Dam55
JF-Expert Member
- Oct 8, 2015
- 5,592
- 11,831
Kwa kifupi kabisa ni kwamba tunakwenda kwenye Uchaguzi ambao mshindi tayari anajulikana. Ninasema haya kwasababu zifuatazo.
1. Kukubalika kwa Rais Magufuli kwa watanzania walio wengi (hili liko wazi na halina ubishi) Watanzania wanampenda sana huyu mtu na hawapo tayari aondoke Ikulu mapema.
2. Upinzani haujajiandaa kushika dola (hawako serious na uchaguzi) hawana hoja zenye mashiko hoja pekee iliyo baki ni Udikteta, wanafanya siasa kutegemea matutio ya ccm (kwakifupi wanayumbishwa na siasa za ccm) mfono mzuri ni jinsi wanavyojikita kwenye mgogoro wa Membe na ccm wenzake.
3. Siasa za uongo za upinzani na kutafuta huruma kwa wananchi kitu ambacho hakina msaada kwao mfano mzuri ni tukio la hivi karibuni la kusingizia serikali kumshambulia MH Mbowe, wakifanya makosa na kukamatwa kwa mujibu wa sheria basi hudai wameonewa au kutekwa ilhali wamakamatwa kwa mujibu wa sheria.
4. Hawana mgombea sahihi mwenye ushawishi mkubwa na anayekubalika na watanzania ambaye anaweza kumtikisa Magufuli, mfano mzuri ni Chadema walio tia nia wote si watu serious wa kwenda kupambana na Magufuli kuanzia Peter Msigwa hadi Tundu Lissu kwa akili tu yakawaida hawa watu niwachanga mno kwa Rais Magufuli.
5. Migogoro ndani ya vyama pinzani ambayo inawagawa wao wenyewe mfano mzuri ni wimbi kubwa la wabunge, madiwani na wanachama wengine wanaohama kutoka Chadema na CUF kwenda vyama vingine, mbaya zaidi badala ya vyama hivi kukaa kutathimini siasa za ndani za vyama vyao ili kufanya marekebisho badala yake wanakuja na tuhuma kuwa wanachama wao wananunuliwa.
Mwisho niseme tu kwamba mwaka huu tunakwenda tu kukamilisha matakwa ya kikatiba kumpa Rais Magufuli nafasi ya kutawala miaka mingine 5 lakini hatuwezi kusema kuwa ni uchaguzi wa ushindani, huu ndio ukweli hata kama utapingwa kwasababu ukweli mara nyingi huwa unaumiza.
Tujipange kwa uchaguzi wa 2025 panapo majaliwa ila kwa huu wa 2020 ccm wamesha shinda tayari wakuu, ila kwasababu siasa ni ajila, kipaji na ni sehemu ya maisha basi natuendelee tu kupiga porojo na kujifurahisha.