uchaguzi

Uchaguzi Tanzania
Uchaguzi hasa wa viongozi katika nchi ni utaratibu (mchakato) rasmi unaoendeshwa kwa mujibu wa sheria kuwawezesha wananchi kufanya maamuzi kwa njia ya kuwapigia kura kuwachagua watu ambao wanawataka kuwaongoza kwa kipindi maalum.

Uchaguzi ni utaratibu wa kawaida wa demokrasia wa kuwapata wawakilishi wa kisiasa ambao umekuwa ukitumika tangu karne ya 17. Kuna aina tatu za msingi za uchaguzi zinazotumiwa kuwapata viongozi kulingana na mfumo unaotumiwa na nchi husika.

Aina hizo ni uchaguzi wa Rais, Uchaguzi wa Wabunge na Wawakilishi katika Baraza la Kutunga Sheria na Uchaguzi wa Viongozi wa Serikali za Mitaa.

Vyama vya Siasa kwa upande wao navyo huendesha chaguzi ambazo zinajulikana kwa jina la “Chaguzi wa Msingi” zinazotumika kuwachagua wateuliwa wa vyama katika aina za uchaguzi ambazo zimetajwa hapo juu.

Endapo Tume haitaridhika kabla ya kutangaza matokeo ya uchaguzi kwamba kulikuwa na kutokufuatwa kwa taratibu, matumizi mabaya au ukiukwaji wa taratibu za uchaguzi au pale ambapo kura za wagombea waliopata kura za juu imelingana, Tume itasimamisha au kufuta uchaguzi au sehemu yoyote ya uchaguzi na itatangaza siku nyengine ya kurudiwa kwa uchaguzi huo.
  1. B

    GE2020 Tume iliwapotosha wagombea Urais nao wakapotoka?

    1. Mapingamizi yaliyowekwa na Lissu ni matokeo ya tafsiri mbaya ya sheria iliyofanywa na Tume, tume inaongozwa na Jaji na wasomi wa Sheria. Je, wanafanya Nini huko ofisini? Unapotoa misleading instructions kwa wagombea Urais si jambo dogo hata kidogo, si makosa ya kibinadamu haya bali ni makosa...
  2. Noel france

    GE2020 Kama leo haya yametokea kwa NEC, vipi kuhusu kesho Matokeo ya Uchaguzi?

    Kiukweli Tume ya Uchaguzi imekosa uhalali wa kuendesha uchaguzi huu. Habari zenu wanajukwaa wenzangu. Nasema hivi "NEC imepelea kwenye kujibu hoja za Tundu Lissu kizembe". Imekosa uhalali wa kuendelea kusimamia uchaguzi, kwasababu Inajipinga yenyewe na Sheria zake zilizopo ambazo zinaongoza...
  3. S

    GE2020 Maelezo haya ya Devotha Minja yanasikitisha, Tume ya Uchaguzi tunaomba muingilie na mtende haki

    Yanayoendelea Morogoro, Mwaka huu hakuna kupita bila kupingwa. Pole sana Devota.#NiYeye2020
  4. lee Vladimir cleef

    GE2020 Lengo ni kuwapata viongozi au lengo ni usahihi wa kujaza fomu?

    Tanzania ni Taifa la ajabu sana sijawahi kuona. Dunia inatushangaa na vizazi vijavyo vitakuja kutushangaa. Hivi lengo ni kuwapata viongozi au lengo ni usahihi wa kujaza FOMU? Kwanini imekua ni kama mtihani fulani hivi kwamba mtu akikosea kujaza FOMU anaondolewa kwenye nafasi ya kugombea? Kwa...
  5. Replica

    GE2020 Tume ya Uchaguzi yatupilia mbali mapingamizi ya Tundu Lissu. Magufuli na Lipumba ni wagombea halali

    Mkurugenzi wa Uchaguzi: Tume ya uchaguzi baada ya kupokea pingamizi dhidi ya wagombea hao, imewataarifu wawekewa pingamizi mapema iwezekanavyo na wahusika wamewasilisha utetezi wao. Pingamizi dhidi ya mgombea wa CUF kwamba hakurudisha fomu kwa mujibu wa masharti yaliwekwa na sheria, tume baada...
  6. S

    GE2020 Halima Mdee: Gwajima alijaza fomu ya maadili nyumbani kwake badala ya kuja mbele ya msimamizi wa uchaguzi hivyo hana sifa ya kugombea

