Uchaguzi 2020 Mapingamizi ya Wasimamizi Uchaguzi Kata yatikisa Karagwe

nivoj.sued

JF-Expert Member
Jul 14, 2009
221
190
Karagwe.jpg

Mapingamizi ya Wasimamizi wa Uchaguzi wa Kata yameitikisa Wilaya ya Karagwe, mkoani Kagera, inayoongozwa na Mkuu wa Wilaya aitwaye Godfrey Mheruka.

Kati ya wagombea 23, kuna wagombea udiwani 12 kutoka Chadema ambao wameenguliwa na Wasimamizi wa Uchaguzi wa Kata.

Takwimu zinaonyesha kwamba, kama uenguzi huu hautatenguliwa na Msimamizi wa uchaguzi wa Wilaya, basi CCM itaingia kwenye uchaguzi ikiwa tayari inao uhakika wa kuongoza Halmashauri ya Wilaya ya Karagwe, kwani kata 12 ambako wagombea wake wamepita bila kupingwa ni sawa na sawa na 52% ya kata zote 23.

Wasimamizi wa Uchaguzi wa Kata walikataa kuwateua wagombea wa Chadema bila kupokea pingamizi kutoka kwa wagombea wenzao. Yaani, kwa hiari yao wenyewe, Wasimamizi wa Uchaguzi wa Kata, waliamua kutafuta makosa, kuandika mapingamizi, na kutoa hukumu kwamba wagombea hao hawana sifa za kugombea.

Miongoni mwa tuhuma zilizoandikwa kwenye fomu ya kuwanyima uteuzi wapinzani ni pamoja na madai ya wadhamini pungufu, kujaza fomu vibaya, kukosea kuandika majina kwa kukosea herufi za “L” na “R.” Wagombea walioenguliwa wanapinga vikali tuhuma hizi, na kutojaza tamko la maadili ya uchaguzi. Wagombea walioongea na mwandishi wa habari hizi wanapinga vikali tuhuma hizi.

Kwa mujibu wa kauli za wagombea walioonekana wamekusanyika mbele ya Ofisi ya Msimamizi wa Wilaya ya Karagwe kata ambazo wagombea wake wameenguliwa ni Kayanga, Bugene, Ndama, Ihanda, Kituntu, Igurwa, Nyaishozi, Nyabiyonza, Kamagambo, Nyaishozi, Kihanga na Chanika.

Kata za Kayanga, Bugene, Ndama zinaunda Mji Mdogo wa Kayanga, ambako yanapatikana Makao Makuu ya Wilaya ya Karagwe. Wagombea wa Chadema walioenguliwa katika kata hizi za kimkakati ni kama ifuatavyo Kayanga ni Amos Kahwa, Bugene ni Deo Mtunzi, na Ndama ni Elineo Mpinzile.

Mwandishi wa habari hizi alishuhudia wagombea udiwani kutoka Kata hizi pamoja na viongozi wa Chadema Wilaya ya Karagwe wakiwa wamekusanyika nje makao makuu ya Wilaya, kusimamia rufaa zao walizoziwasilisha kwenye ofisi ya Msimamizi wa Uchaguzi wa Wilaya.

“Katibu wetu yuko ndani anaongea na Msimamizi wa Uchaguzi wa Wilaya,” kwa niaba yetu, alisema Deo Mtunzi, amgombea wa Kata ya Bugene.

Mtunzi anamtuhumu Mkuu wa Wilaya ya Karagwe, Godfrey Mheruka, kuhusika katika kuenguliwa kwake. “Alikuja jana kwenye ofisi za Kata ya Bugene, wakati tunarudisha fomu, huku akiwa ameambatana na maaskrari watatu na kunitisha,” Anasema Mtunzi.

Hata mgombea udiwani wa Kata ya Kayanga, Amos Kahwa, amemwambia mwandishi wa habari hizi kwamba, Mkuu wa Wilaya Mheruka pia jana mchana alifika kwenye ofisi za Msimamizi wa Uchaguzi wa Kata ya Kayanga akiwa amesindikizana na mapolisi kadhaa wakiwa na dhamira ya kujenga hofu kwa wagombea wa upinzani.

Aidha, Mgombea ubunge wa Chadema wa Wilaya ya Karagwe, Adolf Pelleus Mkono, amewekewa pingamizi na Mgombea wa CCM, Innocent Bashungwa. Mkono ameonekana makao makuu ya Wilaya akijibu pingamizi hilo linalodai kwamba anatuhumiwa kukwepa kodi.

"Nami nimemwekea pingamizi Innocent Bashungwa, mgombea ubunge wa CCM, kwa sababu yeye sio raia halali wa Tanzania, kwani ameishi Marekani na kupewa uraia huko, lakini hajawahi kukana uraia wa Marekani," anasema Mkono.

Mpaka saa 9.30 mchana, kikao cha kusikiliza rufaa hizi kinaendelea. Mwandishi atawaletea maamuzi ya kikao hiki mara yatakapotolewa.
 
Mwaka huu fireeeee yaani naoiona ccm(chama cha mafisi) yanaanguka kama jungu la ugari. Manake hakuna diwani msaliti kama 2015


Ndukiiiii 🏃‍♂️🏃‍♂️🏃‍♂️
 
Hii Ni kutii bosi, nimekuteua, Nakulipa mshahara, alafu utangaze wapinzani
 
Back
Top Bottom