Kinana: Asikudanganye mtu hakuna Uchaguzi rahisi, kura ipo kwenye moyo wa mtu

USSR

JF-Expert Member
Jul 15, 2015
4,516
2,000
Wana JF,

Muda mfupi mfupi uliopita aliyekuwa Waziri wa Ulinzi, Spika wa Bunge la Afrika Mashariki na Katibu Mkuu wa Zamani wa Chama changu cha Mapinduzi ametuonya kuwa hakuna Uchaguzi Mkuu rahisi hata siku moja kuwa kura ya mpiga kura ipo moyoni mwake.

Akiwa hapa msibani Masaki kwenye msiba wa Rais Benjamin Mkapa amewaambia wanahabari kuwa sio kuwa na mawazo ya uchaguzi rahisi maana yeye ameshiriki chaguzi zote tangu1995 akimsaidia marehemu Mkapa mpaka mwaka 2015 akiwa Katibu Mkuu wa CCM kwenye uchaguzi iliopitisha Rais Magufuli kuwa hakuna kutegemea uchaguzi mwepesi kwa kuwa haupo.

"Wanaweza watu wakajaa kwenye kampeni na wala wasikupigie kura, wanaweza wakaja ukadhani tayari ila sio wako hata wakikushangilia ni maneno tu maana kura hazikai mdomoni hukaa mioyoni"

USSR
 

Pohamba

JF-Expert Member
Jun 2, 2015
23,156
2,000
…kwa mara ya kwanza tunaenda kulinda Mapinduzi matukufu ya 1964 bila ya Mzee Mkapa…


Mshauri wa Dereva kamaliza safari… mliobaki sasa mfunge vyema mikanda na mtulie vitini…msilete hekaheka
 

tindo

JF-Expert Member
Sep 28, 2011
35,958
2,000
Kinana yuko sahihi, ila kwa sasa chini ya Magufuli box la kura haliheshimiwi, bali msimamizi wa uchaguzi anaagizwa amtangaze mgombea wa ccm kwa lazima.

Enzi za kina Kinana walikuwa wanaiba kura, ila sasa hivi kura haziibiwi, bali mgombea wa ccm anatangazwa kibabe kwa maagizo ya rais, bila kujali matokeo ni yapi.
 

Mikopo Chefuchefu

JF-Expert Member
May 15, 2017
3,399
2,000
Opinion poll = moyo wa mpiga kura.

Kwenye nchi zilizoendelea, zenye idadi ndogo ya wanafiki (anaowazungumzia Kinana). Final vote hushabihiana sana na Exit/ Opinion poll
 

USSR

JF-Expert Member
Jul 15, 2015
4,516
2,000
Kinana yuko sahihi, ila kwa sasa chini ya Magufuli box la kura haliheshimiwi, bali msimamizi wa uchaguzi anaagizwa amtangaze mgombea wa ccm kwa lazima. Enzi za kina Kinana walikuwa wanaiba kura, ila sasa hivi kura haziibiwi, bali mgombea wa ccm anatangazwa kibabe kwa maagizo ya rais, bila kujali matokeo ni yapi.
Toka 1995 mnapigwa tu sasa mmegeuzia kwa jpm .huko zamani mlikuwa mnashinda
 

tindo

JF-Expert Member
Sep 28, 2011
35,958
2,000
Toka 1995 mnapigwa tu sasa mmegeuzia kwa jpm .huko zamani mlikuwa mnashinda

Hatukuwa tunashinda, na ndio maana madai ya tume huru ya uchaguzi hayajawahi kukoma. Ila upinzani umeendelea kujizolea viti vingi vya ubunge kila muda unavyosogea kwenye mazingira hayo hayo. Kwa maneno marahisi upinzani umekuwa kama shoka dogo linalokaribia kuangusha mti mkubwa. Ila kinachoendelea chini ya Magufuli sio wizi tena, bali ni ubakaji wa wazi wa box la kura.
 

Titicomb

JF-Expert Member
Jan 27, 2012
9,114
2,000
Mfano ushindi wa Nyalandu kwenye kura za maoni za CDM.

Kwa jinsi Lissu anavyoshabikiwa wengi hawakutarajia kilichotokea kwenye zile kura.

Watu wasubirie uchaguzi mkuu, hii inawahusu nwogombea toka vyama vyote.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom