthma attack), hali inaweza kuwa mbaya zaidi kama mtoto hatatumia dawa sahii za pumu. Baada ya kutumia dawa na kupata matibau sahii wakati wa shambulio la ugonjwa wa pumu, njia ya hewa mara nyingi hurudia hali yake ya kawaida, ingawa inaweza kuchukua muda mrefu kidogo wakati mwingine.

  Pumu huwapata watu gani?

  Pumu ni ugonjwa ambao huwapata watu wengi zaidi ya unavyo weza kufikiri.Karibia watoto milioni sita nchini marekani wanaumwa ugonjwa wa pumu(Hatujui hapa kwetu Tanzania ni idadi gani?).Ugonjwa wa pumu humpata mtoto mmoja hadi wawili katika kila watoto 10 kwa marekani. Hii ina maana kwamba kama una watoto 20 darasani, watoto 2-4 kati yao wanaweza kuwa na ugonjwa wa pumu. Ugonjwa wa pumu unaweza kumshika mtu katika umri wowote- kuanzia mtoto mchanga hadi mtu mzima-lakini huwashika zaidi watoto wenye umri wa kwenda shule(kuanzia miaka sita na kuendelea)

  Hakuna anayejua kwa uhakika kwa nini ugonjwa huu unampata mtu mmoja na kuacha mwingine, lakini tunajua kwamba ugonjwa wa pumu unatokea ndani ya familia zetu. Hii ina maana kwamba kama mtoto ana pumu, yeye pia anaweza kuwa na mzazi, ndugu, mjomba au jamaa mwingine mwenye pumu au alikuwa na ugonjwa huu wakati bado mtoto.

  Ugonjwa wa pumu unapoanza,huonyesha kama vile ni mafua,ambayo huambatana na kikohozi chenye kutoa mlio wa filimbi,lakini ugonjwa wa pumu siyo wa kuambukizwa. Huwezi kuambukizwa Kama unavyopata mafua

  Ni sababbu zipi zinazopelekea Kupata shambulio la ugonjwa wa pumu (Asthma attack)?

  Visababishi hutofautiana kutoka mtoto mmoja hadi mwingine. Sababu zipo nyingi.Baadhi ya watoto huwa na mzio(allergy), kwa vile vitu ambavyo huathiri njia ya hewa. Mara nyingi vitu vinavyoleta mzio kwa watoto wenye pumu ni vijidudu vidogo jamii ya mchwa vinavyopatikana kwenye vumbi, harufu mbaya (kama ulikuwa karibu na dimbwi na kuvuta harufu hiyo), mbelewele(pollen) kutoka mitini, majani na kwenye magugu.

  Watoto wengi hupata shambulio la pumu wanapokuwa karibu na wanyama wenye manyoya kama Paka na mbwa,baadhi watoto wanapovuta hewa iliyochanganyika na chembechembe za manyoya hawa wanaweza pata shambulio la pumu.

  Visababishi vingine ni pamoja na marashi(perfumes), vumbi la chaki, na uvutaji wa sigara. Uvutaji wa sigara sio mzuri hasa kwa mtu mwenye pumu.

  Wakati mwingine maambukizi mbalimbali yanaweza kusababisha kulipuka kwa ugonjwa wa pumu,maradhi kama mafua, Kwa baadhi ya watoto, hali ya hewa yenye baridi inaweza kusababisha kulipuka kwa ugonjwa huo,baadhi ya watoto hupatwa na matatizo ya pumu wanapokuwa wanafanya mazoezi,hii ni aina ya pumu inayosababishwa na mazoezi.

  Jinsi gani unaweza kutibu ugonjwa wa pumu kwa watoto?

  Watoto wenye ugonjwa wa pumu wanatakiwa kujaribu kuepuka visababishi vyote vinavyoweza kuwasababishia shambulio la hewa.Ingawa kuna baadhi ya visababishi kama vumbi la chaki ni vigumu kuviepuka katika mzaizngira yetu hasa shuleni,lakini mtoto,wazazi na walimu wajaribu kuwasaidia watoto wenye matatizo haya.

  Sura ya ugonjwa wa pumu hutofautiana kutoka kwa mtoto mmoja hadi mwingine, hivyo kuna dawa mbalimbali za kutibu ugonjwa wa pumu,na matibabu haya hutofautiana kati ya mtoto mmoja na mwingine hii ni baada yake daktari kujaribu kufuatilia sababu zilizopelekea ugonjwa huo, ni kwa kasi gani ugonjwa umetokea, na kiwango cha madhara ya ugonjwa huo. Hapo ndipo ataamua tiba ipi itakuwa sahii na bora kwa mtoto.

