Ngongo
JF-Expert Member
- Sep 20, 2008
- 18,921
- 31,161
Heshima kwenu Ndugu wanajamvi,
Dalili zote zinaonyesha uchaguzi mkuu wa Rais,Wabunge na madiwani utafanyika October 2020.
Ni wazi yapo mambo mawili ambayo hayajakaa sawa.
Mosi ni Tume huru ya uchaguzi.Suala hili limekuwa likipigiwa debe na wadau mbali mbali wakiwemo wansiasa,viongozi wa dini na jumuiya ya kimataifa.Tumekuwa na uchaguzi mkuu tangu mwaka 1995 na tume hii ambayo sasa inalalamikiwa na wadau mbali mbali.Katika chaguzi zilizopita pamoja na ubovu wa tume lakini walionyesha uwanja sawa wasiasa.Chaguzi ndogo za marudio Tume ilipwaya sana na kuonyesha kiwango cha upendeleo ambao haupata kutokea tangu kuundwa kwa taifa leo.Tumeona wakurugenzi wakijificha wakati wapinzania wakirejesha au kuchukua fomu.
Ni wazi tena pasipo shaka uchaguzi mkuu wa October 2020 tutawaona wakurugenzi wakiwakimbia wapinzani katika level mbali mbali,tunshuhudia wapinzani walioshinda wakitangazwa wameshindwa,tutashuhudia wananchi wakiporwa haki za kuchagua kiongozi wanayemtaka,tutashuhudia vituko kuliko uchaguzi wa serekali za mitaa.
Uchaguzi mkuu 2020 utafanyika katika mazingira ambayo Dunia imekumbwa na ugonjwa wa CORONA sioni waangalizi wa uchaguzi wa kimataifa wakitia mguu Tanzania.Hii bahati mbaya la hasha wanajua ugonjwa wa CORONA ni tishio hawatakuwa tayari kuhatarisha maisha yao kwaajili ya uchaguzi wa Tanzania.
Mazingira haya ya uchaguzi 2020 October ni rafiki kwa chama kinachopenda kuiba kura,kukandamiza haki za wananchi wake kuchagua viongozi wanaowataka.Ni hakika uchaguzi huu wagombea wa CCM watasaidiwa na tume na vyombo vya dola.
Vyama vya upinzani sijui kama wamejiandaa kukabiliana na hujuma ambazo wakati huu zitakuwa kubwa kuliko kipindi kingine chochote katika uhai wao.Tumesikia kupitia viongozi wa upinzani John Mnyika kwamba mawakala hawatapewa fomu sijui wamejiandaa vipi kukabiliana na hicho kitisho.Kwasababu kama mgombea wa upinzania atashinda halafu akatangazwa mgombea wa CCM mkienda mahakamani mtatakiwa kuleta ushahidi sasa sijui mtepeleka vielelezo gani ?.
Nadhani badala ya vyama vya upinzani kukimbilia kututangazia idadi ya wagombea waliochukua fomu za kugombea uRais ni vyema wakapambana kisheria kwa kuipeleka tume na mwanasheria mkuu wa serekali Mahakamani na si kusubiri kushindwa halafu mkaja na maelezo yasiyokuwa na maana.Sijasikia Katibu Mkuu wa ACT au CDM wakiwaleza wapiga kura namna walivyojiandaa na uchaguzi huu wakati wanaelewa tayari yapo mazingira mabovu.