Mambo 10 niliyojifunza katika zoezi la kujaza fomu na kupata uteuzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi kwa wagombea wa nafasi za Udiwani, Ubunge na Urais

Nov 27, 2019
35
145
1. Vyama vya upinzani havikuwa na mkakati kabambe wa kuwasaidia wagombea wake kujaza fomu kwa usahihi. Mfn mgombea wa Morogoro mjini DEVOTHA MINJA hakuambatisha picha.

2. Wasimamizi wa uchaguzi waliongozwa na Sheria na kanuni katika kusimamia zoezi, licha ya baadhi ya wagombea kupanga kuichafua Tume, rejea kitendo cha TUNDU LISSU kutokuhakiki wadhamini wake kwa wasimamizi wa uchaguzi wa jimbo husika na baadae kuzusha Tume inataka kumuengua.

3. Vyama Vya Upinzani vilikuwa na hofu isiyokuwepo 'Fear of Unknown' mathalani walitarajia wasimamizi wa uchaguzi wa majimbo wangefunga Ofisi kinyume chake Ofisi zilikuwa wazi kuanzia saa 1 asubuhi hadi saa 10 jioni.

4. Wafuasi wa vyama vya upinzani walichapisha baadhi ya taarifa za uongo kwamba wagombea wake wamenyang'anywa fomu zilizoleta hisia za uwepo wa uonevu kabla ufafanuzi kutolewa. Mathalani JANUARY MAKAMBA alilazimika kutoa ufafanuzi wa tuhuma hizo kwa kupiga picha ya pamoja na mgombea wa CHADEMA wakiwa katika Ofisi za msimamizi wakisubiri kurejesha fomu zao.

5. Baadhi ya wagombea walionesha ukomavu wa kisiasa ambapo waliweka kando tofauti za kisiasa wakapiga picha za pamoja kuonesha licha ya kuwa na vyama tofauti wote wanampenda MAMA TANZANIA. Rejea picha za MRISHO GAMBO na GODBLESS LEMA.

6.Baadhi ya Vyama Vyama vya Upinzani mathalani CCK vimeonesha havina dhamira ya dhati 'seriouz' na Uchaguzi. Haiingii akilini siku ya kurejesha fomu mgombea mwenza hakuhudhuria, pay slip ya malipo ya fedha ya dhamana haikukuambatishwa.

7. Baadhi ya wagombea walioenguliwa na wasimamizi kwa dosari mbalimbali wanatumia muda mwingi kulalamika mitandaoni badala ya kwenda mbali zaidi kwa kuwawekea mapingamizi wagombea waliopitishwa na kwenda kwenye vyombo vya haki kuwasilisha malalamiko yao.

8. Kitendo cha baadhi ya wagombea wa ubunge kupita bila kupingwa licha ya kuwa na uhalali wa KISHERIA, kwa mtazamo wa Demokrasia ya Vyama Vingi kinaleta ukakasi kwani inahitajika kuwepo kwa ushindani wa wagombea kabla ya mshindi kupatikana.

9. Baada ya Mhe. Rais DKt JOHN POMBE MAGUFULI, BERNARD MEMBE, TUNDU LISSU kupata fomu za uteuzi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi kutakuwa na mchuano mkali wa nafasi ya Urais, ingawa mgombea wa CCM ananafasi ku Mambo 10 niliyojifunza katika mikutano ya Tundu Lissu ya kutafuta wadhaminibwa ya kushinda kutokana na Uadilifu, uchapakazi, Uzalendo na udhubutu wake.

10. Ustahimilivu, utulivu na uungwana ulioonekana kwenye zoezi la kurejesha fomu na kusubiri uteuzi wa Tume unahitajika zaidi wakati wa Kampeni, kupiga Kura, kusubiri matokeo, kutangazwa washindi ili wataoshinda waje waendeleze kusukuma GURUDUMU LA UCHUMI WA KATI.

N.B
Wakulungwa kuna mitanange si ya kukosa:- Tulia vs Sugu, Gwajima vs Mdee

Leonard Isaya
Mchambuzi huru na mwandamizi wa masuala ya Siasa na Maendeleo.
 
Kwa hiyo umejifunza mambo kwa Upande wa Upinzania tuu Maswahibu yaliyowapata?


Kama nawe una shahada badi nchi hii imeisha
 
Mtaendelea kutetea ujinga mpaka mwisho wa maisha yenu ndio maana waafrika tunabakia katika lindi la umaskini kwasababu ya kutoona ushenzi wa serikali zetu na kuupinga.
 
Mitanange ambayo sio ya kukosa
Tulia vs sugu
Mdee vs gwajima
Heche vs waitara
Silinde vs mwakajoka
Kitila vs major boniface
Kimei vs mbatia
Gambo vs lemma

NB; kule kwa msigwa anapita bila kupingwa asubuhi tuu
 
Back
Top Bottom