Uchaguzi 2020 Askofu Gwajima atangaza nia ya kugombea ubunge jimbo la Kawe

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Jun 12, 2012
4,572
26,843
Gwaji.JPG

Gwajima.jpg

Askofu Josephat Gwajima ametangaza nia ya kugombea ubunge Jimbo la Kawe kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) na leo amefika kwenye ofisi za chama hicho kupewa utaratibu.

Kuhusu kuunga mkono UKAWA mwaka 2015, amesema hajawahi kuwa Mwanachama wa CHADEMA, ila hutetea haki wakati wote.

===
Aliingia Ofisi ya CCM Wilaya ya Kinondoni

Amesema alikwenda pale baada ya kumsikia Rais na Katibu mkuu wa CCM aliyetangaza kuwa wale wenye nia ya kumsaidi Rais achukue fomu, na yeye ameona aweze kwenda ofisini kujua utaratibu wa kugombea

Amesema inaweza kuwa mtu mchungaji haimzuii kuwa mbunge kwa kuwa wako viongozi wa dini ambao pia ni viongozi kisiasa, amesema hajawahi kuwa mwananchama wa chadema

Amesema amekuwa mwanachama wa CCM tangu mwaka 1994, aliipata katika mkoa wa Mwanza, Wilaya ya Misungwi, kata ya Buhingo kijiji cha Kabale na alipewa kadi na mzee Kasmiriki Futumo, alikuwa ni mwenyekiti wa ccm ambaye katibu wake alikuwa Leoneidas Masungwa

Kadi yake amesha-upgrade kuingia mfumo mpya, amesisitiza hajawahi kuwa mwanachama wa CHADEMA, ila anapenda kutetea haki na tatatetea haki siku zote. Amesema anatetea haki sehemu yoyote, iwe CCM au kokote pale atatetea haki

Hajasema kitu ambacho anaweza kwenda kuwafanyia watu wa Kawe. Aidha ilionekana kuwa angeweza kugombea Misungwi, lakini amesema Misungwi ni sehemu aliyozaliwa lakini maisha yake yamekuwa Kawe kwa hiyo atagombea Kawe

 

HaMachiach

JF-Expert Member
Dec 15, 2015
3,193
5,531
Askofu Josephat Gwajima ametangaza nia ya kugombea ubunge Jimbo la Kawe kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) na leo amefika kwenye ofisi za chama hicho kupewa utaratibu. Kuhusu kuunga mkono UKAWA mwaka 2015, amesema hajawahi kuwa mwanachama wa CHADEMA, ila hutetea haki wakati wote.
Nampa hongera Sana kile Ni kichwa chenye akili kubwa sana yani na naamini atashinda yani ngoja tusubiri mchakato
 

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
63,804
96,415
Askofu Josephat Gwajima ametangaza nia ya kugombea ubunge Jimbo la Kawe kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) na leo amefika kwenye ofisi za chama hicho kupewa utaratibu. Kuhusu kuunga mkono UKAWA mwaka 2015, amesema hajawahi kuwa mwanachama wa CHADEMA, ila hutetea haki wakati wote.
Ni jambo jema... Halima aanze kufungasha virago!
 
18 Reactions
Reply
Top Bottom