Mtukudzi
Senior Member
- Nov 14, 2013
- 103
- 408
Kushinda uchaguzi bila kuchaguliwa kwa kisingizio cha kupita bila kupingwa ni jipu ambalo yafaa litumbuliwe haraka ili kuleta usawa na kushamirisha amani ya Nchi yetu.
Haiingii akilini kuwa mtu anaweza kutumia mbinu wazi au fiche kudhibiti washindani wenzake na kisha aonekane kuwa ni chaguo la wapiga kura wote
Tumesikia mtu anauawa huko Ukerewe katika kile unachoweza kusema ni harakati za kutengeneza mazingira ya "kupita bila kupingwa". Hii ni hatari kwa usalama wa nchi.
Ifike wakati hata kama hakuna mgombea aliyejitokeza au wagombea wanakosa sifa basi tufuate utaratibu wa kura za Ndiyo/Hapana ili kuwadhibiti wagombea wetu na hatimaye kudhibiti amani na hatimaye kupata viongozi waliochaguliwa.
Imani yangu ni kuwa jambo hili lina umuhimu na ndiyo maana Mwalimu Nyerere hakuwahi kupita bila kupingwa hata kama hakuwa na mtu aliyejitikeza kumpinga. Alijua kuna wapiga kura wanaompinga. Si huyo tu hata Mwinyi, Mkapa, Kikwete na hata juzi Magufuli alipigiwa kura za Ndiyo/Hapana kwenye mchakato wa kuteuliwa kuongoza duru ya pili. Hata Mzee Sumaye huko Chadema alipigiwa kura za namna hiyo. Hiyo Ndiyo democracy ya kweli.
Tujitafakari sana kwa sababu kupita bila kupingwa ni bomu ambalo limeanza kuota mizizi!
Soma pia Kupita bila kupingwa - this too is democracy?