Uchaguzi 2020 Tathmini: Hali ya siasa nchini kuelekea uchaguzi mkuu 2020

brazaj

JF-Expert Member
Jul 26, 2016
27,824
35,827
Kuelekeaa uchaguzi mkuu 2020, kama mtanzania wa leo, nimekuwa pia nikifuatilia harakati hizi na kwa nionavyo huu hapa ndiyo ulio ukweli mchungu:

Pana watu wamejivika kuwa washauri wa upande wa upinzani kuwaasa hatari kuhusu uwezekano wa kwenda na Membe.

Ukiangalia ushauri wao na maonyo yao unakuta vinaungwa mkono vilivyo na wale wa ule upande wa kijani.

Sasa kama upande wa kijani unawataka upinzani kuwa macho na Membe ili waweze kushinda uchaguzi hii sasa si ndiyo kichekesho chenyewe?

Yaani kuwa lini mamba mla watu akatoa ushauri ulio bora kabisa kwa mvuka mto ili kumwezesha kuvuka salama ambapo yeye njaa imemkaba vilivyo? Haya kama siyo maajabu ya Mussa, maajabu ya Mussa yatakuwa yapi sasa?

Kwa Upande wa Zanzibar nako. Pana wagombea kibao hasa kwa wana kijani. Anatakikana mgombea mmoja ambaye ameonyesha kwa vitendo kuwa anayaweka maslahi ya chama chake na ya taifa mbele.

Kumekuwa na shutuma toka kwa kigogo mmoja toka huko kijani kuwa, pana baadhi ya wagombea huko kijani wanaotumiwa na mabeberu.

Sasa mtu unajiuliza kama tashwishi za mabeberu zipo, na kama anayetakikana ni mwenye maslahi ya taifa na chama chake, kwa nini asipewe Jecha?

Kwani kuna Mzalendo zaidi ya Jecha? Kwa hakika si jiwe wala yeyote katika kijani mwenye kulinda maslahi ya chama chake wala taifa ki kijani kijani kuliko mheshimiwa Jecha!

Sasa tena kama ukweli huu wa wazi haonekani kwa wagombea au hata viongozi, sasa tena haya si ndiyo yatakuwa maajabu ya Mussa?

Hizi jitihada za wazi za kujaribu kuliita beleshi ni kijiko, zinatulazimu hata tusiopenda agenda agenda hizi za siasa kuziona offside hizi za wazi.

Wajameni, nchi hii ni yetu sote.

Kwanini isiwe haki bin haki kwa kila mmoja na hata kila chama?
 
Wamakonde wa kusini wanasema; "ni ngumu kumeja."
 
Hoja zijibiwe kwa hoja

Zingine ngumu kumeja mkuu.

Janja janja nyingi. Usoni kama watu kumbe utu uliwatoka kitambo. Haki bin haki kwao ni jambo lisilokuwapo.

Mnyonge na anyongwe walakini haki yake apewe.
 
Back
Top Bottom