uchaguzi

Uchaguzi Tanzania
Uchaguzi hasa wa viongozi katika nchi ni utaratibu (mchakato) rasmi unaoendeshwa kwa mujibu wa sheria kuwawezesha wananchi kufanya maamuzi kwa njia ya kuwapigia kura kuwachagua watu ambao wanawataka kuwaongoza kwa kipindi maalum.

Uchaguzi ni utaratibu wa kawaida wa demokrasia wa kuwapata wawakilishi wa kisiasa ambao umekuwa ukitumika tangu karne ya 17. Kuna aina tatu za msingi za uchaguzi zinazotumiwa kuwapata viongozi kulingana na mfumo unaotumiwa na nchi husika.

Aina hizo ni uchaguzi wa Rais, Uchaguzi wa Wabunge na Wawakilishi katika Baraza la Kutunga Sheria na Uchaguzi wa Viongozi wa Serikali za Mitaa.

Vyama vya Siasa kwa upande wao navyo huendesha chaguzi ambazo zinajulikana kwa jina la “Chaguzi wa Msingi” zinazotumika kuwachagua wateuliwa wa vyama katika aina za uchaguzi ambazo zimetajwa hapo juu.

Endapo Tume haitaridhika kabla ya kutangaza matokeo ya uchaguzi kwamba kulikuwa na kutokufuatwa kwa taratibu, matumizi mabaya au ukiukwaji wa taratibu za uchaguzi au pale ambapo kura za wagombea waliopata kura za juu imelingana, Tume itasimamisha au kufuta uchaguzi au sehemu yoyote ya uchaguzi na itatangaza siku nyengine ya kurudiwa kwa uchaguzi huo.
  1. J

    JamiiForums Tanzania GE2020 RC Makonda: Viongozi wa dini ombeeni uchaguzi ili tupate viongozi Watakatifu wa kumsaidia Rais Magufuli na watoa kafara wasifurukute

    Mkuu wa mkoa wa Dsm mh Makonda amefanya kikao na viongozi wa dini kupitia jukwaa lao la Kamati ya maridhiano. Makonda amewataka viongozi hao wa dini kuuombea uchaguzi mkuu ili wakapatikane viongozi watakatifu watakaomsaidia Rais Magufuli katika awamu yake ya pili ya uongozi. Makonda amesema...
  2. chiembe

    JamiiForums Tanzania GE2020 Ni mambo yapi unaiambia serikali ya CCM "we can't breathe" ili CCM iondoe goti katika shingo za Watanzania, ili yawe ajenda ya uchaguzi?

    "I can't breath" ni kauli aliyoitoa George Floyd wakati askari mmoja huko marekani alipomkamata na askari huyo kuweka goti lake katika shingo ya George Floyd, jambo lililosababisha akose hewa kisha kufariki. Naipa kauli hiyo muktadha wa kitanzania kisiasa. Ni mambo gani ambayo yanafanya...
  3. RAKI BIG

    JamiiForums Tanzania Bila tume huru hakuna uchaguzi huru

    (Hotuba ya Mwenyekiti wa ACT Wazalendo Ndugu Maalim Seif Sharif Hamad,Mwenyekiti wa Chama Taifa Kuhusu Masuala ya Msingi Kuelekea Uchaguzi Mkuu 2020) Ndugu Watanzania, Kama inavyofahamika, 2020 ni mwaka wa Uchaguzi Mkuu. Tanzania inatarajiwa kufanya uchaguzi wa madiwani, wabunge, wawakilishi na...
  4. S

    JamiiForums Tanzania GE2020 Kabla ya Uchaguzi Mkuu wa baadae mwaka huu, Mungu atatufuta machozi wapinzani kwa kuangusha mbuyu

    Maandiko matakatifu yanasema "anaeua kwa upanga,atakufa kwa upanga" na Waswahili wanasema "Mungu si Athumani".Pia kuna msemo:" Mungu hadhihakiwi." Kwa kuzingatia misemo hiyo na kwa kuzingatia machozi,machungu na kilio cha watu wake,Mungu atajibu kadri atavyyona inafaa na anaweza kujibu kwa...
  5. Mzee Koyu Mbochi

