uchaguzi

Uchaguzi Tanzania
Uchaguzi hasa wa viongozi katika nchi ni utaratibu (mchakato) rasmi unaoendeshwa kwa mujibu wa sheria kuwawezesha wananchi kufanya maamuzi kwa njia ya kuwapigia kura kuwachagua watu ambao wanawataka kuwaongoza kwa kipindi maalum.

Uchaguzi ni utaratibu wa kawaida wa demokrasia wa kuwapata wawakilishi wa kisiasa ambao umekuwa ukitumika tangu karne ya 17. Kuna aina tatu za msingi za uchaguzi zinazotumiwa kuwapata viongozi kulingana na mfumo unaotumiwa na nchi husika.

Aina hizo ni uchaguzi wa Rais, Uchaguzi wa Wabunge na Wawakilishi katika Baraza la Kutunga Sheria na Uchaguzi wa Viongozi wa Serikali za Mitaa.

Vyama vya Siasa kwa upande wao navyo huendesha chaguzi ambazo zinajulikana kwa jina la “Chaguzi wa Msingi” zinazotumika kuwachagua wateuliwa wa vyama katika aina za uchaguzi ambazo zimetajwa hapo juu.

Endapo Tume haitaridhika kabla ya kutangaza matokeo ya uchaguzi kwamba kulikuwa na kutokufuatwa kwa taratibu, matumizi mabaya au ukiukwaji wa taratibu za uchaguzi au pale ambapo kura za wagombea waliopata kura za juu imelingana, Tume itasimamisha au kufuta uchaguzi au sehemu yoyote ya uchaguzi na itatangaza siku nyengine ya kurudiwa kwa uchaguzi huo.
  1. G Sam

    Hivi utajisikiaje mbunge umehamia CCM halafu unaenda kukataliwa na wanaccm kwenye kura za maoni? Angalizo: mtatukanwa sana na wapinzani wenu chamani!

    Mbunge umehamia CCM tena unawatukana waliokupa ridhaa ya chama kugombea. Unatukana sana huku unajisahau kuwa unaenda kugombea ubunge kwa tiketi ya chama ambacho umehamia juzi. Chama ambacho unaenda kukutana na magwiji ha propaganda chafu yaliyojipanga tangia 2016. Nawaambieni mtapata tabu sana...
  2. YEHODAYA

    Patana na mgomvi wako kabla safari CHADEMA wanafanya kosa la Lowassa wanaingia uchaguzi wakiwa na ugomvi na Serikali,vyombo vya dola,mahakama na Tume

    Kuna usemi mmoja kwenye Biblia unasema Mathayo 5:23-24 “Basi, ukipeleka sadaka yako mbele ya madhabahu na hapo ukakumbuka kwamba ndugu yako ana ugomvi nawe, iache sadaka yako mbele ya madhabahu, nenda kwanza ukapatane na ndugu yako, ndipo urudi utoe sadaka yako." Lowasa aliendekeza ugomvi na...
  3. E

    Mambo haya yatakipa ushindi mkubwa CCM na yanaweza kupoteza wabunge wengi wa upinzani kwa kuzingatia muda uliobaki kufanya uchaguzi

    Mambo yafuatayo CCM ikijipanga vizuri itashinda kwa kishindo .... 1. Kitendo cha Tundu Lissu kwenda kuichafua nchi kwa wazungu. 2. Kitendo cha Zitto Kabwe kutaka nchi isipewe mkopo wa elimu na WB, na baadaye nchi kukopeshwa 3. Kitendo cha wapinzani kupinga kila kitu 4. Kitendo cha...
  4. J

    Kuelekea uchaguzi mkuu, Ngeleja " amkumbatia" Haji Manara Bungeni

    Wakati akichangia hotuba ya bajeti mbunge wa Sengerema mh Ngeleja ametumia muda mwingi kumsifia afisa habari wa Simba Haji Manara. Ngeleja amedai kuwa Manara ni mtu makini ambaye uwepo wake klabuni umeifanya Club ya Simba ing'ae na siyo haki kuelezea mafanikio ya serikali ya awamu ya 5 bila ya...
  5. FRANC THE GREAT

    Hizi kauli za Joe Biden kuelekea uchaguzi wa Novemba zinaashiria kitu gani?