  Baadhi ya watoto wanatakiwa wameze dawa za pumu mara kwa mara punde wanapopata ugonjwa huu. Hii huitwa dawa ya dharura kwa sababu hufanya kazi ya kufungua njia ya hewa ili mtu aweze kupumua. Watoto wengine wanatakiwa kutumia dawa za kudhibiti ugonjwa wa pumu kila siku,Dawa hizi huzuia shambulio la ugonjwa(asthma attack) kutokea.Kwa hiyo matibabu ya Pumu yanatofautina kutoka mtoto mmoja na mwingine.

  Kwa watoto walio wengi ugonjwa wa pumu hupona au hupata nafuu wanapokua wakubwa. Baadhi ya madaktari wanadai kwamba hii hutokea kwa sababu, njia ya hewa hupanuka kadri mtoto anavyokua mkubwa. Njia ya hewa inapopanuka, hewa huingia na kutoka kiurahisi

  Baadhi ya watu wazima hupata ugonjwa wa pumu, lakini hii haiwasumbui.Wanariadha wengi katika mbio za olimpiki na magwiji wengine wa michezo wanaweza kuendelea na michezo hata wanapokuwa na ugonjwa wa pumu.

  UJUMBE WA KUPELEKA NYUMBANI:


  Mzazi au mlezi anayeona mtoto mwenye dalili za ugonjwa wa pumu kama nilivyouelezea hapo juu kitu cha kwanza cha kufanya ni kumwaisha Katika kituo chochote cha Afya au Hospitali iliyo karibu nae.

  Na kwa wale watoto walikwisha gundulika tayari na ugonjwa huu wa Pumu ni kuhakikisha wanafuta masharti yote ya Matibabu ili kuzuia shambulio la ugonjwa huu.

  Mtoto anayejua mapema kwamba kuna vitu vinamletea madhara katika njia ya hewa au sababu nyingine anaweza kutumia dawa mapema zitakazosaidia kufanya njia ya hewa iendelee kuwa wazi.Mtoto ambaye hupata pumu anapofanya mazoezi anaweza kutumia dawa kabla ya kufanya mazoezi ili waweze kumaliza mbio au michezo vizuri.

  Kwa watoto walio wengi ugonjwa wa pumu hupona au hupata nafuu wanapokua wakubwa. Baadhi ya madaktari wanadai kwamba hii hutokea kwa sababu, njia ya hewa hupanuka kadri mtoto anavyokua mkubwa. Njia ya hewa inapopanuka, hewa huingia na kutoka kiurahisi

  Baadhi ya watu wazima hupata ugonjwa wa pumu, lakini hii haiwasumbui.Wanariadha wengi katika mbio za olimpiki na magwiji wengine wa michezo wanaweza kuendelea na michezo hata wanapokuwa na ugonjwa wa pumu.
   
 2. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #2
  Apr 10, 2009
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  pumu ya ngozi?.... dah... kwakweli ndio mara ya kwanza hata mimi kuusikia huo ugonjwa...

  hata hivyo, waweza jifunza zaidi hapa, kwani yaelekea hauna tiba, ila waweza tafuta sababu za kuzuia hiyo allergy inayomletea hizo rashes... poleni sana jamani.


  =====================================================
  Vyakula muhimu kwa ajili ya ugonjwa wa pumu
  =====================================================

   
 3. Saikosisi

  Saikosisi JF-Expert Member

  #3
  Apr 10, 2009
  Joined: May 4, 2007
  Messages: 528
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0


  Pumu ya ngozi

  Pumu ya ngozi? Mie pia sina uhakika ni nini hiyo, lakini bado nadhani ni aina fulani ya allergy kwani allergy pia yarithiwa yakhe.
  Na kama ndio hivyo, inategemeana na umri - sometimes jinsi age inavyoongezeka tatizo huisha lenyewe.

  Na kuhusu dawa inabidi upate ushauri wa karibu wa wataalam (kwa kumuona mtoto live, sio kwa internet) kwani kumpa sana dawa zingine zaweza kumletea matatizo tena makubwa, hasa zile zenye steroids.

  Ni hayo tu.
   
 4. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #4
  Apr 10, 2009
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Kuna daktari bingwa wa mambo ya ngozi pale mitaa ya Sokoine Drive kama sikosei, ila jengo ni Luther House, Dar es Salaam.

  Unaweza kwenda pale kwa kuweka mihadi ya kuonana naye ni daktari mzuri sana. Ila sina uhakika kama bado yupo ama lah.