    Kanuni ya 26(3) ya Kanuni za Uchaguzi zinataka Fomu ya KUTEKELEZA MAADILI kujazwa mbele ya Msimamizi wa Uchaguzi. Ndugu yangu wa CCM KAWE alijaza tarehe 20/8/2020 NYUMBANI kwake. Na BADO MSIMAMIZI wa UCHAGUZI Kinondoni AKAMTEUA!⁩ HUYU Mgombea HANA SIFA-Halima Mdee on twitter.
  7. Course Coordinator

    GE2020 Kwa mujibu wa Sheria ya Uchaguzi, aliewekewa pingamizi atajibu hoja mbele ya mweka pingamizi, Lissu na Magufuli uso kwa uso

    Kwa mujibu wa Sheria ya Uchaguzi namba 13 ya mwaka 2004 kipengele cha 48 mgombea aliewekewa pingamizi anatakiwa kwenda kujibu hoja mbele ya mgombea aliyemwekea pingamizi na kujibu hoja Sasa leo Mhe. Lissu amemuwekea mgombea mwenzake John Pombe Magufuli wa CCM pingamizi baada ya kushindwa...
  8. BAVICHA Taifa

    GE2020 Tundu Lissu awawekea pingamizi wagombea wawili wa nafasi ya Urais wa Tanzania. John Magufuli (CCM) na Prof. Ibrahim Lipumba (CUF)

    Taarifa kwa Vyombo vya Habari na Umma Mgombea wa Kiti cha Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Mhe. Tundu Lissu, akiwa pamoja na Mgombea wa Kiti cha Makamu wa Rais, Mhe. Salum Mwalim Juma Mwalim, muda huu wanaelekea Ofisi za Tume ya...
  9. M

    GE2020 Kama NEC inabariki ubakwaji wa haki ya Msingi ya Wananchi ya kuchagua na kuchaguliwa basi wananchi wataanza kudharau chaguzi na hii ni hatari sana

    Tunasoma kila mahali, watu wanafanyiwa michezo ya ajabu kwenye uchaguzi, kuna vyama vinavyolalamika wagombea wake kutekwa, kuna vyama vinavyolalamika fomu zao kuporwa, kuna watu wanalalamika wakurugenzi kutokutoa ushirikiano, wengine wanalalamika ofisi za Taasisi muhimu za Uchaguzi kufungwa...
  10. nivoj.sued

    GE2020 Mapingamizi ya Wasimamizi Uchaguzi Kata yatikisa Karagwe

    Mapingamizi ya Wasimamizi wa Uchaguzi wa Kata yameitikisa Wilaya ya Karagwe, mkoani Kagera, inayoongozwa na Mkuu wa Wilaya aitwaye Godfrey Mheruka. Kati ya wagombea 23, kuna wagombea udiwani 12 kutoka Chadema ambao wameenguliwa na Wasimamizi wa Uchaguzi wa Kata. Takwimu zinaonyesha kwamba...
  11. J

    GE2020 Tume ya Uchaguzi imevionya Vyombo vya Habari vinavyotangaza wagombea wamepita bila kupingwa Kinyume cha Sheria

    NEC imesema muda wa kutangaza wateule bado kwani kuna mapingamizi yanayoshughulikiwa na kwa mujibu wa ratiba mwisho wa kupokea mapingamizi ni leo 26 Agosti, saa 10.00 jioni. NEC imesema taarifa hizo zinaweza kupeleka uvunjifu wa amani Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Dk. Wilson...
  12. M

    Mambo 10 niliyojifunza katika zoezi la kujaza fomu na kupata uteuzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi kwa wagombea wa nafasi za Udiwani, Ubunge na Urais

    1. Vyama vya upinzani havikuwa na mkakati kabambe wa kuwasaidia wagombea wake kujaza fomu kwa usahihi. Mfn mgombea wa Morogoro mjini DEVOTHA MINJA hakuambatisha picha. 2. Wasimamizi wa uchaguzi waliongozwa na Sheria na kanuni katika kusimamia zoezi, licha ya baadhi ya wagombea kupanga...
  13. B

    GE2020 Mizengwe mizengwe ya nini Uchaguzi Mkuu?

