Uchaguzi 2020 Malengo ya vyama uchaguzi mkuu 2020

Oct 7, 2019
51
156
Kila chama kina malengo yake kwenye uchaguzi huu.

1. ACT Wazalendo Lengo lao kubwa ni kugawana majimbo na CCM Zanzibar. Hili asilimia za kufanikiwa ni asilimia 60% PLUS. Siasa za Zanzibar zilikuwa Ni za CCM VS CUF lakini CUF hii iwe chini ya Maalim Seif. Kwa hiyo Mambo yanavyooneka Ni kuwa CUF inaenda kufutika Zanzibar na ACT wanaenda kuchukua nafasi ya CUF. Hili ndio Jambo kubwa kabisa ambalo wanaweza kulivuna 2020. Kusema wanataka kuiongoza dola ni kujitapa tu Hakuna maana kwenye hesabu zao.

2. CCM wao kwenye uchaguzi huu malengo yao makubwa ni kuunda Serikali zote mbili ya Jamhuri Ya Muungano na ile ya Mapinduzi ya Zanzibar. Hili kwao sio kazi kubwa Sana wana kila kitu cha kufanikisha hili. Lakini Wana lengo ya Pili ambayo kwa jicho la kawaida halionekani hili Lengo, lengo lenyewe Ni kuhakikisha wanakichakaza Chama Cha Chadema nje-ndani yaani Bora hata CUF ishinde mahali kuliko Chadema.

3. Chadema wao Lengo lao ni kuiondoa CCM Madarakani, lengo hili ni gumu kweli hivyo walipaswa kuwa na Option zaidi ya Moja. Ninavyowaona wanakwenda kwenye uchaguzi na Option Moja tu kuiondoa CCM, Ningelikuwa ndani CHADEMA ningeshauri kuwepo na Option ya Pili Kama tusipofanikiwa Lengo hili tuwe na lengo lingine angalau kutetea majimbo yote ambayo walikuwa nayo Hadi bunge kuvunjwa. Kuna Kosa Moja kubwa la Kiufundi limefanyika kwa miaka mitano wameshindwa kabisa ku reconcile na vyama vingine na Serikali. Kulikuwa na Dalili palebowe alipopewa nafasi ya kuhutubia pale Mwanza sijui kilitokea nn Tena yale mahusiano hayakuendelea Kati ya CHADEMA na Serikali. NADHANI HAPA MNANIELEWA.... Kufanya reconciliation ni kufanya makubaliano ya kuachiana baadhi ya Mambo. Chadema ndio chama pekee wanaoingia kwenye uchaguzi mkuu wakiwa na Hali ngumu zaidi.

4. NCCR Mageuzi wao wanaingia kwenye uchaguzi wakiwa na hesabu Kali, wao kidogo walifanya reconciliation na Serikali kwa maana ya kutafuta angle yoyote ya kujificha angalau majimbo matano Hadi kumi, wanajua wakiongezea Hapo na Viti maalumu watasogea. Lengo lao jingine Ni kujaribu kuweka watu kwenye Ubunge wa Africa Mashariki. Kwa tabia waliyoionyesha mwishoni mwishoni mwa Serikali ya awamu ya Tano hapa wanaweza kupata angalau wabunge wawili au watatu. Hesabu zao kwa kuanzia zinagomea hapa. Tatizo lao kubwa Ni kuwa majimbo gani wanaweza kudokoa angalau washinde? Hili ni la kusubiri na kufuatilia.

5. CUF wao jahazi limepoteza mwelekeo, wao hawajui wasimamie wapi, malengo yao walitamani Sana wabakie na wabunge waliowapata kwenye Ukawa. Lakini haiwezekani Tena kwa kuwa wamepoteza Rasilimali watu ambao walikuwa ni Taswira ya chama. Walioibomoa zaidi Cuf Ni wao wenyewe ACT imekuja kuzika tu lakini haihusiki. Naweza kusema mpaka Sasa lengo lao kwenye uchaguzi huu halipo Measurable Wala Specific.

6. TLP kupitia Mwenyekiti wao Wana Malengo makuu mawili. Moja na la Muhimu Ni Jimbo la Vunjo, yaani Mrema yeye pamoja na kumuunga JPM na Kumfanya awe Mgombea wao Ni kutaka JPM amuunge mkono kwenye Jimbo hili. Vurugu za chama hiki kuipenda CCM zimezidi baada ya Mahusiano mazuri Kati ya Mbatia na JPM. ANACHOKIFANYA Mrema Ni kutaka kuimba pambio la juu zaidi kuliko Mbatia ili aungwe mkono hapa. Katika hili Ni kama ndoa ya Mke Mwenza kila mmoja anataka kumteka mume kwa maneno mazuri. Lengo la Pili la Mrema ni kutaka kubakia kwenye nafasi yake ya Bodi ya Parole. Malengo ya TLP si ya Wanachama wote Bali ni ya Mwenyekiti peke yake, yakikamilika maslahi yake Mambo yanakuwa safi. Wale wanachama ni Kama wanafamilia anachokipata Mrema ndicho anachowagawia kwenye Payroll yake.

7. Vyama vingine vilivyobakia malengo yao Ni kuendelea kutabasamu mbele ya Mwenyekiti wa CCM ili akishinda waalikwe kwenye Sherehe za kuapishwa.
 
Back
Top Bottom