   
 5. k

  kizimkazi Member

  #5
  Apr 10, 2009
  Joined: Mar 10, 2009
  Messages: 59
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  ndugu yangu hiyo ni shida kubwa mimi naifaham kwa mtoto wa nduguwangu kabisa na inapona ikirudi na wataalaam wametuambia tujaribu kumuachisha baadhi ya vyakula,ilitubaini kipi kinamdhuru.na inapomzidia huwwa inamuwasha na kujikuna mpaka dam zinaanza kutoka.na huwa inaachia kwenye umri wa miaka 7 au 8 na saa ingine haiponi kabisa.kwahiyo ndugu yangu yukoktk kusubiri kama itapona au lah lakini mtoto huwa anasumbuka sana.
   
 6. b

  baraka1 Member

  #6
  Apr 11, 2009
  Joined: Jan 13, 2008
  Messages: 26
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 5
  Nashukuru sana kwa ushauri wenu na ni kweli kabisa huwa anapata shida sana wakati kunapokuwa na joto kali na Dar es salaam is always humidy. Kwa ushauri wenu nitamcheki huyu Dk. wa hapo Luther house and I hope kama tukiweza kujua ni vyakula gani au mazingira gani ya kuepuka then tutam-save mtoto but shida kubwa ni pale anaokuwa nje ya nyumbani especially in school. Ni vigumu sana ku-m-control kwenye mazingira hayo.
   
 7. S

  Sunshine OLD Member

  #7
  Apr 11, 2009
  Joined: Jul 17, 2008
  Messages: 51
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Poleni sana.
  Pumu ya ngozi ipo.
  Mie ninayo. Kawaida it's on and off inategemea na allergic reaction.
  I was advised to stop taking eggs and fish kwani zinaongeza sana joto mwilini.
  I was treated with Nerisone Cream, zipo tatu, cream, ointment na pommade.
  Ni tabu sana kupatikana kwake.
  Nilikuwa natibiwa na Prof. Masawe wa MNH, he is a skin specialist.
  Nilishauriwa kuvaa cotton outfits, nioge kwa sabuni mbuni kwani perfumed soaps zinasababisha nawashwa sana ngozi na kupiga chafya sana.
  I used to scratch myself a lot, nikoga kwa maji baridi hali inakuwa mbaya zaidi najikuna kupita kiasi. Nilifanyiwa allergy test na Dr. Mboneko naye wa MNH ila Saturdays anakuwa Luther house.
  Jaribu kuwaona hao kwa ushauri zaidi.
  Once when I was young, a Chinese Dr. advised me to take at least 16 glasses of water everyday, sikuweza. Ila he said, as I grow older tatizo linapungua,ni kweli limepungua ila halijaisha.
  Siruhusiwi kutumia hair chemicals, perfumes,etc kwani muwasho huongezeka,lakini kusema kweli, I use perfumes making sure they don't touch my skin kwa sababu I have a sensitive skin.
  Jaribu kuwaona kwa ushauri zaidi.
  Inabidi wazazi muwe waangalifu na perfumes zenu zisimpate mtoto or any other cosmetics zinazoweza kumuongezea reaction.
  Ukweli ni kwamba natumia dawa hadi leo, ila nikiona nimevimba sana, i apply the ointment, ikiishia au kupungua,naacha kabisa,it's on and off and very tiring too.
  usafi inabidi uwe wa hali ya juu.
  Poleni sana, please consult the above mentioned Dr.s.
   
 8. S

  Sunshine OLD Member

  #8
  Apr 11, 2009
  Joined: Jul 17, 2008
  Messages: 51
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Nikisisitiza swala la nguo.

  Hakikisha mashuka ya mtoto ni 100% cotton, kuna mashuka yasiyokuwa ya cotton,yanasababisha kuwashwa.
  Ikibidi kuvaa sweater liwe la material inaitwa flunnel kwani wool inasababisha ngozi iwashe.
  Blanket material haifai kwake, atumie something in cotton.
  Hakikisha nguo yake yoyote ile iwe 100% cotton kwani itamgusa ngozi atawashwa tu.
  Frommy experience, taulo pia linaniwasha,unapojifuta it's like you are stimulating the itchy skin, so dry the baby using a cotton/flunnel material uwe kama unam-sponge sio kufuta, ukifuta the sensitive skin becomes itchy again.
  Wakati wa kuoga,usitumie dodoki,it's too rough for the skin and the itchiness worsens!
  Vizuri don't scrub the child kabisa,make sure you apply the mbuni soap thoroughly ili atakate vizuri.
  Mpake Vaseline Blue Seal not perfumed lotions or body butter.
  If the skin becomes too dry it cracks na kutoa damu.
  Pumu ya ngozi need to be handled with a lot of care and patience.
  If you need to know something niulize, i live with it for many years now!
  Poleni sana.
   
