Uchaguzi 2020 Vitisho kuelekea uchaguzi huu ni mkakati kama ile ya kurubuni Wapinzani wajitoe ili wapite bila kupingwa na vitisho lengo msishiriki wapite kiulaini

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
47,013
144,371
Ni kweli hatuna Tume Huru na bila shaka ni kweli kuna hujuma zinapangwa (naona hata Lema kagusia hili la hujuma kupitia Twitter) ila pamoja na yote haya, plan waliyonayo na wasioweka wazi ni kutumia vitisho ili wapinzani wakate tamaa ya kushiriki kabisa huu uchaguzi.

Faida ya Wapinzani kutoshiriki: itawaondolea usumbufu wa kukwaruzana nao na pia wataepuka kuonekana wanafanya hujuma katika huu uchaguzi hivyo wangependelea wapinzani hasa CHADEMA na ACT wasishiriki kabisa kwani tayari kuna vyama fulani vitashiriki kuhalalisha kinachoitwa uchaguzi wa vyama vingi.

Hivyo, mnavyoona fomu zao zinaongelea kugombea uongozi wa vyombo vya dola, mjue tu hilo halijatokea kwa bahati mbaya bali lengo ni kuwaogopesha kisha mtishike, muwe-demoralized na muame kujitoa au ili wao wapite kiulaini tena bila kulaumiwa kwa kuhujumu uchaguzi. Ninatarajia vitisho vitaendelea ili kuwakatisha tamaa.

Cha msingi si kabarasha la form za mgombea limebeba ujumbe gani, bali kinachotazamwa form zinahusu nini maana form ndio kila kitu, lile kabrasha halina uzito wowote hivyo vile vilikuwa ni vitisho tu na wanajua teyari tumejaa hofu hivyo wanatuoongezea kututisha zaidi.

Jambo lingine: huu ni mtego wa kisiasa wanatutega ili tujitoe alafu uchaguzi ukipita, watubeze mnalalamika nini wakati hamkushiriki kwenye uchaguzi (wataanza kutuita waoga, n.k).

Naamini hata wao hawapendi kuonekana wanatumia mabavu hivyo lazima watumie njia zote kuepusha haya yasitokee.

Kwahiyo, hivi vitisho ni Plan "A"ila tukivishinda, basi watakuja na Plan "B" ya miaka yote ingawa this time inaweza kuwa ni worse.

Hivyo, tupime wenyewe kipi bora kati ya kushiriki au kutoshoriki, na kama tunasusia,basi tuwe tumejipanga tunapanga kufanya nini.

Huu ndio mtazamo wangu.
 
Salary Slip,

Kuna nchi nyingi sana hapa duniani viongozi wake walijipanga tokea nje ya nchi na kwenda kuiangusha serikali,nadhani hata kagame alitokea bongo. Nitamshangaa Lissu Kama alikuwa amekaa tu Belgium bila mipango yoyote akitegemea tume inayoundwa na hawa walafi wanaCCM ndo wamtangaze kuwa rais.
 
Kuna nchi nyingi sana hapa duniani viongozi wake walikipanga tokea nje ya nchi na kwenda kuiangusha serikali, nadhani hata Kagame alitokea Bongo. Nitamshangaa Lissu Kama alikuwa amekaa tu Belgium bila mipango yoyote akitegemea tume inayoundwa undwa na hawa walafi wanaCCM ndo wamtangaze kuwa rais
Akili ya kitumwa
 
Back
Top Bottom