Uchaguzi 2020 Ushauri: Wapinzani, mikakati yenu yote kuhusu uchaguzi ikiwemo kusimamisha mgombea mmoja, msiifanye kwa njia ya simu

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
47,014
144,372
Kutokana na maongezi ya vigogo wa chama fulani kuvujishwa mitandaoni kwa siku za karibuni huku wahusika wakipeta utadhani hawajavunja sheria, nawashauri sana kuepuka kujadili mipango yenu yoyote inayohusu uchaguzi kwa njia ya simu kwani inaweza kuvujishwa kwa lengo la kutoa siri zenu na hata kuwachonganisha kama sio kuwavuruga.

Mawasiliano ya simu myatumie kuwasiliana kwa lengo la kupanga mkutane wapi,iwe lini,n.k lakini sio kujadili wala kushauriana mumsimamishe nani, mshirikiane vipi, mumuchague nani, n.k.

Na muwe makini sana hasa mnapowasiliana na Lissu alieko nje na kama kuna issue sensitive na inayoweza kusubiri arudi, basi ni vizuri mkasubiri atakaporudi ndio mumushirikishe lakini sio kufanya hivyo kwa njia ya simu. Tusiishe kwa mazoea, zama zimabadilika.

Kwa sasa inawezekana mkawa mnafuatiliwa kuliko wakati mwingine wowote ule, hivyo ni bora muwe makini na mnayoyaongea kupitia simu zenu.

Ni ushauri tu kwa nia njema.
 
Huwezi kufanya chochote bila mawasiliano ya simu katika zama hizi, labda kama unafikiria kufanya mawasiliano through a third party. Lakini kama ni siri ubakinayo moyoni maana ukimwambia mtu moja tu sio siri tena.
 
Back
Top Bottom