    JamiiForums Tanzania Kuelekea Uchaguzi Mkuu: Rais Magufuli amecheza kama Messi

    Salaam wanajamvi, Itakumbukwa kwamba ujio wa COVID-19 umekuwa ni mtihani mkubwa kwa marais wa mataifa mbalimbali hususani yanayotegemewa kufanya uchaguzi mwaka huu na mwaka ujao. Corona imekuwa ni moja ya mitihani mikubwa mwaka huu. Niende moja kwa moja nchini (Tanzania), Corona ilipoanza...
  6. mkiluvya

    JamiiForums Tanzania GE2020 CHAUMMA kushiriki Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba 2020

    Chama cha Upinzani cha CHAUMMA, kimetangaza rasmi kushiriki Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba mwaka huu. Mwenyekiti wake, Hashim Rungwe Spunda amesema wanavikaribisha vyama vingine kuungana nao wakati ambao CHAUMMA inaelekekea kuchukua dola. Rungwe amesema, hivi karibuni Chaumma itatoa...
  7. S

    JamiiForums Tanzania GE2020 Wapinzani msimuamini sana Membe kwa yoyote atakayosema na kuyatenda kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu baadae mwaka huu

    Mwanasiasa ambae anaweza kujiamini kusema na kufanya lolote kwa lengo la kukosoa watawala waliopo madarakani bila hofu ya kushitakiwa,mali zake kutaifishwa au kunyang'anywa,n.k ni yule tu ambae wakati alipokuwa kwenye system, hakuwahi kutuhumiwa kufanya ufisadi,wizi,kujihusisha na...
  8. FRANC THE GREAT

    JamiiForums Tanzania Joe Biden ashinda rasmi uteuzi wa Chama cha Democratic kugombea nafasi ya urais nchini Marekani

    Joe Biden ameshinda rasmi uteuzi wa Chama cha Democratic kumkabili rais Donald Trump katika kinyang'anyiro cha uchaguzi wa rais utakaofanyika panapo mwezi Novemba mwaka huu. Biden amesema katika ukurasa wake wa Twitter kwamba amefanikisha kujikusanyia wajumbe 1,991 wanaohitajika ili kupitishwa...
  9. ubongokid

    JamiiForums Tanzania GE2020 Siasa za uchaguzi na fursa kwa wajasiriamali

    Habari za wakati huu, Kwanza nianze kwa kuwapa pole wale ambao katika kipindi hiki cha COVID wamejikuta katika wakati mgumu kwa sababu moja ama nyingine katika biashara zao na maisha kwa ujumla na kwa wale ambao wameifariki dunia katika kipindi hiki wapumzike kwa amani. Nirudi kwenye mada kwa...
  10. Allen Kilewella

    JamiiForums Tanzania GE2020 Kusipokuwa na uchaguzi wa kuchagua Rais kuna haja ya kufanya uchaguzi?

    Wana CCM wengi sana wanatamani kwa mtizamo wao ghushi na uliojaa ugoto katika kufikiri, kuwa John Magufuli asipingwe na mgombea toka CHADEMA. Wao wanadai kwa aliyoyafanya Magufuli kama Rais wa Tanzania hakuna haja ya kupingwa. Lakini najiuliza kama Magufuli wanataka apite bila ya kupingwa, je...
  11. Roving Journalist

    JamiiForums Tanzania Rais Magufuli afungua mkutano Mkuu wa Chama cha Waalimu, Corona imeisha, Shule za Msingi kufunguliwa karibuni

    Salaam Wakuu, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, Leo anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika Mkutano Mkuu wa Uchaguzi wa Chama Cha Walimu Tanzania-CWT. Mkutano huo utafanyika katika Uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma, huku watu wote wakitakiwa kuzingatia na kuchukua...
  12. Mzalendo2015

    JamiiForums Tanzania GE2020 Rais Magufuli lipa Mafao ya Wastaafu kabla ya Uchaguzi Oktoba 2020

    Kulingana na report ya Ukaguzi ya CAG 2019/20 Serikali inadaiwa na Mifuko ya Jamii PSSSF kiasi cha zaidi ya Tshs. 700 Bilioni ambazo Serikali imekopa toka PSSSF na haijarudisha/kulipa fedha hizo. Kuna Habari za kuaminika kwamba fedha hiyo imekopwa kwenda kujengea miradi mikubwa ya Serikali...
  13. M

    JamiiForums Tanzania GE2020 Ilani ya Uchaguzi inayofaa 2020 ni ile itakayochochea Ukuaji wa Uchumi kwa wote

    Ilani ya uchaguzi itakayochochea ukuaji wa uchumi kwa wote na kuongezea serikali kodi ndio inafaa. Vyama vya Siasa inatakiwa vije na Ilani na Mipango ambayo inampa Mtanzania Uhuru wa kuchagua ni wakati gani wa kuajiriwa na ni wakati gani wa kujiajiri. Ilani ipange kuondoa vipingamizi kwa...
  14. Q

    JamiiForums Tanzania CCM imezindua kituo cha kutoa taarifa za wala rushwa wakati wa uchaguzi. Hawaiamini TAKUKURU?

