Uchaguzi ni mchakato unaoanzia kwenye kutia nia hadi angalau kutangazwa kwa mshindi.
Watia nia na hata wapiga kura wote ni wana wa nchi hii hii. Fitina, ufedhuli, chuki, pepo wachafu wachafu, uchawi uchawi, uonevu nk vya nini wakati sisi sote tu-watanzania?
Kweli haiwezekani kutendeana haki wakati kila siku tuko kwenye nyumba za ibada ati kuomba, kuombeana na hata kuliombea taifa hili kheri?
Hivi ni Mungu yupi huyu wa kupokea hizi sala zetu wakati kimsingi sisi wenyewe tu-majahili na waovu wakubwa tuliotayari kutoana roho bila hata ya simile?
Inakera mno kusikia kuwa ati kuna mgombea yeyote kazuiwa kugombea tena ikiwa hata kwa mzengwe mzengwe tu. Au ati kuwa kawekewa pingamizi la kijinga jinga tu ili asipate fursa ya kufika kwenye sanduku la kura.
Jidanganyeni. Ila Mungu anawaona na ufedhuli wenu wote unaozijaza nyoyo zenu. Kumbukeni yote yana mwisho.
Hofu yote hii ya kuwahofia washindani wenu inatoka wapi kama kweli nyie ndiyo mnaofaa sana kwa (mema yenu) kuwa washindi?
Kwa nini pawe na wagombea waliopita ati tu kwa sababu wengine wote walienguliwa ili kuwawezesha hawa kupita bila kupingwa? Mambo mengine haya mbona ni ya kutia kinyaa kwa kweli?
Atasikilizwa mno mgombea yeyote atakaye kuja na agenda yenye muarobaini wa kuondosha hizi janja janja, ghiliba ghiliba na ufedhuli yaliofanywa kuwa ni sehemu katika michakato ya chaguzi.
Hata kama tumeishi katika chaguzi zenye ufedhuli wa namna hii, angalau basi wajukuu wa wajukuu zetu yasiwakute haya, inshallah.
Kwa nini isiwe kuwa jitihada zote zifanyike ili kuwawezesha wagombea wote kukamilisha nia zao za kugombea kwa halali tu?
Kwa nini kupata nafasi ya kutumia vyombo vya habari kujitangaza ihusishwe na uwezo wa mgombea kifedha?
Uhalali wa kufanya kampeni kupitia vyombo vya habari kuwa ni fursa ya kiuchumi kwa vyombo vya habari inatoka wapi?
Tutakula vipi 'ubwabwa' kwa mipangilio ya kunadi sera kwa pesa ki hivi?
Fursa sawa katika kampeni zinapatikana vipi kama pana vyama vyenye TV, radio, na hata magazeti yao hali habari za wengine zikiminywa waziwazi kama tunavyoona?
Enyi wenye mamlaka kwa hakika mjitafakari.
Mko nayo nafasi ya kurekebisha mambo na historia haitawasahau:
Pongezi Sirro, Mahakama na Tume ya Uchaguzi kazi kwenu