Je, wajua? - Special Thread

mandella

mandella

JF-Expert Member
Joined
Oct 29, 2011
Messages
2,886
Points
2,000
mandella

mandella

JF-Expert Member
Joined Oct 29, 2011
2,886 2,000
Habari zenu wadau.

Wote tunaamini kua kuna mambo mengi sana ya kisiasa, elimu, sayansi, geografia, na maarifa mengine mengi tu ambapo kwa namna moja au nyingine mtu unakua hujapata fursa ya kuyashuhudia au kuyasikia kwa muda muafaka. Hii inaweza kua kipindi kilichopita au hata kwa wakati huu ulipo.

Basi kupitia Thread hii ni vyema wadau tukafahamishana haya kwa lengo moja la kuelimishana.

Hivyo niwakaribishe wote wenye nia njema kuwekea wayajuayo, kwani ukijuacho wewe naweza nisikijue na akijuacho mwenzanko unaweza usikijue.

Karibuni.Mende ni mdudu anayeweza kuishi zaidi ya mwezi bila ya kula chakula chochote.

Ni mdudu anayeweza kuishi wiki mbili bila ya kunywa maji.

Wakati moyo wa mwanadamu ni mmoja wenye chemba nne mende ana moyo mmoja wenye chemba kumi na tatu.

Baadhi ya mende wa kike hawaitaji wanaume kuweza kuzalisha mayai hupandana wao kwa wao na kutaga mayai katika kipindi chote cha maisha yao.

Mende ana uwezo wa kukaa kwa zaidi ya dakika 40 bila ya kupumua.

Mende ana uwezo wa kuishi zaidi ya wiki mbili akiwa amekatwa kichwa.

Ana uwezo wa zaidi ya mara 15 ya binadamu wa kuzuia miale mikali ya nuklia isimdhuru na kubaki hai

Mende ni mdudu asiye na mapafu.

Ana uwezo wa kuruka maili 3 kwa saa


1:mtu akiwa analia halafu chozi la kwanza kudondoka likatokea jicho la kulia basi kilio kile ni cha furaha na likitokea jicho la kushoto linaasharia ni majonzi

2:tunavalishana Pete za ndoa kwenye kidole cha kushoto kwa sababu hiki kidole ni pekee kilichoonganishwa moja kwa moja na mshipa wa vein unao peleka damu kwenye moyo moja kwa moja

3:duniani tupo billion 7 hivyo ukisema ukutane na kila mtu kwa kila sekunde moja basi utachukua miaka 32 kukutana na sisi wote

4:utafiti umeonyesha kuwa binadam wengi tunakuwa na furaha kila inapofika 7:26 pm (saa moja jion) kila jumamosi

5:kumbe mende akikugusa labda hata kwa bahati mbaya basi ni lazima akimbilie mahali salama na akifika anafanya kama kujisafisha

6:kila mwaka kwa wastani wanakufa watu 7000 kutokana na madhara ya miandiko ya ki daktari ambayo inapelekea kuchambuliwa na kueleweka vibaya mfano na wauza madawa wanatafsiri vibaya na wkakupa dawa nyingine tofauti na iliyoandikwa

7:ukiingia Google ukawa search hizi namba "241543903" basi utakutana na picha za watu mbalimbali wame piga wamejifungia kwenye friji
8:96% ya watu hawajui kama osman bin laden alishawahi kuwa agent wa CIA MIAKA ya 1980

9:watu wanaocheza game za video wanakuwa wepesi wa kufanya maamuzi hata katika maisha yao ya kila siku ya kawaida

10:95% hawaipendi Sauti yao wenyewe iliyorokediwa kwenye video
11:bill Gates alishawahi kumwambia mwalim wake kuwa lazima atakuwa millionea akifikisha miaka 30.. Akawa billionea akiwa na miaka 31

12:mabadiliko ya haraka ya kihisia kutoka kwenye mood ya furaha ukaingia kwenye mood ya huzuni ni kiashiria kwamba kuna mtu una mmiss sana

13:uwezo wa mwanamke kusoma hisia za mtu ni mara kumi ya uwezo alionao mwanaume

14:75% ya watu hujaribu kurud kitandani asubuhi Ili wamalize tu ndoto zao mbazo hazikukamilika

15:utafiti uliofanyika kwa watu wazima 3000 unasema kulala upande wa kushoto wa kitandani una kufanya uwe na mitazamo chanya zaidi

16:viatu virefu wanavovaa dada zetu vilitengenezwa kwa ajili ya wanaume hasa wanaouza nyama buchan na lengo ilikuwa kuzuia kugusana na damu iliyopo chini