 9. H

  Habarindiyohiyo JF-Expert Member

  #9
  Apr 11, 2009
  Joined: Aug 11, 2008
  Messages: 263
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  I have been athmatic since birth. Is there cure?

  .......ndiyohiyo
   
 10. Saikosisi

  Saikosisi JF-Expert Member

  #10
  Apr 12, 2009
  Joined: May 4, 2007
  Messages: 528
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Asthma not athma has no cure.

  However, about 50% of children diagnosed of asthma have spontaneous recovery by adulthood. Spontaneous recovery in adult-onset asthma is unlikely.

  Pole ila there are a lot you can do to live normally.

  Nasikia Scholes ni Asthmatic!
   
 11. H

  Habarindiyohiyo JF-Expert Member

  #11
  Apr 12, 2009
  Joined: Aug 11, 2008
  Messages: 263
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Asante, I am 33 years old, still caught by it periodically. What can I do to live normally?

  .......ndiyohiyo
   
 12. Saikosisi

  Saikosisi JF-Expert Member

  #12
  Apr 12, 2009
  Joined: May 4, 2007
  Messages: 528
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  You will probably live with it, pole.

  *Identify factors which exacerbate your asthma eg. house dust, strong scents, heavy exertion, etc. and avoid them.
  *Compliance to step-by-step prescribed medications; sio leo aminophylline tabs, kesho salbutamol tabs, siku nyingine steroid inhaler, etc.
  *Ukihisi dalili za attack pata dawa mapema usisubiri kifua kibane sana.
  *Avoid smoking, hata mtu mwingine akivuta wewe inabidi usogee mbali.
  *Live normally, meaning punguza hofu juu ya asthma yako kwani hata kwa kuwa na hofu tu waweza kupata attack.

  Good luck.
   
 13. b

  baraka1 Member

  #13
  Apr 13, 2009
  Joined: Jan 13, 2008
  Messages: 26
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 5
  Thanx Sunshine, nashukuru sana kwa ushauri wako na pole pia kwa kuishi nayo manake ni kweli kabisa inahitaji uangalifu na uvumilivu wa hali ya juu. Surely nitakutafuta kwa ushauri zaidi na tumeplan tuende kwa huyo Dk. hapo Luther house tuone what we can do to help this litle boy.
   
 14. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #14
  May 24, 2009
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,611
  Likes Received: 4,603
  Trophy Points: 280
  Asthma Home Remedy Using Garlic And Milk


  Conditions Treated: Chronic Illness

  Specific Conditions Treated: Asthma

  Ingredients Used: Garlic, Milk

  Description: Asthma is an ancient Greek word meaning 'panting' or 'short-drawn breath'. It is an allergic condition resulting from the reaction of the body to one or more allergens, and is the most troublesome of respiratory diseases.

  An asthma patient gets frequent attacks of breathlessness, in between which he may even be completely normal.

  Patients suffering from asthma appear to be gasping for breath, Actually, they have more difficulty in breathing out than breathing m, and this is caused by spasms or sudden involuntary muscular contractions of the smaller air passages in the lungs. The effect is to blow the lungs up because the patient cannot drive the air properly out of the lungs before he has to take another breath. Most asthmatics have more difficulty at night or early morning.

  Asthma is caused by a variety of factors. It may be due to an allergy caused by weather conditions, food, drugs, perfumes, and other irritants. Allergies to dust are the must common. Foods which generally cause allergic reactions are wheat, eggs, milk, chocolates, beans, fish, and sea foods. The disease may also result from psychological factors. According to some studies, about twenty-five percent of young asthmatics have a deep-seated emotional insecurity and an intense need for parental love and protection. Heredity also plays an important role.