    Habari! Awali ya yote, natumai mu wazima wa afya. Nimemsikia Joe Biden akisema kuwa ana wasiwasi kwamba rais Donald Trump "atajaribu kufanya wizi" katika uchaguzi ujao wa rais wa mwezi Novemba mwaka huu. Joe Biden hakuishia hapo tu bali amedai kuwa anaamini Jeshi litalazimika kumuondoa kwa...
  6. J

    GE2020 RC Makonda: Viongozi wa dini ombeeni uchaguzi ili tupate viongozi Watakatifu wa kumsaidia Rais Magufuli na watoa kafara wasifurukute

    Mkuu wa mkoa wa Dsm mh Makonda amefanya kikao na viongozi wa dini kupitia jukwaa lao la Kamati ya maridhiano. Makonda amewataka viongozi hao wa dini kuuombea uchaguzi mkuu ili wakapatikane viongozi watakatifu watakaomsaidia Rais Magufuli katika awamu yake ya pili ya uongozi. Makonda amesema...
  7. chiembe

    GE2020 Ni mambo yapi unaiambia serikali ya CCM "we can't breathe" ili CCM iondoe goti katika shingo za Watanzania, ili yawe ajenda ya uchaguzi?

    "I can't breath" ni kauli aliyoitoa George Floyd wakati askari mmoja huko marekani alipomkamata na askari huyo kuweka goti lake katika shingo ya George Floyd, jambo lililosababisha akose hewa kisha kufariki. Naipa kauli hiyo muktadha wa kitanzania kisiasa. Ni mambo gani ambayo yanafanya...
  8. RAKI BIG

    Bila tume huru hakuna uchaguzi huru

    (Hotuba ya Mwenyekiti wa ACT Wazalendo Ndugu Maalim Seif Sharif Hamad,Mwenyekiti wa Chama Taifa Kuhusu Masuala ya Msingi Kuelekea Uchaguzi Mkuu 2020) Ndugu Watanzania, Kama inavyofahamika, 2020 ni mwaka wa Uchaguzi Mkuu. Tanzania inatarajiwa kufanya uchaguzi wa madiwani, wabunge, wawakilishi na...
  9. S

    GE2020 Kabla ya Uchaguzi Mkuu wa baadae mwaka huu, Mungu atatufuta machozi wapinzani kwa kuangusha mbuyu

    Maandiko matakatifu yanasema "anaeua kwa upanga,atakufa kwa upanga" na Waswahili wanasema "Mungu si Athumani".Pia kuna msemo:" Mungu hadhihakiwi." Kwa kuzingatia misemo hiyo na kwa kuzingatia machozi,machungu na kilio cha watu wake,Mungu atajibu kadri atavyyona inafaa na anaweza kujibu kwa...
  10. Mzee Koyu Mbochi

    Kuelekea Uchaguzi Mkuu: Rais Magufuli amecheza kama Messi

    Salaam wanajamvi, Itakumbukwa kwamba ujio wa COVID-19 umekuwa ni mtihani mkubwa kwa marais wa mataifa mbalimbali hususani yanayotegemewa kufanya uchaguzi mwaka huu na mwaka ujao. Corona imekuwa ni moja ya mitihani mikubwa mwaka huu. Niende moja kwa moja nchini (Tanzania), Corona ilipoanza...
  11. mkiluvya

    GE2020 CHAUMMA kushiriki Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba 2020

    Chama cha Upinzani cha CHAUMMA, kimetangaza rasmi kushiriki Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba mwaka huu. Mwenyekiti wake, Hashim Rungwe Spunda amesema wanavikaribisha vyama vingine kuungana nao wakati ambao CHAUMMA inaelekekea kuchukua dola. Rungwe amesema, hivi karibuni Chaumma itatoa...
  12. S

    GE2020 Wapinzani msimuamini sana Membe kwa yoyote atakayosema na kuyatenda kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu baadae mwaka huu

    Mwanasiasa ambae anaweza kujiamini kusema na kufanya lolote kwa lengo la kukosoa watawala waliopo madarakani bila hofu ya kushitakiwa,mali zake kutaifishwa au kunyang'anywa,n.k ni yule tu ambae wakati alipokuwa kwenye system, hakuwahi kutuhumiwa kufanya ufisadi,wizi,kujihusisha na...
  13. FRANC THE GREAT

