UCHAMBUZI: Anguko kubwa kwa watu wote maarufu wanaodandia siasa za CCM wakati wa uchaguzi

Zanzibar-ASP

JF-Expert Member
Nov 28, 2013
10,129
35,143
Mwaka huu wa 2020 kuna uchaguzi mkuu, kumekuwa na heka heka kila kona ya nchi, katika vyama mbali mbali watu wakipigana vikumbo kuomba kugombea nafasi mbali mbali, hususani viti vya ubunge. Kwa leo hapa nitajikita kuchambua heka heka hizo kwa nafasi ya ubunge hasa kwa chama cha mapinduzi (CCM).

Watu wameona ubunge ni kama gulio la mnada, kila mtu anayejihisi anajulikana kijamii (Prominent Person, Public figure, Social Popular etc) kichwa kichwa, anavaa shati la kijani na kujitumbukiza kwenye kinyang'anyiro cha ubunge ndani ya CCM. Bahati mbaya sana, tena sana, wengi wao hawajui hata misingi muhimu ya kucheza katika siasa za kiCCM, hivyo kirahisi sana wataishia kuangukia pua, aibu, kuchafuliwa, kupoteza muda na pesa nk.

Kwa kifupi sana, mgombea nafasi ya ubunge ndani ya CCM anapatikana kwa kuunganisha mambo haya:

1. Nguvu ya kisiasa uliyonayo ndani ya wajumbe wa CCM katika eneo husika.
Hapo sahau umaarufu wako wote ulionao katika jamii, embu jiulize, ni kwa kiasi gani umeweza kushiriki na kushinda katika harakati za ndani kwa ndani katika CCM kwa hilo jimbo hapo kabla. Na hapo ndio ule msemo wa CCM ina wenyewe unapojidhihirisha. (Katika hili ninawahurumia sana watu kama Gwajma, Master J, Steve Nyerere, Professor Kitila Mkumbo, Waitara, Mollel na makapi wengine wote waliorejea CCM nk. Hakuna atakavuka hicho kigingi)

2. Siasa za sarakasi, fitna na zengwe. Huo ni mkondo wa machafuko, kuna hadi vitisho vya kulogana. Kama hujui kucheza hizo siasa, kamwe usijaribu kuchukua fomu. CCM ni mabingwa wa hizo siasa. Ukisikia siasa ni mchezo mchafu, basi huenda udhihirisho uko hapo.

3. Pesa za kutosha kuweza kuendesha harakati. Hapo ni mwendo wa Rushwa na Takrima.
Mkono mtupu haulambwi, na ukiwa na mkono mfupi, utaishia kuvaa manguo ya kijani tu, kiti cha ubunge utakisikia tu. Huwezi kuzitenganisha siasa za CCM na matumzi holela ya kugawa pesa kwa lengo la kununua cheo. Huo ndio utamaduni wake. (Katika hili nina wahurumia sana wasomi na matumishi kadhaa wa umma ikiwemo madaktari, wahandisi ambao wamejitumbukiza huko kugombea wakati mifukoni wamechacha, hakuna atakayetoboa!)

4. Siasa za kisultani. Hapo ninamaanisha, wewe kama mgombea unapaswa kuwa na Connection ya hali ya juu na wakuu wa chama wenye maamuzi ya kuchuja na kupitisha wagombea. Mfano rahisi ni wewe kuwa mtoto wa mkubwa, hawara wa mkubwa, mkwe wa mkubwa, rafiki wa karibu wa mkubwa, mwanamkakati wa karibu wa mkubwa fulani nk.
 
Mwaka huu wa 2020 kuna uchaguzi mkuu, kumekuwa na heka heka kila kona ya nchi, katika vyama mbali mbali watu wakipigana vikumbo kuomba kugombea nafasi mbali mbali, hususani viti vya ubunge. Kwa leo hapa nitajikita kuchambua heka heka hizo kwa nafasi ya ubunge hasa kwa chama cha mapinduzi (CCM).

Watu wameona ubunge ni kama gulio la mnada, kila mtu anayejihisi anajulikana kijamii (Prominent Person, Public figure, Social Popular etc) kichwa kichwa, anavaa shati la kijani na kujitumbukiza kwenye kinyang'anyiro cha ubunge ndani ya CCM. Bahati mbaya sana, tena sana, wengi wao hawajui hata misingi muhimu ya kucheza katika siasa za kiCCM, hivyo kirahisi sana wataishia kuangukia pua, aibu, kuchafuliwa, kupoteza muda na pesa nk.

Kwa kifupi sana, mgombea nafasi ya ubunge ndani ya CCM anapatikana kwa kuunganisha mambo haya:

1. Nguvu ya kisiasa uliyonayo ndani ya wajumbe wa CCM katika eneo husika.
Hapo sahau umaarufu wako wote ulionao katika jamii, embu jiulize, ni kwa kiasi gani umeweza kushiriki na kushinda katika harakati za ndani kwa ndani katika CCM kwa hilo jimbo hapo kabla. Na hapo ndio ule msemo wa CCM ina wenyewe unapojidhihirisha. (Katika hili ninawahurumia sana watu kama Gwajma, Master J, Steve Nyerere, Professor Kitila Mkumbo, Waitara, Mollel na makapi wengine wote waliorejea CCM nk. Hakuna atakavuka hicho kigingi)

2. Siasa za sarakasi, fitna na zengwe. Huo ni mkondo wa machafuko, kuna hadi vitisho vya kulogana. Kama hujui kucheza hizo siasa, kamwe usijaribu kuchukua fomu. CCM ni mabingwa wa hizo siasa. Ukisikia siasa ni mchezo mchafu, basi huenda udhihirisho uko hapo.

3. Pesa za kutosha kuweza kuendesha harakati. Hapo ni mwendo wa Rushwa na Takrima. Mkono mtupu haulambwi, na ukiwa na mkono mfupi, utaishia kuvaa manguo ya kijani tu, kiti cha ubunge utakisikia tu. Huwezi kuzitenganisha siasa za CCM na matumzi holela ya kugawa pesa kwa lengo la kununua cheo. Huo ndio utamaduni wake. (Katika hili nina wahurumia sana wasomi na matumishi kadhaa wa umma ikiwemo madaktari, wahandisi ambao wamejitumbukiza huko kugombea wakati mifukoni wamechacha, hakuna atakayetoboa!)

4. Siasa za kisultani. Hapo ninamaanisha, wewe kama mgombea unapaswa kuwa na Connection ya hali ya juu na wakuu wa chama wenye maamuzi ya kuchuja na kupitisha wagombea. Mfano rahisi ni wewe kuwa mtoto wa mkubwa, hawara wa mkubwa, mkwe wa mkubwa, rafiki wa karibu wa mkubwa, mwanamkakati wa karibu wa mkubwa fulani nk.
Hii post yako Haina mashiko kajipange upya
 
Ngoja tutaona kwa hawa waliohama vyama vyao kuunga mkono juhudi kama watakumbana na hayo.
 
Unaweza kuvuka vigingi vyote hivyo lakini ukakatwa pale Dodoma.
 
Back
Top Bottom