17:kwa wastani unaweza kujiangalia kwenye kioo mara tano na kiasi kikubwa ukajiona unavutia tofauti na uhalisia kumbe hata huvutii sana sasa ile ni kazi ya part fulani katika ubongo. Asante ubongo

18:kwa utafiti wa wanawake wa UK umeonyesha kwa siku wanawake hujitathimi juu ya muonekano wake si chini ya mara tisa
Na ni asilimia 4 tu ya wanawake ndo wanaridhika na muonekano walionao

19:111111111 mara 111111111=12345678987654321

20:ukilia unatoa homoni ya stress na ndo maana ukimaliza tu kulia unaanza kuhisi kama unajiskia vizuri hivi

21:rangi halisi ya pundamilia ni nyeusi ile nyeupe ndo mkanda tu iliyojizungusha

22:HATA UJITAHIDI KWA NAMNA GANI HUWEZI KUKUMBUKA JINSI NDOTO ULIYOOTA ILIVYOANZA SANA SANA UTAKUMBUKA KATIKATI NA ILIVYOISHIA

23:kama mabinti mapacha wakiolewa na wanaume wawili mapacha basi Watoto watakaozaliwa na kila couple watafanana kila kitu

24:KUNA WAKATI UNAHISI UME MMISS MTU FULANI UKWELI NI KUWA HAUJAMMISS YEYE BALI NI MEMORIES

25:75% ya mawazo yetu ni tafakar za kurudisha kumbukumbu na kutengeneza kwa Ubunifu wa hali ya juu namna tunavotaka maisha yawe mazuri

26:watu wenye tabia ya kuisaidia wengine mara kwa mara huwa na furaha na ina ongezeka jinsi wanavyozeeka

27:ASILIMIA 90 YA BINADAMU WANAFIKIRIA KUFANYA MAAMUZI MAGUMU JUU YA JAMBO FULANI KIPINDI WAKIWA WANAOGA

28:asilimia 90 ya unawowasamehe bado unawahitaji kuwa sehemu ya maisha yako

29:mamalia anayekuwa haraka ni nyangumi na anayekuwa taratibu kupita wote ni BINADAMU

30:WANAUME WANAOWABUSU WAKE ZAO KILA ASUBUHI WANA FAIDA YA KUISHI MIAKA 5 ZAIDI MBELE

31:WANAWAKE WANA JIKUTA WANAVUTIWA NA WEWE ENDAPO TU WAKIGUNDUA KUNA WANAWAKE WENZAO ZAIDI YA WAWILI WANAKUANGALIA WEWE BILA YA WEWE KUWAONA WAKIKUANGALIA

32:mimba ya jack chain HAIKUWA miezi 9 ilikuwa 12

33:ng'ombe ana uwezo wa Kutoa maziwa mengi akikamuliwa kipindi anasikiliza nyimbo tulivu

34:KUMBE MBU AKISHAKUNYONYA DAMU HAKUACHI MPAKA AKUKOJOLEE JAPO KIDOGO
1. Nchi ya Gambia ina chuo kikuu kimoja tu (The University of Gambia).

2. Equatorial Guinea ni nchi pekee Afrika ambayo lugha yake ya Taifa ni Kispaniola (Spanish). Hakuna nchi nyingine Afrika inayozungumza Kispaniola.

3. Afrika kusini ndiyo nchi inayotembelewa na wageni wengi zaidi kuliko nchi zote za Afrika.

4. Nigeria ndio nchi yenye matajiri wengi weusi kuliko nchi nyingine za Afrika (richest Black people).

5. Samuel Eto’o ndiye mchezaji anayelipwa ghali zaidi kuliko wachezaji wengine kutoka Afrika. Analipwa Euro 350,000 kwa wiki (sawa na shilingi milioni 980,000/=). Kwa lugha rahisi ni kwamba mshahara wa Et'oo wa wiki 7 unalingana na pesa zote alizoiba Rugemalira kupitia Escrow na kugawia kina Tibaijuka na Ngeleja.

6. Raia kutoka Nigeria anaitwa Nigerian, Raia wa Niger anaitwa Nigerien na raia wa Burkina Faso anaitwa Burkinabe.

7. Nigeria imeshinda vikombe vingi vya soka kuliko Uingereza (England).

8. Ethiopia na Liberia ni nchi pekee Afrika ambazo hazijawahi kutawaliwa. Italia ilipojaribu kuitawala Ethiopia iliishia kupigwa vibaya na ikassurender.

9. Kabila la Limba huko Zambia, mama wa mvulana ndiye anayemtafutia mwanae binti wa kuoa. Mama ndiye anayemuapproach binti, na kulipa mahari kabla hata binti hajamuona kijana mwenyewe. Kinachotakiwa ni binti kumkubali mama tu.. Ukimkubali mama means umemkubali na mwanae. So mwanae utakutana nae kwenye harusi, mambo mengine kabla ya harusi anafanya mama yake.

10. Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe ndiye Rais msomi zaidi duniani. Ana degree 7 alizozisomea ktk vyuo vikuu mbalimbali, mbili kati ya hizo ni Masters.

11. Zinedine Zidane aliwahi kurudi nchi yake ya asili Algeria ili aichezee kwenye mashindano ya kimataifa. Alipofika waziri wa michezo wa Algeria, Abdelmalek Sellal akamwambia "tuna wachezaji wengi wazuri kuliko wewe na hawajapata nafasi kwenye kikosi. Labda tungeruhusiwa kucheza zaidi ya 11 uwanjani ungeweza kubatika kupata namba"

12. Robert Mugabe ndiye Rais mzee zaidi duniani. Anashikilia rekodi kwa kuwa na umri wa miaka 91 akifuatiwa na Shimon Peres, Rais wa Israeli mwenye miaka 90.

13. Shelisheli (Seychellois) ndio nchi ya kwanza duniani ambayo raia wake wameelimika kuliko nchi nyingine. Inakadiriwa kuwa asilimia 91.9% ya watu wake wana elimu ya sekondari na kuendelea. (Tanzania wenye elimu ya sekondari na kuendelea ni asilimia 13.5 kwa mujibu wa HakiElimu.)

14. Mauritius ndiyo nchi pekee Afrika inayoingiza fedha nyingi kupitia utalii wa fukwe (Beach Tourism). Mwaka 2013 iliingiza takribali shilingi trilioni 4.5 kupitia utalii wa fukwe. Tanzania tuliingiza shilingi bilioni 1.7 kupitia Utalii wa fukwe mwaka huohuo.

15. Rwanda ndiyo nchi pekee yenye usawa wa kijinsia kuliko nchi zote duniani (Bunge la Rwanda ni 50% wanaume na 50% wanawake).

16. Ethiopia ndio nchi pekee Afrika yenye viwanja vingi vya ndege vyenye hadhi ya kimataifa (International Airports). Ina viwanja vya ndege 23 vyenye hadhi ya kimataifa. (Tanzania tuna viwanja vya ndege vitatu vyenye hadhi ya kimataifa (JNIA-Dar, KIA-Moshi, na Songwe-Mbeya).

17. Uchumi wa Ethiopia unakua kwa kasi kuliko Uchumi wa China. Uchumi wa Ethiopia (GDP) unakua kwa wastani wa 18.7% kwa mwaka, China GDP inakua kwa wastani wa 11.4% kwa mwaka (according to the World bank fact sheet, 2014)

18. Rais wa Eritrea Isaias Afwerki ndiye Rais Maskini kuliko wote Afrika. Analipwa mshahara wa Dola 500 za kimarekani ($ 500) sawa na Shilingi 945,000/=. Hiki ni kiwango kidogo cha mshahara kuliko daktari wa mfunzo nchini Tanzania (Intern Doctor).

19. Angola ina watu wengi wanaoongea Kireno kuliko Ureno kwenyewe. Angola ina watu milioni 22 na wote wanaongea Kireno, lakini Ureno ambao ndio wenye lugha wana watu milioni 10.7 tu.

20. Somalia ilipata mashine yake ya kwanza ya ATM tarehe 7, October, 2014. Kabla ya hapo hakukuwa na ATM yoyote nchini Somalia.
Je, wajua kwamba kuna mambo haya yanayokuzunguka?

1. Je, wajua kwamba binadamu pamoja na akili zake zote, pamoja na mbwembwe zake nyingi, bado hana uwezo wa kufikisha ulimi kwenye kiwiko cha mkono wake?

2. Je, wajua kwamba kama piza zinazoliwa kwenye bara la Amerika kwa siku zingepangwa zingeweza kuchukua eneo lenye ukubwa wa hekta 18?

3. Je, wajua kwamba kila binadamu ana alama tofauti kabisa na za kipekee katika ulimi wake (tongue-prints) kama zilivyo za vidole?

4. Je, wajua kuwa mnyama aina ya mamba huwa hana uwezo wa kutoa ulimi wake nje kutokana na maumbile yake?

5. Je, wajua kuwa farasi na panya ndio wanyama pekee wasiotapika?

6. Je, wajua kuwa jicho la mbuni ni kubwa kuliko ubongo wake?


7. Je, wajua kuwa licha ya binadamu kuwa na uwezo wa kubana pumzi zake, bado hawezi kujiua kwa njia hiyo?

8. Je, wajua kwamba kwa wastani kichwa cha mwanadamu hubeba nywele zipatazo 100,000 na kila unywele unakua kwa wastani wa sentimita 12.5 kwa mwaka?