    Joe Biden ashinda rasmi uteuzi wa Chama cha Democratic kugombea nafasi ya urais nchini Marekani

    Joe Biden ameshinda rasmi uteuzi wa Chama cha Democratic kumkabili rais Donald Trump katika kinyang'anyiro cha uchaguzi wa rais utakaofanyika panapo mwezi Novemba mwaka huu. Biden amesema katika ukurasa wake wa Twitter kwamba amefanikisha kujikusanyia wajumbe 1,991 wanaohitajika ili kupitishwa...
  14. ubongokid

    GE2020 Siasa za uchaguzi na fursa kwa wajasiriamali

    Habari za wakati huu, Kwanza nianze kwa kuwapa pole wale ambao katika kipindi hiki cha COVID wamejikuta katika wakati mgumu kwa sababu moja ama nyingine katika biashara zao na maisha kwa ujumla na kwa wale ambao wameifariki dunia katika kipindi hiki wapumzike kwa amani. Nirudi kwenye mada kwa...
  15. Allen Kilewella

    GE2020 Kusipokuwa na uchaguzi wa kuchagua Rais kuna haja ya kufanya uchaguzi?

    Wana CCM wengi sana wanatamani kwa mtizamo wao ghushi na uliojaa ugoto katika kufikiri, kuwa John Magufuli asipingwe na mgombea toka CHADEMA. Wao wanadai kwa aliyoyafanya Magufuli kama Rais wa Tanzania hakuna haja ya kupingwa. Lakini najiuliza kama Magufuli wanataka apite bila ya kupingwa, je...
  16. Roving Journalist

    Rais Magufuli afungua mkutano Mkuu wa Chama cha Waalimu, Corona imeisha, Shule za Msingi kufunguliwa karibuni

    Salaam Wakuu, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, Leo anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika Mkutano Mkuu wa Uchaguzi wa Chama Cha Walimu Tanzania-CWT. Mkutano huo utafanyika katika Uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma, huku watu wote wakitakiwa kuzingatia na kuchukua...
  17. Mzalendo2015

    GE2020 Rais Magufuli lipa Mafao ya Wastaafu kabla ya Uchaguzi Oktoba 2020

    Kulingana na report ya Ukaguzi ya CAG 2019/20 Serikali inadaiwa na Mifuko ya Jamii PSSSF kiasi cha zaidi ya Tshs. 700 Bilioni ambazo Serikali imekopa toka PSSSF na haijarudisha/kulipa fedha hizo. Kuna Habari za kuaminika kwamba fedha hiyo imekopwa kwenda kujengea miradi mikubwa ya Serikali...
  18. M

    GE2020 Ilani ya Uchaguzi inayofaa 2020 ni ile itakayochochea Ukuaji wa Uchumi kwa wote

    Ilani ya uchaguzi itakayochochea ukuaji wa uchumi kwa wote na kuongezea serikali kodi ndio inafaa. Vyama vya Siasa inatakiwa vije na Ilani na Mipango ambayo inampa Mtanzania Uhuru wa kuchagua ni wakati gani wa kuajiriwa na ni wakati gani wa kujiajiri. Ilani ipange kuondoa vipingamizi kwa...
  19. Q

    CCM imezindua kituo cha kutoa taarifa za wala rushwa wakati wa uchaguzi. Hawaiamini TAKUKURU?

    Katibu wa Halmashauri Kuu Itikadi na Uenezi, Humphrey Polepole amesema kwamba Chama Cha Mapinduzi kimezindua kituo maalum cha wananchi kutoa taarifa za Uchaguzi kimaadili ili kuwabaini wala na watoa Rushwa, kuelekea Uchaguzi Mkuu Oktoba 2020.
  20. YEHODAYA

    Vyama vya upinzani, uchaguzi huu ungeni mkono mgombea urais wa CCM hamna mgombea wa maana wa kushinda kwenu

    Vyama vya upinzani havina mgombea yeyote wa maana wa kushinda uchaguzi wa urais kupitia vyama vyao sababu vyote kwanza havina nguvu pande zote za muungano. Chadema ina nguvu Tanzania bara tu mkoa wa Kilimanjaro tu kidogo mji wa Arusha upande wa Zanzibar hamna kitu. Hivyo akiwekwa mgombea uraisi...
Back
Top Bottom