Uchaguzi 2020 Mtia nia Jecha na Hoja ya Mwigulu Nchemba juu ya Tume huru ya Uchaguzi Tanzania

Kinoamiguu

JF-Expert Member
Nov 29, 2018
10,526
13,013
Hapo juzi aliyekuwa waziri wa mambo ya ndani wa Tanzania shushu mbobezi, bwana Benard Camilius Membe alijitokeza kupitia mitandao ya kijamii akihoji juu ya uwepo wa tume huru ya uchaguzi. kauli ya Membe juu ya jambo hilo ilizua kelele nyingi miongoni mwa wahafidhina wa chama tawala ccm. kwao wao Tume ya uchaguzi ya Tanzania ni huru ati kwakuwa kuna wabunge wa vyama vya upinzani waliopatikana kupitia tume hii. hoja hii ni mufilisi na mfu itokayo vinywani mwa watu waliochoka kufikiria na kuvimbiwa madaraka. kwamba ati kwakuwa unalala kwenye nyumba hata kama ni mbovu usiseme hii ni aibu.

Mtu anayejiita kama kweli ana PhD na ambaye pia ni waziri wa sharia na mambo ya katiba akajitokeza tena kwa kufoka kama ilivyokawaida yake (alishawahi kuchana bajeti ya upinzani bungeni) kwamba Membe anapotosha na kwamba hana haki ya kudai katiba mpya kwa sasa tu kwakuwa naye alikuwepo serikalini na hakuidai akiwa humo.

Hapo majuzi huko Unguja kimejitokeza kiroja cha mwaka, ni pale ambapo aliyekuwa mwenyekiti wa Tume ya uchaguzi ya huko alipojitokeza hadharani na kuchukua fomu ya kuwania uraisi wa Unguja. Ni Jecha ndiye aliyewanyima Wazanzibar haki ya kuongozwa na raisi waliyemchagua wao, pale alipoufuta bila sababu uchaguzi mkuu wa huko hapo 2015. Refa kaingia mwenyewe. Uchukuaji wa fomu wa Jecha ni kiashiria kwamba alsimamia uchaguzi ule akipendelea chama chake .

Mwigulu anajua hakuna mtu Neutral kwa asilimia zote lakini inapofikia kada wa chama kusimamia uchaguzi ni dhahir kwamba haki itasiginwa kwa wengine Kuwajibu wanaodai tume huru ya uchaguzi kwamba wametumwa na MABEBERU/WABIA/WAHISANI/WAFADHIRI wa maendeleo ni kufirisika kimawazo, fikra na mtazamo kama alivyo mwigulu. sitashangaa siku akisema Magufuli ni malaika hivyo aongozwe muda. Malaika gani asiye na huruma kwa watu wake. Tunakumbuka bado kauli zile za kifedhuli kwa wahanga wa tetemeko la Bukoba, huyo malaika wa wapi asiye na huruma.

Sasa Jecha kajitokeza kuchukua fomu sema tena uchaguzi wa Zanzibar 2015 ulikuwa huru na wa haki. hii haihitaji PhD za kuandikiana kujua ukweli wake. Tunamtaka Nchemba aheshimu mawazo ya Membe kwakuwa mtu kutoa mawazo yake si dhambi ati kwakuwa alikuwepo ndani ya serikali. Hata huyo Nyerere alishawahi kukosoa baadhi ya mambo aliyoyafanya akiwa ikulu ndiyo tuseme nae alitumwa na MABEBERU?

Mkapa kwenye kitabu chake alikili namna alivyokandamiza haki za watu huko Pemba 2001 pale walipoandamana kupinga matendo haramu ya kina Jecha na kundi lake tuseme nae anatumiwa na Mabeberu?

Tunamtaka bwana Nchemba atambue kwamba watu kuhoji kama alivyofanya Membe sio kosa hata kidogo ndiyo afya kwa uahi wa taifa japo wanasema wanataka kuleta vurugu. upuuzi tu.

Nimalizie kwa kuwapongeza watu wa MALAWI kwa kusimamia haki hata uchaguzi kurudiwa. MSITUTENGENEZEE TAIFA LINALOTEGEMEA FIKRA ZA KUHANI MMOJA SISI NI VIUMBE HAI WENYE UTASHI NA FIKRA HURU.

Kazi njema corona haishi kwa vitisho wala data za kupika.
 
Membe anadhani kikwete atamsaidia kwenye hili hajui anguko lake lilishatimia
 
Pamoja na kuwa Jecha anahaki kikatiba kutia nia na kuchukua fomu ya kugombea uchaguzi wa aina yoyote hapa nchini ikiwemo Zanzibar, kimaadili hiyo ni dosari

Kwa mtu anyejiheshimu na kuheshimu nafasi aliyowahi kuitumikia alikua na wajibu wa kimaadili( moral responsibility) wa kujiweka mbali na nafasi za kugombea kupitia vyama vya siasa
 
Membe anadhani kikwete atamsaidia kwenye hili hajui anguko lake lilishatimia
asaidiwe au asisidiwe amesema ukweli. mnasumbuliwa na unafiki. chuki na majungu ndo maana Mnawekeana Sumu
 
Membe anadhani kikwete atamsaidia kwenye hili hajui anguko lake lilishatimia
Nina uhakika Membe anaelewa kua hawezi kuchukua fomu au hata akichukua hawezi kufika popote kwenye mchakato wa ndani wa CCM hata kama asingekua na "mgogoro" na chama chake

Ukitafakari kauli zake, vitendo vyake na ukimsoma kati ya mistari utaona anaongea kitu ambacho bado hajakisema au hajakiweka wazi. Kuna ujumbe mzito na maalum anajaribu kuufikisha kwa umma na hasa kwa wahusika. Tafakari utajua kua ambacho hajakisema kwa uwazi ndio ujumbe aliokusudia, na kuna kila dalili hata kama haukubaliki lakini umewafikia walengwa wote
 
Back
Top Bottom