  Modem medical system has not been able to find a cure for this crippling disease. Drugs and vaccines have only limited value in alleviating the symptoms. Most of these are habit forming and the dose has to be increased from time to time to give the same amount of relief. The frequent introduction of drugs in the system, while giving only temporary relief, tends to make asthma chronic and incurable. Allergy, which is the immediate cause of asthma, itself is an indication of lowered resistance and internal disharmony caused by faulty eating and bad habits. This is the root cause and the real cure lies in a return to nature
  Directions For Use: Ten garlic cloves, boiled in 30 ml of milk, make an excellent medicine for the early stages of asthma. This mixture should be taken once daily by the patient. Steaming ginger tea with two minced garlic cloves in it, can also help to keep the problem under control, and should be taken in the morning and evening.
  Expected Results Within: 1 month
   
 15. Sipo

  Sipo JF-Expert Member

  #15
  Aug 27, 2009
  Joined: Jul 25, 2008
  Messages: 2,146
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  napenda kuuliza dawa ya athma kwa mtoto wa miaka miwili ni ipi na naweza kupata wapi?
  Kimsingi nina mtoto wa ndugu yangu anapata sana shida na athma kiasi cha kumuonea huruma
  Tusaidiane kama kuna mtu ana uelewa wa dawa za ugonjwa huu hasa zile zisizo umiza kama hujuavyo mtoto mdogo ni mvivu wa kula sasa akipa dawa kali inakuwa tatizo tena

  Asanteni
   
 16. BelindaJacob

  BelindaJacob JF-Expert Member

  #16
  Aug 27, 2009
  Joined: Nov 24, 2008
  Messages: 6,060
  Likes Received: 475
  Trophy Points: 180
  Umeenda hospital? maana dawa hupaswi kunywa tu bila ushauri wa kitabibu.
  Nenda Morocco kwa hospital ya Dr. Massawe anashughulikia matatizo ya watoto, inahitaji uvumilivu tu kwenye kusubiri mana foleni ni kubwa ila mtoto wenu atapata kutibiwa na kupewa dawa kwa ushauri wa Doc.. Au kama uko mbali, pia tatufa Doc maeneo mlioko mtapata kumtibu mtoto pia.
   
 17. Sipo

  Sipo JF-Expert Member

  #17
  Aug 28, 2009
  Joined: Jul 25, 2008
  Messages: 2,146
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Ngoja nitoe hii habari kwa mhusika ili amcheki dr. Massawe
  Asante belinda
   
 18. Sipo

  Sipo JF-Expert Member

  #18
  Aug 28, 2009
  Joined: Jul 25, 2008
  Messages: 2,146
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  lakini inakuwaje mtoto anapoenda kwa daktari ananyimwa kula vitu vifuatavyo kwa ushauri kuwa vinamletea aleji
  Maziwa
  Nyama
  Samaki
  Juice
  Soseji
  Blueband
  Jam

  Sasa atumie vyakula gani mbadala?
   
 19. P

  Paul S.S Verified User

  #19
  Jan 4, 2011
  Joined: Aug 27, 2009
  Messages: 5,933
  Likes Received: 276
  Trophy Points: 180
  Wadau naombeni mawazo yenu nina mtoto wa dada yangu anasumbuliwa sana na kifua, haipiti miezi miwili lazima atabanwa na kifua sana.
  Baada ya uchunguzi ikaja gundulika baba yake anamatatizo ya pumu na kwakuwa ugojwa huu ni wa kurithi, basi amemuachia na mwanae.
  Katika harakati za matibabu kuna nesi akamwambia sister pumu kwa hospitali haina dawa ila kuna mitishamba yaani dawa za kienyeji zinaponesha pumu na hasa akiwa bado mdogo.
  Je kuna yeyote mwenye experiance na hili au amewahi sikia tufahamishane.
  Nawasilisha.
   
 20. Riwa

  Riwa JF-Expert Member

  #20
  Jan 4, 2011
  Joined: Oct 11, 2007
  Messages: 2,601
  Likes Received: 232
  Trophy Points: 160
  Mimi ni mdau wa afya...kwa taaluma yangu nafahamu kuwa hakuna tiba ya Pumu (kwamba haitibiki ikakoma isitokee tena). Pumu inafanana na allergy jinsi inavyotokea, kunakuwa na kianzishi (allergen/trigger) halafu njia ya hewa ina'respond' kwa kubana haswa wakati wa kutoa hewa nje. Kikohozi na mafua ni moja ya vianzishi. Wakati mwingine Pumu inaweza ikaacha yenyewe (hasa inayoanzia utotoni) lakini sio mara zote.

  Dawa zilizopo sasa na kupatikana hospitali au madukani husimamisha 'attack' inapotokea kwa kupanua njia za hewa ili mgonjwa apumue kawaida, hazitibu kuponyesha tatizo moja kwa moja.

  Sijasikia bado dawa ya kienyeji iliyothibitishwa kuwa inapunguza kutokea kwa pumu au kutibu pumu kabisa. Kwa maelezo zaidi unaweza kwenda Muhimbili kitengo cha dawa asilia watakufahamisha.
   
Loading...