    Uchaguzi ni mchakato unaoanzia kwenye kutia nia hadi angalau kutangazwa kwa mshindi. Watia nia na hata wapiga kura wote ni wana wa nchi hii hii. Fitina, ufedhuli, chuki, pepo wachafu wachafu, uchawi uchawi, uonevu nk vya nini wakati sisi sote tu-watanzania? Kweli haiwezekani kutendeana haki...
  14. Titicomb

    GE2020 Serikali Amkeni: Taarifa lukuki za kutekwa wagombea wa chama kimoja tu cha siasa zisizo na uthibitisho ni hatari kwa usalama wa taifa

    Kuna taarifa mpya ya kutekwa mgombea wa CHADEMA kwa ngazi ya UDIWANI na UBUNGE kila baada ya dakika chache ndani ya siku 5 za mwisho kuelekea siku ya leo tarehe 25/08/2020 ya kupitishwa majina ya wagombea na NEC. Nyingi ya hizi taarifa hazina uthibitisho kiasi kwamba zinaleta hofu kuna watu...
  15. USSR

    Kinana: Asikudanganye mtu hakuna Uchaguzi rahisi, kura ipo kwenye moyo wa mtu

    Wana JF, Muda mfupi mfupi uliopita aliyekuwa Waziri wa Ulinzi, Spika wa Bunge la Afrika Mashariki na Katibu Mkuu wa Zamani wa Chama changu cha Mapinduzi ametuonya kuwa hakuna Uchaguzi Mkuu rahisi hata siku moja kuwa kura ya mpiga kura ipo moyoni mwake. Akiwa hapa msibani Masaki kwenye msiba wa...
  16. Barbarosa

    Wagombea wa CHADEMA hawajui kujaza Fomu za Uchaguzi, hii kali

    Tundu Lisu yuko kila mahali, vitisho kila kona lakini anashindwa vitu vidogo sana kama tu kusimamia na kuhakikisha vinakwenda sawa, akina Halima Mdee wapo kila mahali kila siku Mahakamani kujifanya Wanasheria sasa kwa nini hawawasaidii wagombea wao? Wakati mwingine nafikiri chadema hata...
  17. J

    Ijue tofauti ya Kupita bila Kupingwa na Kupitishwa bila kupingwa kwenye Uchaguzi

    Moja kwa moja kwenye mada Kupita bila kupingwa ni pale inapotokea mgombea mmoja tu amejitokeza na kuchukua fomu na kukidhi vigezo vyote huyo anapita bila kupingwa Au endapo wagombea wengi wamechukua fomu na kukidhi vigezo lakini ndani ya muda uliowekwa kisheria wanaamua kujitoa ili kumpisha...
  18. Dam55

    GE2020 Hoja binafsi: Jaji Kaijage apongezwe kwa busara zake zilizombeba Tundu Lissu, busara zaidi itumike kuepuka sintofahamu za makusudi kwenye Uchaguzi

    Jaji Kaijage na team yake ya Tume ya uchaguzi kama si busara zao za kukubali kufanya uhakiki wa wadhamini wa mgombea urais Jamhuri ya muungano wa Tanzania kupitia CHADEMA Mhe. Tundu Lissu jambo ambalo kikanuni lilipaswa kufanyika kwenye ofisi za majimbo za Tume ya Uchaguzi basi ni dhahiri Lissu...
  19. Mtukudzi

    GE2020 Dhana ya kushinda Uchaguzi bila Kupingwa ni hatari kwa Usalama wetu

    Kushinda uchaguzi bila kuchaguliwa kwa kisingizio cha kupita bila kupingwa ni jipu ambalo yafaa litumbuliwe haraka ili kuleta usawa na kushamirisha amani ya Nchi yetu. Haiingii akilini kuwa mtu anaweza kutumia mbinu wazi au fiche kudhibiti washindani wenzake na kisha aonekane kuwa ni chaguo la...
  20. Sir John Deere

    GE2020 CHADEMA mna saa 24 kuanzia sasa kuweka pingamizi kwenye Majimbo mliyopoteza

    CHADEMA nawaasa kuanzia leo saa 10 jioni mna saa 24 tu za kupinga uteuzi kwa maeneo yote ambayo viongozi wenu wamekatwa kwa hila za CCM. Hakuna muda wa kupoteza shughuli ianze usiku huu huu sasa kama mtalala shauri yenu, wenzenu CCM hawalali. Mapambano bado yanaendelea!
Back
Top Bottom