9. Je, wajua kuwa siafu ndio viumbe pekee wasiolala maisha yao yote?

10. Je, wajua kwamba mwanadamu ambaye anaweza kuishi kwa wastani wa miaka kati ya 50-60, anaweza kuzalisha kiasi cha mate kinachofikia galoni 10,000?

Je, wajua kuwa mwili wa mwanadamu una kiwango cha mafuta chenye kuweza kuzalisha miche saba ya sabuni?

11. Je, wajua kuwa katika ngozi ya mwanadamu mmoja pekee kuna idadi kubwa ya viumbe hai kuliko idadi ya wanadamu wote walioko katika ulimwengu mzima?

12. Je, wajua kuwa kama mdomo wako ukiwa mkavu kabisa huwezi kutofautisha ladha mbalimbali?

13. Je, wajua kuwa ubongo wa mwanadamu hutumia zaidi ya asilimia 25 ya oksijeni yote inayotumiwa na mwanadamu?

14. Je, wajua kuwa kila dakika moja inayopita, kuna seli kati ya alfu 30 hadi 40 zilizokufa zinazodondoka toka katika mwili wa mwanadamu?

15. Je, wajua kuwa ubongo wa mwanadamu umeumbwa kwa maji kwa kiwango cha asilimia 80?

16. Je, wajua kuwa kati ya viumbe wote duniani, ni mwanadamu pekee ambaye anaweza kulala kwa kutumia mgongo wake?

17. Je, wajua kuwa ukubwa wa jicho la mwanadamu daima ni ule ule toka anapozaliwa hadi anapozeeka? Pua na masikio hukua kwa kadiri mwanadamu anavyozidi kukua.

18. Je, wajua kuwa paka ana uwezo wa kubadili sauti yake na kufanya milio zaidi ya 100 tofauti tofauti wakati mbwa ana uwezo wa kufanya hivyo na kutoa sauti kumi tu?

19. Je, wajua kuwa visiwa vya Hawaii huvisogelea vile vya Japan kwa umbali wa inchi 4 kila mwaka?

20. Je, unajua kuwa kutengeneza karatasi mpya kutokana na karatasi za zamani zilizoisha matumizi yake kunaweza kusaidia kupunguza matumizi ya nishati kwa asilimia takriban 70 kulinganisha na kutengeneza karatasi hizo kutokana na miti
Chakula cha ubongo

Je wajua?

1. Mbu wanafurahi sana kuuchezea mwili wa mtu aliyetoka kula ndizi

2. Wanaume wa calibri huko kusini mwa australia husalimiana kwa kutingishana sehemu zao za siri badala ya mikono

3. Wakati wa mazishi ya mgunduzi wa simu sir alexander graham bell mitambo yote ya simu marekani ilizimwa kwa dakika moja.

4. Kanisa katoliki limeweka historia ya kuwa na mtakatifu alyekuwa na uwezo wa kuonekana sehemu mbili kwa wakati mmoja (mult location)

5. Ulaji wa ini la kuku mara kwa mara laweza kubadilisha group la damu toka group a kwenda o.

6. Wanadamu wote tunaongezeka urefu sentimita moja kila asubuhi na kurudi katika hali ya kawaida kadri muda unavyozidi kusogea.

7. Ng'ombe huongeza utoaji wa maziwa wanaposikiliza muziki ukiwa jirani na wanapokamuliwa.

8. Mbu ana meno 47.

9. Tembo anasikia sana ukiongea kwa sauti ya chini.

10. Simba akiwa jirani akinguruma sauti yake husikika kama mtu anayepiga debe au bati.

Hiyo ni kumi kutoka kwangu.
 
YAKUTA

YAKUTA

JF-Expert Member
Joined
Aug 11, 2013
Messages
387
Points
225
YAKUTA

YAKUTA

JF-Expert Member
Joined Aug 11, 2013
387 225
Je wajua Kisiwa cha Mafia kilichopo bahari ya Hindi chenye kata 7 na wakazi wapatao 60,000 hakuna hata shule moja ya kidato cha sita?
sasa kama shule nzima inawanafunz 120 kuanzia form 1-1V we unadhan form V wataenda wangap kwa ufaulu wa miaka hii?
 
Doyi

Doyi

JF-Expert Member
Joined
Dec 4, 2011
Messages
852
Points
250
Doyi

Doyi

JF-Expert Member
Joined Dec 4, 2011
852 250
ju wajua uzito wa tembo unalingana au umepishana kidogo sana na uzito wa mnyama nyangumi?? wajua hilo??
 

Forum statistics

Threads 1,304,903
Members 501,587
Posts 31,531,248
Top