    Katibu wa Halmashauri Kuu Itikadi na Uenezi, Humphrey Polepole amesema kwamba Chama Cha Mapinduzi kimezindua kituo maalum cha wananchi kutoa taarifa za Uchaguzi kimaadili ili kuwabaini wala na watoa Rushwa, kuelekea Uchaguzi Mkuu Oktoba 2020.
  15. YEHODAYA

    JamiiForums Tanzania Vyama vya upinzani, uchaguzi huu ungeni mkono mgombea urais wa CCM hamna mgombea wa maana wa kushinda kwenu

    Vyama vya upinzani havina mgombea yeyote wa maana wa kushinda uchaguzi wa urais kupitia vyama vyao sababu vyote kwanza havina nguvu pande zote za muungano. Chadema ina nguvu Tanzania bara tu mkoa wa Kilimanjaro tu kidogo mji wa Arusha upande wa Zanzibar hamna kitu. Hivyo akiwekwa mgombea uraisi...
  16. J

    JamiiForums Tanzania Ni ujinga uliopitiliza kupanga foleni kumpigia kura mgombea wa CHADEMA/upinzani wakati msimamizi wa uchaguzi ni kada wa CCM

    Wananchi ni lazima tujue kwamba katiba ya JMT ndio inayobariki ushindi wa CCM. Na kiukweli ukiangalia maeneo ambayo upinzani huwa unashinda mara nyingi inakuwa ni ulegelege wa mkurugenzi ambaye ndiye msimamizi wa uchaguzi au huruma tu ya CCM yenyewe. Ni wale wananchi wapenda mageuzi mkaendelea...
  17. Roving Journalist

    JamiiForums Tanzania Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC): Hatuwezi kubeba lawama kwa wananchi kukosa Vitambulisho vya Mzanzibar mkaazi kwani sio Mamlaka yetu

    Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) Jaji mstaafu Hamid Mohamoud Hamid, amesema Tume hiyo haiwezi kubeba lawama kwa wananchi kukosa Vitambulisho vya Mzanzibar mkaazi kwani hiyo sio Mamlaka yake kwa mujibu wa sheria. Akizungumza na Waandishi wa habari, Ofisi ya Tume ndogo ya Uchaguzi...
  18. Miss Zomboko

    JamiiForums Tanzania ACT Wazalendo: Maoni ya Upinzani kuhusu mabadiliko ya rasimu ya Uchaguzi hayazingatiwi

    Chama cha ACT- Wazalendo kimelalamikia kutozingatiwa kwa maoni ya vyama vya upinzani katika mchakakato wa mabadiliko wa maadili ya uchaguzi katika uchaguzi mkuu unaotarajia kufanyika Oktoba mwaka huu. Akizungumza leo na vyombo vya habari katika ofisi ndogo za chama hicho zilizopo Magomeni...
  19. RAKI BIG

    JamiiForums Tanzania GE2020 Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) iachane na njama za kuvuruga uchaguzi, zitaligharimu Taifa

    Taarifa ya Katibu Mkuu wa ACT Wazalendo, Ndg. Ado Shaibu, leo tarehe 02 Juni 2020. Chama cha ACT Wazalendo kinasikitishwa na kupinga vikali mwenendo wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kuendesha mchakato wa mabadiliko ya Kanuni mbalimbali za Uchaguzi bila kuwashirikisha vya kutosha wadau wa...
  20. APA CHICAGO

    JamiiForums Tanzania Ombi kwa Serikali yetu kwenye Sheria za Uchaguzi

    Ninaombi kwenye sheria zetu za uchaguzi kipengele kimoja tu kibadilishwe au kiongezwe. Kwa maoni yangu ningependa iwe hivi Mbunge yeyote " Akijihudhuru au kuhama chama" basi aliyekuwa anafuatia kwenye kura wakati wa uchaguzi Mkuu yaani wa pili aapishwe ili kuchukua nafasi iliyoachwa wazi...
Back
Top Bottom